Ni tabia zisizopendeza na za aibu kwa 'Ke' asiyestahiki katika maisha yako

Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
3,240
5,245
Habari wana JF,

Nimekuwa nikiishi na mshua na mama yangu wa kambo kwa kipindi kirefu sasa yapata miaka 14 sasa,tokea marehemu mama apate kufariki.
Huyu mama amekuwa akifanya mambo ya ajabu ajabu ambayo kiukweli hayaridhishi.

Hafui wala kufanya usafi wa nyumba ni mchafu,ana mambo ya kiswahili mno na ni mpenda sifa anatuchoresha kwa watu,ukileta vitu home toka safarini kama michele anagawa kwa watu,ni mchoyo na ana roho ya kwanini,ana gubu sana yani ni mchochezi na anapenda ligi kwa vitu vya kijinga,anatabia ya kutuharibia kwa mshua ili tuonekane wabaya.

Ameharibu vyombo na kuvigawa vitu vya marehemu maza ilihali yeye hana vyombo zaidi ya vikombe vya plastiki na masufuria,hapendi maisha yawe mepesi kwetu yani anatabia ya kuficha ficha vitu km blender,majiko,electric jug,funguo za friji chumbani ili tusipike wakati yeye hayupo yani haya ni machache tu on top of all she is very ugly hajipendi ananyoa para kama sempai wa kichina.

Hajawahi kufanya lolote la maendeleo kama wanawake wengine ndani ya nyumba hata kubadili mapazia tu,hata kupanda bustani nje hana muamko ukipanda anazifyeka kama magugu shambani,Kiukweli nashindwa kuelewa huyu mtu ametufikaje maishani ni aibu tupu kwetu tokea mama afariki hakujawahi kuja wageni kwa mtindo ule uliokuwepo zamani,kuna ndugu hawaji kabisa kwetu.Nyumba ipo kama haina mwanamke.

Binafsi mwanamke wa namna hii hatokuwa na nafasi katika maisha yangu namtanguliza mungu anisimamie katika kufanya chaguo sahihi,nawasihi na wanaume wenzangu muwe makini sana katika kuchagua wenza.

Cheat rahisi ya kumjua mwanamke wa hovyo ni kumpima imani yake kwenye vyakula tu.Ukiona ana choyo ya chakula hilo ni bomu na wanawake wote wenye tabia hii jitahidini mjirekebishe jamani haipendezi,laiti mngelijua sehemu ya kwanza mwanadamu kuoza utapofariki ni tumbo msingelifikiri kufanya choyo hata mara moja.
 
Issue rahisi sana mbona, tafuta kwako na uoe wako. Baba yako yuko kwake na karidhika na huyo jinsi alivyo. Haya machungu hayana msingi zaidi ya kukuumiza tu.
 
Huyo ni mama yako, baba yako kafika hapo, huwezi kulibadili labda yeye aamue. Tafuta kwako uhamie uondokane na hizo kero.
 
Wewe mwenyewe mleta mada inaonekana ipo shida kwako, moyoni na katika fikra zako. Hapo chapa lapa kajitafutie chako. Mwaache baba yako na ampendae au mwambie baba yako amfukuze mke wake akuoe wewe. Acha kumvua baba yako suruali
 
Pamoja na hayo, ndo kiburudisho cha mshua hicho
hujafikia umri wa kua kwako na vitu vyako hadi mliane timing na maza kutumia blenda?
 
Yaani mtiririko wa malalamiko toka mwanzo nikafikiria ni KE kumbe ni ME...aagrh!!! mbona unatutia aibu wewe???... yaani para ya mwisho ndiyo nikakutambua....lakini mwandiko wa kikekike kabisa....tafuta kwako!
 
UJUMBE NI HUU
( Cheat rahisi ya kumjua mwanamke wa hovyo
ni kumpima imani yake kwenye vyakula
tu.Ukiona ana choyo ya chakula hilo ni bomu)

Naona ke" wote humu mnamshambulia mleta mada bila shaka Ujumbe hapo juu umewagusa sana hasa Miss chaga na Evelyn Salt chumvichumviii..
 
unatuchanganya 1- anagawa vitu kama mchele,vyombo n.k
2. ni mchoyo sana

hebu weka vizuri hapo kwanza! isijekuwa akigawa vitu roho yakuuma

hajabadilisha chochote vipi umemuuliza mshua kwamba kampa hela ya mapazia na vitu vya ndani?
 
Back
Top Bottom