Ni Tume gani ya Rais huko Nyuma iliyosikilizwa na Serikali na mapendekezo yote kutekelezwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Tume gani ya Rais huko Nyuma iliyosikilizwa na Serikali na mapendekezo yote kutekelezwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 21, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tunaambiwa kuwa tuwe tayari kutoa maoni yetu kwenye hii tuma inayopendekezwa. Kwamba, watu wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao na maoni hayo yatakusanywa na kuratibiwa na baadaye kufanyiwa kazi. Wapo ambao wameshakubali prima facie kuwa kutoa maoni ndicho kitu tunachokitaka na kwamba kwa vile nafasi imepatikana basi watu watoe maoni yao halafu wasubiri kuona kitakachofuata.

  Nimebakia kufikiria na kutafuta mfano wa Tume ya Rais yoyote huko nyuma ambayo ilisikilizwa na Serikali kwa asilimia mia moja. Najiuliza ni tume ipi iliyoundwa na Rais ambayo ilikusanya maoni ya wananchi halafu maoni yale yakazingatiwa kabisa na kukubaliwa na serikali. HIvi, tume hii ikikusanya maoni ambayo serikali haitaki wananchi watafanya nini?

  Tume ya Nyalali (Chini ya Urais wa Mzee Mwinyi)- Tume hii iliundwa na Mzee Mwinyi kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu mambo mbalimbali yanayohusiana na demokrasia na sheria. Miaka ishirini baadaye, maoni ya Watanzania yaliyotolewa kwa tume hii hayakutekelezwa yote na mengine yalikataliwa na serikali.


  Tume ya Kisanga (chini ya Urais wa Ben Mkapa)- hii ilikuwa ni katika kufuatilia White Paper ya serikali na kama wengi wanakumbuka ripoti yake ilikataliwa na serikali kwa sehemu kubwa na kuwa ilienda zaidi ya kazi iliyotumwa kufanya. Baadhi ya mapendekezo yalifanyiwa kazi lakini mengine yalikataliwa kwa sababu serikali haikupenda maoni hayo. Prof. Peter Maina anaandika hivi kwenye mojawapo ya kazi zake kuhusu hili "The government kept its work, in an unprecedented fashion, after reading the report for a month and without releasing it to the public, the President decided to blast the Kisanga Committee for going beyond its mandate by making recommendations which were not in conformity with the views of the people [read here views of the government]. On his side, the Chairman of the Committee informed the press that he would not enter into a debate with the President and that the President was entitled to his own views and could pick whatever he found useful in the report. With this the whole momentum built through the work of the Committee was lost. That meant that another opportunity to meaningfully better the Constitution of the country was lost"

  Tume ya Bomani - kwa wanaokumbuka hii ni mojawapo ya tume ambayo iliundwa na RAis Kikwete (2007) ili kupitia sekta ya madini na kutoa mapendekezo yake. Tume hii - wengine tulipinga mapema - ilitarajiwa kuja na mapendekezo ambayo yangeweza kabisa kubadilisha mwelekeo wa sekta ya madini nchini na hivyo kutengeneza kile ambacho Rais Kikwete alikiita "win win win situation". Tume ilitoa ripoti nzuri na ya kufurahisha. Miaka minne baadaye mapendekezo yake kadhaa yamefanyiwa kazi na mengine ndiyo 'hivyo tena'.


  Kumbe tuna ushahidi wa kutosha wa kihistoria usiopingika kuwa Tume ya Rais ya kukusanya maoni haina maana kuwa maoni ya yatakayokusanywa yatakubaliwa kwani mwisho wa siku ni wao serikali (na siyo wananchi) ambao wataamua ni maoni yapi ya kuyakubali hata kama ni ya wananchi wengi. Kwa mfano, wengi tunafahamu kuwa uamuzi wa kuingia kwenye vyama vingi ulichukuliwa kinyume na matakwa ya wananchi wengi (asilimia 80 walitaka tuendelee chini ya chama kimoja). Je yawezekana Watanzania wengi walikuwa sahihi kuwa tungeendelea kwenye chama kimoja ila mabadiliko fulani muhimu yangetakiwa? Kama Serikali kweli 'inasikiliza' wananchi wake tungekuwa bado kwenye chama kimoja! Kwa ufupi ni kuwa serikali iliamua kukataa maoni ya wananchi na kuchukua maoni ya kikundi cha watu wachache. Yawezekana ndio chanzo cha mgongano uliopo sasa?

  Lakini baada ya kusema hayo swali langu linabakia. Je ni tume gani ya Rais ya kukusanya maoni huko nyuma ambayo ilifanya kazi yake na maoni yake yakasikilizwa na serikali bila kukataliwa au kupuuzwa? Kwa nini ni vigumu wakati mwingine kwa serikali kukubali maoni ambayo imeyataka kutoka kwa wananchi? Je, ni kwanini wapo wanaoamini kuwa katika "tume" hii ambayo inapendekezwa kwenye mchakato wa Katiba maoni yake yatasikilizwa na serikali wakati Sheria iliyopitishwa hailazimishi serikali kukubali maoni hayo ya wananchi?
   
 2. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Hakuna hata moja.
  Nitanakili maneno ya Einstein, “Insanity is doing the same thing, over and over again, but expecting different results.”
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanakijiji kwa maoni yangu nilidhani Kikwete ataitumia nafasi hii ya mchakato wa kupata katiba mpya na hivyo kuhakikisha mchakato wote wa kuipata katiba mpya unakubalika pia na vyama vya upinzani. Kikwete kwa kujua kwamba katiba hii si ya CCM au kikundi fulani cha watu wa chache ndani ya Tanzania angesimama imara kuhakikisha haki inatendeka kuanzia mwanzo wa mchakato mpaka mwisho ili kupata katiba ambayo itadumu kwa miaka mingi ijayo na hivyo kusaidia katika kupata Viongozi wa kuongoza nchi yetu bila kutumia ujanja ujanja au utapeli na pia katiba hiyo kusaidia kuleta maendeleo ya kweli katika nchi yetu ambayo yamekosekana kwa miaka mingi sasa.

  Kikwete kwa kufanya hivyo angejijengea heshima kubwa sana kwa Watanzania walio wengi bila kujali itikadi zetu za kisiasa na kuwemo katika historia ya nchi yetu kwa miaka mingi ijayo kwa kusimamia kwa haki mchakato mzima wa upatikanaji wa katiba inayokubalika na wengi.

  Kwa mara nyingine tena Kikwete amevurunda kama vile alivyovurunda katika siku za nyuma katika maswala ya EPA, Richmond/Dowans, kurekebisha mikataba ya uchimbaji wa madini yetu, Meremeta, Kagoda, uuzwaji wa nyumba za Serikali n.k. Kama kuna lolote baya litakalotokea katika mchakato wa kuipata katiba mpya kama vile vurugu na labda maafa kufuatia vurugu hizo au kupatikana katiba ambayo Watanzania wengi hawataikubali na hivyo kusababisha zoezi hilo lianze upya baada ya kupoteza muda mrefu basi atakayestahili kubebeshwa lawama zote si mwingine bali Kikwete.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  In addition, TUME YA RUSHWA ya JAJI WARIOBA, under Mkapa. was also a waste of Public fund.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Tanzania tunapenda sana kuunda tume?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280

  Dah! Ahsante sana Mkuu kwa kumbukumbu. Mkapa alianza kwa changa la macho Watanzania tukafurahia sana. Baada ya kukabidhiwa ripoti ile na Warioba akaamua kuiweka kabatini ikapigwa vumbi mpaka akamaliza awamu zote mbili hadi hii leo hatujui yaliyomo katika ripoti ile.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni njia rahisi ya kupoza mijadala inayosumbua fikra za watawala.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lakini kuna watu kabisa wanataka turuke ruke kuwa "tume itauondwa tukatoe maoni" kana kwamba tuna amnesia ya historia!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Watanzania hatuzipendi ila hawa waliokabidhiwa madaraka ndio huzipenda sana pamoja na kuwepo ushahidi wa kutosha kwamba matokeo ya tume zote hizo za miaka ya nyuma hadi sasa si ya kuridhisha hata kidogo.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hivi hakujawahi kuundwa tume ya kuchunguza tume? Manake sisi bana aaah...you can't put anything past us!
   
 11. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Japo Serikali ina Matatizo but Tatizo Kubwa ni wale wanaojipendekeza kwenda kutoa maoni ambayo hayatafanyiwi kazi!
  Katika Nchi za wengine hata wabunge husimama kidete kutetea mapendekezo ya Tume yanayolenga maslahi ya Taifa...But hapa kwetu ni zero!
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii judgment ni premature. Tukiwa waoga wa Tume kwa kuangalia huko nyuma basi hatutafika popote maana kuna maamuzi yamepata kuchukuliwa kwa kuangalia maoni ya Tume lakini siyo kila kilichopo kwenye ripoti ya Tume kinastahili kutekelezwa kwa sababu mengine yanakuwa prectically impossible to implement. Tuwe positive, siyo kusikiliza maoni ya wanaharakati ambao hawajui hata wanachokitaka.
   
 13. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  MM:

  Binafsi niliumizwa sana na mawazo ya wabunge wa ccm na CuF. Kwa waliofuatilia mjadala star tv jana pale moven pick watakuwa wameona jinsi wanasiasa uchwara wanavyoligharimu taifa hili kwa maslahi yao binafsi. Kina Mnyaa wameonesha njia. Haiwezekani CuF waliokuwa mstari wa mbele kupigania maboresho ya Muungano, na kupatikana kwa katiba leo wamegeuka vibaraka wa serikali ili kupata vyeo. Hii ni hatari.

  Wanaolazimisha tukubaliane na mawazo ya hovyo ya Raisi Kikwete kuwa ati katiba inampa mamlaka ya kuandika katiba mpya kinyume cha katiba aliyoapa kuilinda ni wendawazimu tu wanaoweza kukubaliana nao. Haya ni mawazo ya utawala wa 'kiimla' au wa 'kifalme' kwa maana ya ccm kujiona wao pekee ndio wenye haki na mamlaka ya kuongoza nchi hii hata pale inapothibitika pasipo na shaka yeyote kuwa wameshindwa kuongoza. Kama ulivyoeleza hapo juu, hakuna tume iliyowahi kuwasilisha ripoti yenye mawazo halisi ya wananchi kinyume na yale ya watawala ikakubaliwa. Hii ya katiba nayo haitakuwa na tofauti. Kama alivyosema JK, muswada kwenda bungeni ilikuwa kuhalalisha dhamira yake na wala haukuwa na lengo la kuwashirikisha wananchi. Hakuna haja ya watanzania kutoa maoni yao katika tume hiyo atakayounda kwani watakuwa wanapotea muda. Nukuu ya R.Einstein, “Insanity is doing the same thing, over and over again, but expecting different results.” We are not insane, we must prove that to the rulers.

  Kabla ya kusomwa kwa muswada bungeni, bwana mmoja aliyekaribu sana na waziri kombani alimuuliza waziri kwa njia ya simu: Nanukuu "Mbona mnatetemeka kuhusu muswada huu, mnaogopa nini?", Waziri akajibu; "Kwa upande wa serikali tunahofu mbili 1. Kuvunjika kwa muungano 2. Tukiwaruhu wananchi kutoa maoni yao na kuruhusu mchakato wa kukusanya maoni juu ya muswada huu CHADEMA watatumia mwanya huo kuwaelimisha watu na huo utakuwa mwanzo wa mwisho kwa ccm 2015".

  Mawazo hayo ya waziri yanathibitishwa na ukweli kwamba kamati ya bunge ilikwamishwa na spika kukusanya maoni ya wanachi katika mikoa 10 kama ilivyoagizwa na bunge. Kamti ya bunge haikupewa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake, hii haikuwa bahati mbaya. Spika na serikali walijua wanachofanya.
   
 14. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Are you insane?
  Robert Einstein said this, “Insanity is doing the same thing, over and over again, but expecting different results.”

  I hope you are not.

  Remember, History is one of the best teachers for mankind.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Unasema tume? mabomu yamelipuka Mbagalla na Gongo la Mboto na kuuwa watu hadi leo report imekuwa 'siri' Hivi utajisikiaje ndugu yako au mwanao au mzazi wake afe kwenye mabomu lakini hakuna mtu anakuambia kwa nini mabomu yalilipuka? Au nani alikuwa na makosa? Au sababu zilizofanya mabomu yakalipuka zimethibitiwa? Hili la katiba is nothing kama kwenye life/death situation rais anakaa kimya. Watu wameshaanza kusema hawataki urais wa kifalme, sasa ccm waruhusu kamati ya wananchi waondoe madaraka ya kifalme?
   
 16. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hizi tume zinatugarimu sana output yake inakuwa ziro. hapa kama hatutakuwa makini kuna wasiwasi wakukosa katiba mpya 2015, mfano huo mchakato ukifika wakati wa kupiga kura ya hapana ikashinda imekula kwetu
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  I wonder what was practically impossible to implement. Mara nyingi unapounda tume huwa unakubali kuwa kuna jambo hujui unataka kujua ili ufanye uamuzi na utekelezaji. Kama ukiunda tume, halafu unasema findings ni impractical then unatuachia maswali zaidi, kuliko unayokuwa nayo kabla ya kuunda tume.

  "Tatizo" kubwa ni kwamba wanapounda tume, kunakuwa na professionals na academicians. Ni bahati mbaya kuwa hawa watu sio wale wa ku-kiss ass, na wengi wanakuwa no-non sense people, especially wanapopewa uhuru na madaraka ya kufanya kazi zao. Ni tofauti na wanasiasa ambao kissing ass ni way forward in their political career.

  Kwa system yetu ya sasa, maamuzi yanayochukuliwa kutokana na mapendekezo ya tume ni sehemu tu ya mapendekezo mengi, na yanayochukuliwa hasa yale yanayolinda status-quo, sio yale yanayotaka kukabiliana na hali inayosababisha kuundwa kwa tume.

  Ukianza kuangalia unaweza kuona wazi kuwa mengi yanayoitafuna Tanzania kwa sasa, yalishawahi kupendekezwa kwenye ripoti za tume mbalimbali. Angalia Ripoti ya Nyalali, utaona kuwa mapendekezo yake yalihusu katiba, na ni ujinga kwa sasa kuunda tume kufanya kazi ambayo ilishafanyika. Angalia ufisadi, yote yaliyopo sasa yanatokana na kukaidi yaliyomo kwenye ripoti ya Warioba.
  Kwa hiyo ni simple, kama tume ina watu wenye uwezo na independent, no doubt kuwa yaliyomo yataachwa, ikiundwa na yes men na wanaopenda kukiss ass majibu tunayajua.
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MK utaacha lini kutumiwa na cdm ????

   
 19. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  kilichonifurahisha juzi na JK kukiri kushindwa hadharani kwa mara ya pili japo imekuwa ikiongelewa pembeni.
  Mara ya kwanza ni pale aliposema Mwalimu, Mwinyi na mzee Mkapa walifanya wakayaacha ....nami pia nitayaacha!
  Wakati yeye ndiye alitueleza wakati nakuja kuwa natakuwa tofauti na watangulizi wake kwa kuja na slogana ya "Kasi mpya ...."
  lakini juzi anarudi yaleyale kuwa Mwalimu, Mwinyi na Mkapa walifanya hivyo na yeye pia anafuata mkondo huo huo! Japo sikupenda kwa yeye kuifananisha serikari yake na za watangulizi wake ...hako nyuma angalau seriousness ilikuwepo kidogo ila wakati huu control ya muhimili huu imepwaya mno na inadhihirisha ilivyo vigumu kupata maoni ya katiba!
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ooh boy!
   
Loading...