Ni **** Tu Ambaye Haambiliki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni **** Tu Ambaye Haambiliki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, May 19, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni **** Tu Ambaye Haambiliki!

  SAFARI moja **** alikaa mwisho wa tawi la mti, akilikata tawi hilo kwa kutumia msumeno. Akapita mtu mmoja akamtahadharisha kuwa kitendo alichokuwa akikifanya ni cha hatari. Alimwambia kuwa lile tawi likikatika naye ataanguka! Alimshauri akae kwenye shina la tawi atanusurika.

  **** hakutaka kabisa kusikiliza ule ushauri aliopewa. Alimgeukia yule mtu na kumwambia, "Wewe imekuhusu nini? Nikianguka, mimi ndiye nitakayeumia! Hebu achana na mimi, shika njia uende zako!"

  Yule mtu, ingawa alikuwa ana hakika kuwa **** ataanguka tu, lakini hakuwa na njia ya kumzuia. Akaona bora aende zake. **** alipomwona anaondoka akaaanza kumpigia kelele, "Mtanzameni huyo. Hana analolijua isipokuwa kuwaombea wenziwe mabaya tu".

  Yule bwana akajifanya kama hakuwa akiyasikia yale aliyokuwa akiambiwa. Lakini alikuwa akisema moyoni, "Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu!"

  Kabla hajafika mbali akasikia kishindo na mayowe yakipigwa. Alipogeuka akamwona **** yuko chini na lile tawi la mti limwelemea juu yake. Anapiga kelele kuomba msaada. Basi yule mtu akawaita wapita njia, wasaidiane kumwokoa ****. Walifanikiwa kumnusuru, lakini **** alikuwa ameumia kiuno!

  Yule mtu akamwuliza ****, "unalia nini? Ungelisikiliza maneno yangu yangalikufika haya?" **** akajibu, "kweli ningalikusikiliza uliyoniambia nisingalianguka! Lakini mimi sikuwa nikijua kuwa wewe una ujuzi wa kutabiri mambo yajayo, ndiyo maana niliudharau ushauri wako. Kwa vile sasa nimeelewa kuwa wewe ni bingwa wa kutabiri basi niambiye na siku yangu ya kufa!"

  Yule mtu akastaajabu sana kwa swali hilo. Akamwuliza ****, "Tokea lini mtu akaweza kuagua siku ya kifo cha mtu mwengine?" **** akamjibu, "Mbona ulitabiri kuwa ningeanguka, na kweli nikaanguka? Basi hapana shaka, na siku yangu ya kufa unaijua!"

  Yule mtu ilipombainikia kuwa yule hakuwa **** wa jina tu, bali hata wa vitendo, aliamua kumwacha kama alivyo, na kuendelea na safari yake.

  Kisa hiki si cha kweli. Ni katika zile hekaya za Abunuwasi. Ni hadithi za PAUKWA, PAKAWA! Lakini ni kisa chenye mazingatio makubwa kwa wale wenye kutaka kuzingatia watazingatia. Basi ndugu zetu mnao itwa vyama vya upinzani shikeni maneno haya kwa kuungana pamoja ili msije mkaanguka kama **** yule, msije sema kuwa hatuja waambia. Mkaja mbio kwetu kutulilia kuagua vifo vyenu.
  ..Unganeni sasa maana jiti mnalotaka kuling'oa lina mizizi migumu kushinda mti wa mpingo kama si m-buyu.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tatizo kuna wenzetu wengine wabinafsi, hawaambiliki...ruzuku inawatoa roho...ipo haja kweli kwa vyama vya upinzani kukaa na kupanga stratejia za ushindi walau kwa viti vya ubunge ili tuwe wengi bungeni, inafaa tuwe na mkakati hasa wa maeneo yepi tukishirikiana ni rahisi kupambana na chama tawala kwenye uchaguzi mkuu, huu un'ga n'ganizi wa kujidai unakubalika wapi na wapi sijuwi hauna maana sana wakati huu, wenzetu wa Congeress kule India walipoli'ngamua hili haikuwachukuwa mda kuwaondoa BJP na kurejea madarakani .
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wagombea wengi ni waroho wa madaraka, hao wanao dai kuwa wanakubalika kwani hayo majimbo ni sawa na familia zao mpaka washindwe kuwaachia wengine? Ni kutokuwa na uzalendo wa kweli, na kama wakishindwa kuungana kila baada ya miaka mitano chama kitachochukuwa kura nyingi kitabakia hicho hicho chama tawala.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ukweli ni kwamba kitu chochote hata kikiwa kizuri kiasi gani, kikichanganywa tu na ubinafsi basi kinakuwa shubiri na nia njema hutoweka. Mifano ni mingi. Mfumo wetu tu wa utawala na kuchaguana uongozi umejengwa juu ya ubinafsi. Na ndio maana watu wanaenda ktk magenge yao ya ubinafsi yanyoaitwa vyama vya siasa. Lakini ukiwauliza haswa sababu ya wao kuwa ktk hivo 'vyama' au awali tu uwepo wa hivo vyama , sababu watakazotoa utashangaa na unaeza kufa kwa kihoro. Kwa sababu ya kutokuwa na nia njema ndio siri ya wizi wa kura, kugombania madaraka, na vitimbi vingine vinavyokutanika kwenye haya magenge ya kihalifu yanaitwa vyama vya siasa, CCM ikiwa kinara.

  Nilishawahi kuuliza siku za awali kwamba kama uongozi ni utumwa au utumishi kwanini basi watu wanag'ang'ania kuwa viongozi ilhali 'uongozi' wao unazidi kutudidimiza ktk lindi la umaskini siku hadi siku kwa zaidi ya miaka 40 tangu uhuru. Ukweli ni kwamba kitu kiitwacho uongozi ktk nchi yetu si utumishi bali ni ujangili na ujambazi. Sababu upatikanaji wenyewe wa hawa majangili umejengwa kwene misingi iliojaa ubinafsi left and right plus many other wrong reasons. Unless we understand in principle what we need to tackle tutaendelea kila siku kuongelea jambo lilelile over and over.
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  heshima Mkuu.....wenye macho wasome............siku hizi waambie 'karibia miaka 50" tangu uhuru...........
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  May 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kuungana kivipi hebu fafanua tafadhali..
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nimekusoma kiongozi..Miaka yaenda kasi ..
   
Loading...