FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Habari!
Taifa ni watu na tunapozungumzia mchango wa taifa katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia tunamaanisha jitihada za watu katika taifa husika katika kulitekeleza hilo.
Katika historia kuna watu wengi maarufu kutokana na vipaji pamoja na maarifa waliyokuwa nayo hapo zamani yaliyokuwa chanzo kikubwa cha mabadiliko mbalimbali ya kimaisha katika dunia yetu ambao wengi huyaita 'maendeleo'.
Watu kama vile Isaac Newton, Albert Einstein, Galileo Galilei, Aristotle, Leonardo da Vinci, Johannes Kepler, Marie Curie, Michael Faraday, Archimedes, Nikola Tesla, Alexander Graham Bell, Thomas Edison, James Watt ni baadhi tu.
Kuna mataifa mengi ambayo kwa umoja wake yamechangia katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia lakini kwa sasa tuzungumzie mataifa haya manne ya barani Ulaya yenye historia ndefu sana.
1) BRITAIN (Uingereza)
2) FRANCE (Ufaransa)
3) GERMANY (Ujerumani)
4) ITALY (Italia)
Kwa maoni yako, ni taifa lipi kati ya hayo ambalo kwa muda wote limekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Kisayansi na Teknolojia tuzitumiazo hivi sasa na kwa sababu zipi?
Karibu!