Ni Tukio/jambo gani limewahi kukutokea ambalo hukuwahi waza/ tegemea kama lingekutokea

mzado

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
1,013
1,483
Habari wananzengo,

Karibuni tushirikishane japo kwa ufupi yale tumewahi kukutananayo katika maisha ambayo kimsingi hatukuwahi tegemea au tarajia kwamba tungepitia/kuyapata kwa wakati huo, liwe la kufurahisha, kheri au lakusikitisha lengo ni kupeana expirence, mafunzo na burudani.

Binafisi nitaelezea matukio mawili.

La kwanza ilikua ni kuondokewa na Baba mzazi (Mshua msater), mshua alikua mtu mwamba na mpiganaji sanaa, katika kumbukumbu zangu hakuna siku aliwahi kushinda nyumbani (nadhani ndio wale wa ridhiki ya mbwa ipo miguuni pake) au kuugua akalazwa, mzee alikua mtata na suala la kufokewa au kichapo ilikua ni kugusa.

Alikua na pikipiki yake mtaa mzima walikua wamekariri mlio wake yani ulikua ukiskia mlio wa pikipiki kama upo mbali na home hapo ni unatimka nduki mpaka home na wakati huo waliopo home wakisikia mlio wa pikipiki ni hekaheka kuhakikisha kilakitu kinakaa mahala pake na tunakaa attention, hilo halijalishi unaumri gani as long as upo kwenye himaya yake unapaswa kutii, tulikua extended familly, alitamani tupate future bora kupitia elimu jambo lililopelekea kukatisha ndoto yangu yakuwa mchezaji.

Mshua alifariki kwa ajali, siku anafariki ilikua ndio tarehe yakwenda kuanza kibarua kipya baada ya kumaliza chuo by then home mambo yalikua magumu mno, mimi ndio first born na nilikua mkoa wa mbali, yani napata taarifa ya msiba nakufungasha virago vyangu kurudi home kupambana, sikutegemea kama angeondoka wakati inaonekana tunamuhitaji the most, sikuwahi waza kama mtu imara namna ile angeondoka katikati ya mapambano, sikuwahi waza kama ningejikuta nalia kwasababu yake,

Kubwa zaidi sikujua namuhitaji na nampenda kiasi kile na kwa umati uliojitokeza sikujua kama anaconnection kubwa namna ile, umati mkubwa kiasi chakupelekea baadhi ya barabara kufungwa.
The man was Great.

Tukio la pili ilikua ni kufaulu kidato cha nne,

Nakumbuka matokeo yametoka mida ya usiku tumejikusanya kwenda internet cafe, kufika tunakuta shazi, bahati nzuri tunakutana na washkaji wamelipia lisaa, ikawa mtandao ukikubali tunataja shule wanafungua unatafuta namba yako ukijiona unasepa.

Nakumbuka nilijiona na Dv III ya mwanzo na combi zilibalance, sikuamimi, sikutegemea pia sikushangilia, nilirudi home nkawaambia wazazi, kesho bimkubwa alipika pilau kunipongeza.

Binasfi sikuwahi penda shule na hili halikua siri, though sikuwahi feli lkn nilikua mtu wa michezo mno, wale wanafunzi wakupata wastani wa "C" sikumbuki kama niliwahi vuka au kushuka hilo daraja, hata nafanya mtihani wa NECTA sikuwa nimejianda vizuri ilikua ni mimi na mamichezo, lakini baada ya kumaliza na kukaa mtaa ndio nikawa nawaza na kutamani kufaulu, si kwaajili yangu bali kwaajili ya wadogo zangu yaani kuwaonesha njia "maana mm ndio mkubwa hivyo nilipaswa kufungua njia" maneno ya wazazi hayo ambayo nilijikuta nayaishi,

Namshukuru Mungu nilitoboa na huo ufaulu, lkn baada ya hapo niliamua kuwa mfungua njia kwa madogo kiukwelikweli.

Karibuni nanyi mtupie mzoefu..
 
Sikutegemea kama ningepata mtoto mwengine sikutegemea nasikutaka aiseee....lakin chakushangaza nampenda mno my handsome little boy h
 
Mie sikutegemea kabisa kuwa nitafukisha miaka 42 sina mke mtoto na ninaishi kwa matumaini baada ya kuunganishwa grid ya taifa
Pole sana mkuu, kama hutojali unaweza ukaelezea kidogo ilikuaje, tujifunze na kushauri pale tutakapoweza..
 
Tukio langu ni kuahirisha mwaka chuoni sababu sikupata mkopo aisee lile tukio sitakuja kulisahau. But Mungu mwema mwaka uliofuata nikaomba nakupata course ya ndoto yangu now ninatumikia Taifa.
Hongera chief, hii pia ilinitokea lakini hata baada ya kuomba tena bado sikufanikiwa lkn Mungu ni mwema mno.
 
Back
Top Bottom