Ni tukio gani hutalisahau katika malezi ya mtoto kuanzia age 0?

Nakumbuka wangu akiwa na miezi kama mitano hivi, mtoto wa mpangaji mwenzangu akaja kumchukua ambebe bahati mbaya mtoto akajigonga, akawa anatoka damu mdomoni.
Sikuweza hata kumshika, mwili ulikuwa kama unatetemeka huku namuangalia kwa huruma.
Akaja jirani kumchukua, akamuosha kwa maji ya vuguvugu na chumvi kidogo.
Hilo ndio tukio pekee lililofanya mwili wangu upate ganzi mpaka sasa anaelekea miaka minne.
 
Mimi mwanangu ndio alikuwa ametimiza siku 7 yaani wiki toka azaliwe. Usiku saa 6 nimemnyonyesha nikamlaza ile nageuka nakuta anatoa maziwa na mapovu mdomoni na puani. Mungu tuu anajua vile nilichanganyikiwa. Usiku huo huko tukatoka na baba yake kumkimbiza hospitali umbali mrefu sana ( Kiseke hadi kamanga hospital Nyegezi) wenyeji wa Mwanza wanajua umbali wake. Watoto wana changamoto sana jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiseke hadi Nyegezi!!! Mbona mlipapita mjini kati sasa kwenye hospitali nyingi na bora?
 
Watoto wadogo kuwalea inahitaji umakini sana. Ndiyo mana mama mwacheni aitwe mama tu. Kama mtt mchanga ukikosea tu wkt wa kumnyonyesha unaweza kumuua kwa kumziba pua zake kutokana na jinsi ulivyoliweka ziwa lako. Au akapaliwa maziwa.

Na pia wkt wa kumuogesha kuna mtindo wake wa kumuogesha ukikosea tu bs umeharibu na umemsababishia matatizo mtt. Akiwa mdg hujui km anaumwa nini maana hasemi. Lkn mama unatakiwa ukisie apa mtt anaweza akawa anaumwa ichi au ichi. Mama ni mama asikwambie mtu.

Mimi mama angu ana alama mpk leo niliomsababishia mimi wkt wa kuokoa maisha yng. Tena almanusura apate ajali. Na mie mwenyw mpk leo nna alama kwa paja sbb ya iyo ajali. Hajasahau mpk leo. Nampenda sn mama angu.

The Most Winner
Pole kwa changamoto ya ajari ila Mungu aliepusha wazaz wawe makini kwa kipindi hiki cha umri Mdogo wa mtoto.
 
Pole kwa changamoto ya ajari ila Mungu aliepusha wazaz wawe makini kwa kipindi hiki cha umri Mdogo wa mtoto.
Ni kweli. Ila si unajua tena mtt ndiyo kakata moto, mama ndiyo uko peke yako ndani. Unachanganyikiwa hujui pa kuelekea. Acha kabisa. Mama angu alitoka peku peku mimi mkononi.
 
Mimi mwanangu ndio alikuwa ametimiza siku 7 yaani wiki toka azaliwe. Usiku saa 6 nimemnyonyesha nikamlaza ile nageuka nakuta anatoa maziwa na mapovu mdomoni na puani. Mungu tuu anajua vile nilichanganyikiwa. Usiku huo huko tukatoka na baba yake kumkimbiza hospitali umbali mrefu sana ( Kiseke hadi kamanga hospital Nyegezi) wenyeji wa Mwanza wanajua umbali wake. Watoto wana changamoto sana jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole.Hukumcheulisha ndo mana.Inatakiwa kila unapomaliza kumnyonyesha mtoto muweke begani kumcheulisha atoe gesi.Mi hii ilinitokea Kwa mtoto wangu nikiwa bado hosp.nesi akaniambia huyo mtoto hujamcheulisha kwanini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi juzi juzi tu namwogesha Sasa nikawa nampaka sabuni kichwan nikamwagia maji kwann kasivute maji yale mtu akaanza kukohoa Mara kakakamaa anahema juu juu nilichanganyikiwa machozi yananitoka sijui nifanyaje Niko pekeangu alivyokuja kutulia nilijikuta natetemeka, nikumvutaga kumvesha tu nguo, Hapo Ana umri wa mwez. Mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe unaweza kumnyonya puani. Sasa ilichanganya na kupaliwa halafu mtoto mwenyewe muoga hatari anahangaika hakuna Mfano . Nilishauriwa kwamba mtoto hapaswi kuogeshwa Mara tu anapomaliza kulishwa au kunyonya unapaswa kumpumzisha Kama nusu saa au saa moja hivi ndipo aoge, na lingine la kuzingatia ni kumcheulisha mtoto kila baada ya mlo

Hii mada itatufunza mengi sana.

Unafanyaje ili acheuwe?
 
Pole.Hukumcheulisha ndo mana.Inatakiwa kila unapomaliza kumnyonyesha mtoto muweke begani kumcheulisha atoe gesi.Mi hii ilinitokea Kwa mtoto wangu nikiwa bado hosp.nesi akaniambia huyo mtoto hujamcheulisha kwanini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli sikuwa nimcheulisha ila nilichanganyikiwa sana. Na unajua kutokujua maana ndio alikuwa mtoto wa kwanza vitu vingi vinakuwa vigeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nikiwa nimerud hme kichanga kimelazwa nishasahau kama kuna kichanga, sinikajitupia dah! naskia tu kinalia nilihisi nimeua bt mungu ni mkubwa sana wakuu.. watoto hulindwa na malaika wa mungu coz kama sivyo kichanganya kisingepona maana kilo zangu 75 zililala juu ya kichanga, hadi leo hua siamini na nikikasimulia hua tunacheka tu


Qn
 
Matukio mawili yanahuzunisha

1. Dogo alivyofikisha wiki tatu tu, tangu azaliwe akaanza tabia ya kulia usiku. Alikuwa anaanza kulia saa nne hadi saa Saba usiku kila siku hadi alipofikisha miezi sita. Ilikuwa inahuzunisha sana. Tulikuwa tunabembeleza nyumba nzima, kuanzia mama, baba, dada wa kazi , bibi na hata babu( mke wangu alikuwa kajifungulia kwao)

2. Kuna siku alipofikisha mwaka , akaumwa sana homa, na joto likawa halishuki. Nikaenda nae hosp usiku, naona Dr wa zamu anamzamisha kidonge cha matakoni ili kushusha joto. Nilishangaa sana, yaani nikajisemea mbona mwanangu, tena wa kiume anafanyiwa hivi bado mdogo sana. Medical officer incharge akaniambia worry not, tunashusha Joto, Joto liko juu sana, na hii ikizidi itasababisha matatizo mengine. Na hapo dogo ana siku ya pili, kila anachokula anatema( hakikai mdomoni).Niliumia sana. Lkn baaada ya kama siku nne hv , nakutumia dawa, alikuja akapona.

3. Mwanangu mwengine wa mke wa pili, huyu ana blood group( Ni either O Au A hapa huwa nachanganya kila siku) ambayo alirithi kwa mama yake soon baada ya kuzaliwa. Sasa kuna siku aliumwa sana tukampeleka hosp usiku, kwa bahati mbaya sana , hatukujua kuwa wenye blood group hiyo ( na hasa mwanangu) huwa wako allergic na dawa zenye sulphur. Basi akaaandikiwa Dawa zenye sulphur, kilichotokea tumerudi home, baada ya km siku mbili hv, tunashangaa ugonjwa unazidi badala ya kupungua. Aisee Nilichanganyikiwa mno. Na hii ilipelekea hadi kulala usiku mzima kuguza mm na mke wangu. Tuliumia sana. Nilipoamka asubuhi , ilibidi tumpeleke kwa specialist wa watoto, yuko mmoja pale k/koo anaitwa Dr hameer, akampima na kucheki blood group na dawa alizopewa akasema, huyu yuko allergic na hizo dawa , Ambazo pia zinasababisha Immnunity yake kushuka. Tangu siku hiyo, ndio akawa Dr wetu wa huyu mtoto, na akiumwa tu, huwa tunampeleka hapo, na hatibiwi sehem nyingine yoyote.


Ulezi changamoto sana. Kwa wale ambao wazazi wetu wako hai, Tuwapende mno. Huwezi jua thamani ya wazazi kama na wewe hujaanzisha Familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom