Ni tukio lipi la ajabu zaidi ulilowahi kulishuhudia?

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,908
2,000
Wakuu wa jukwaa amani iwe nanyi.

Karibuni tushirikishane matukio ya ajabu tuliyowahi kushuhudia[siyo ambayo uliyotenda].
Binafsi nitasimulia kwa ufupi matukio ya ajabu niliyowahi kuyashuhudia ambayo imeniwia vigumu kuyasahau.

1.KUSHUHUDIA MTU AKIJINYONGA:
Wakati huo nikiwa mdogo [7] nilienda kutembea sehemu yenye miti na vichaka vingi.
Nilichuma peaches kwenye moja ya miti, wakati naondoka alikuja Kaka mmoja kwa kasi sana,
Nilikimbia nikidhani mwenye mti wa peaches amekuja kunikamata.Akiwa ameshikilia mfuko wa rambo nyeusi mkononi alinipita huku akiimba.......Pakistani zindaba.....Pakistani zindaba.
Alisimama na kupanda mti uliokuwa mbele yangu kidogo, akachukua kamba akafunga na kujivalisha kitanzi kisha akajitupa na kuning'inia hewani.
Alikufa kifo cha mateso sana, ulimi ulitoka nje nao ukaanza kuning'nia hewani.
Licha ya kwamba nilishuhudia tukio lote sikumweleza mtu hadi watu wengine walipomgundua siku mbili baadae.

2.NG'OMBE KUZAA NDAMA MWENYE VICHWA VIWILI:
Ilikuwa kwenye shamba la mkulima mmoja, ng'ombe alizaa ndama mwenye vichwa viwili, vyote vikifanya kazi kama kawaida mf. kulia, kuhema, n.k.
Ndama hakuwa na tatizo lolote isipokuwa vichwa viwili na shingo moja iliyotengeneza 'Y'-Shape.
Tukio lilishangaza wengi lakini baadae kidogo mwenye shamba alimuua yule ndama kwa kugonga vichwa vyote viwili kwa shoka.

3.NDOA YA KAKA NA DADA:
Hawa walikuwa ndugu wa damu kabisa, watoto wa Baba mmoja na Mama mmoja,
Dada ndiye mkubwa kuliko Kaka mtu.Walifanya maamuzi ya kuishi kwa pamoja kama mume na mke.Familia, ndugu na baadhi ya marafiki walilaani sana kitendo walichokifanya lakini wao walitilia mkazo maamuzi yao kwa kusema wanapendana sana kiasi cha kufikia hatua ya kuoana.
Wamewahi kusema mahusiano yao ya kimapenzi yalianza tangu wakiwa utotoni bila kugundulika na sii rahisi kuachana.
Kwa sasa wana familia yenye watoto wawili na maendeleo makubwa pia.

Yangu ya ajabu[Baadhi] niliyoyashuhudia ni hayo. Wadau ni matukio yapi ya ajabu uliyowahi kuyashuhudia?.....Karibuni tujuzane.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom