Ni taifa gani kati ya haya ambalo limekuwa na mchango mkubwa zaidi Duniani katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa muda wote na kwanini?

Huu uzi ni wa muda mrefu kidogo. Nimekuwa 'bize' sana kiasi kwamba nimeshindwa kufuatilia michango ya members.

Baadhi ya wachangiaji wamejibu vyema kwa kutaja nchi kama ambavyo swali liliuliza pamoja na sababu za msingi za kuitaja nchi husika. Hongereni na asanteni!

Ila, wapo wengine waliotaja nchi tu bila kutaja sababu mahususi. Kama ni mtihani, hapo tayari kuna maksi nyingi zimepotea kutokana na kushindwa kujibu swali vyema.

Hata hivyo, nanyi asanteni pia!
 
• WAGIRIKI / WAYUNANI

√ Elimu hasa ya darasani kwa dunia hii na Mifumo yake tangu utotoni mpaka Uzeeni (Elementary Education) kuhusu Saikolojia ya Binadamu, Falsafa ya ndani kabisa, na Matibabu

• WAISRAEL

√ Kilimo, Ubunifu na Ugunduzi wa Viwanda mbalimbali vikubwa duniani kote pamoja na silaha za kivita

• WALATINI YAANI WARUMI na nchi zake hasa ITALY, SPAIN & FRANCE

√ Uendelezaji na Uekezaji wa Elimu ya Wagiriki wa kale (Ancient Greeks) pamoja na Mapinduzi ya Uhandisi wa Majengo, hasa Makanisa, Shule, Barabara, Madaraja na Nyumba Imara na bora za kuishi

• WAMISRI WA KALE /ANCIENT EGYPTIANS

√ Uhandisi wa makaburi ya mapiramidi ya kudumu, Matibabu na Utawala


• WACHINA WA KALE / ANCIENT CHINESE

√ Matibabu na Madawa


• WAINGEREZA YAANI GREAT BRITAIN (GB) & OTHER GERMANIC NATIONS KAMA GERMANY YENYEWE

√ Kwa Modern world Baadae around karne ya 16 mpaka leo hii hawa wali take Over, wakaasisi Mapinduzi ya Viwanda vikubwa sana na Ugunduzi wa Umeme. Viwanda vya Magari, Meli, Treni, Vifaa vya Umeme, Drillers, Millers na Uongozi bora pamoja na Sheria hasa ile Magna Carta

• USA, JAPAN, KOREA, RUSSIA & TURKEY

√ Waliendeleza zaidi walichoanzisha Waisrael, Waingereza na Wajerumani ila USA na RUSSIA wakaenda mbali zaidi kugundua usafiri wa Anga (Aircrafts), Internet na Silaha kali za kivita


• ISRAEL, HOLLAND

√ Kilimo cha kisasa na Ufugaji

Ahsante kubwa zaidi kwa Waingereza na Wamarekani kwani Sayansi, Elimu, Utawala, Sheria na teknolojia yao ndio tunayoiishi hata sasa, ambapo China na India nazo zinasambaza.

.........XXX.........XXX.........XXX.........XXX......
Shukrani sana kwa mchango wako. Ingawa, umetaja nchi ama umetoa majibu mengine ambayo hayako ndani ya mipaka (scope) ya swali.

Asante!
 
Mbona Misri, Ethiopia, Sudan na Zimbabwe hutaji ukiachia mbali Mali kulikokuwa chuo kikuu maarufu kwenye mji wa Timbuktu?
Huu uzi ni wa muda mrefu kidogo kama ambavyo nimesema.

Swali liliulizwa hivyo kwa wakati huo kama ambavyo linaonekana. Lakini, haimaanishi kuwa hizo nchi nilizozitaja ndizo nchi pekee duniani zenye mchango wowote ule katika mandeleo ya sayansi na teknolojia. Pia, nilisema kuhusu hilo kabla hata ya kuuliza swali kuu.
 
Sijaelewa mantiki ya swali lako,

Inavyoonesha jibu unalo na linafahamika,

Kumbuka nchi nyingi Zina michango hapa duniani,ila tofauti ni idadi ya michango,

Ukifanya utafiti ukawakusanya watoto wote wa darasa Fulani wa shule za misingi mfano wote wioshika nafasi ya kwanza katika mwaka Fulani ukawapa mtihani ni lazima atapatikana wa kwanza na WA mwisho.
Lkn haimaanishi wa mwisho ni kilaza.
Hivyo katika orodha ya hizo nchi ulizozitaja yupo atakaeonekana ana mchango mkubwa na mwingine mchango mdogo.

Kumbuka watu wote hatufansni mahitani.

Hatufanani changamoto.

Na hizi ndo chanzo Cha maendeleo.

Sasa najibu,Uingereza Ina mchango mkubwa kuliko wengene uliowataja.
Umetaja nchi tu bila ya kutoa sababu zozote zile za kuitaja nchi husika.

Pia, jaribu kutumia muda mwingi zaidi kujikita katika kujibu swali ama hoja, tumia muda mchache sana katika kuzungumza masuala mengine tofauti na kile kilichoulizwa.
 
Back
Top Bottom