Ni tabia mbaya na isiyo na maadili kukosoa kila jambo linalofanywa/kuanzishwa na Serikali

Eberhard

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,138
786
Ndugu zangu na watanzania wenzangu tuamke kutoka usingizini. Tuache tabia ya kukosoa kila jambo linalofanywa na serikali. Tuipongeze serikali yetu kwa mazuri inayofanya. Tuwaombee viongozi wetu. Tuwatie moyo na pale panapohitajika kukosoa tukosoe kwa nia kujenga. Tutoe positive alternative siyo kuishambulia na kuikatisha tamaa serikali.

Ebu jiulize ungekuwa wewe ungefanya nini? Je usingefanya makosa?

Tumepata rais anayepinga ufisadi kwa vitendo. Nchi yetu imeanza kupata heshima kimataifa. Watanzania tumeanza kuaminika. Wavivu wameanza kuchapa kazi. Apandacho mtu ndicho anachokivuna. Hapo zamani za kale Kuna watu walikuwa wanavuna bila kupanda. Kuna walioweza kuwapangishia vimada nyumbani yenye gharama hata ya m1 kwa mwezi kwa pesa ya serikali yetu. Rais Huyu siyo mjinga anania njema. Unawauzaje mema Nchi yetu. Anatoe Elimu bure, hospitalini na mahakamani Heshima imeongezeka na rusha imepungua, anajenga barabada, analeta treni ya umeme, ndege tumeziona, flyover hizo na mambo mengine mengi. Mlitaka rais afanye nini?

Nimepitia facebook page ya rais Museveni nikafurahishwa sana na namna ya wananchi wa Uganda wanavyomuunga mkono rais wao. Why not us?

Imefika wakati inakera sana. Kila kinachofanywa na serikali kibaya tu. Where are we heading? Serikali ifanye nini ili tuwe na shukurani? Ndiyo maana rais amesema yeye ni kama dereva hanaangalia tunafika salama hivyo hatasikiliza kelele za abiria. Go my president If I was me I could do the same. Forward ever backward never.

Binafsi yangu nimebadilika sana. Ninamuunga mkono rais wangu na serikali yetu. Nawe ubadilike.
 
Kama ambavyo tunapenda kusifiwa na kupambwa ndivyo tuwe tayari kukosolewa. Labda nikukumbushe tu kipimo cha juu zaidi cha uzalendo ni kukubali kutofautiana mawazo na misimamo tukienda hivo tutaishi kwa harmony ila kuanza kukimbizana na wanaokukosoa haitoleta tija yoyote kwa taifa zaidi ya kutekana na kuuana!!!
 
serikali iachie madaraka tujiendeshe wenyewe, yaani ww unataka tusifie kila kitu hata upuuzi
 
Wenye tabia hizo wengi wao hawataacha, kwasababu awamu hii ya 5 wanaisoma namba na kusaga meno. Subiri wale 9,000 wakiguswa nao watajiunga kufanya hayo na wengineo wengi tu.
 
Tunatamani iwe hivyo lakini haiwezekani kwa sababu upinzani unataka kuaminiwa na wananchi pia hivyo ukisifu utaenda kuwaeleza nini watanzania hadi wakuchague wewe?
Tegemea kupingwa tu siku zote kwa masilahi ya upinzani.
 
Asili mia kubwa ya watanzania ni WANAFIKI wa hali ya juu na MAGUFULI ameshalijua hilo thats why hasikii la mwazini wala la mnadi swala,na ni bora iwe hivyo ili tunyooke,mazoea hujenga tabia.
 
We unafikiri kuna alternative gani ya kumshauri mtu ambaye hashauriki? Ameshasema kuwa hakuna anayempangia cha kufanya. We acha apingwe tu maana hakuna namna.

Ifike wakati aruhusu vyama vya siasa vimshauri (awaruhusu waongee).

Hakuna kitu kibaya kama kumnyima mtu uhuru wa kuongea maana siku akipata ka upenyo hataongea tu bali atabwatuka. Na ubwatukaji huo unaweza kuzaa outcomes kubwa. Mazuri yake yote (Mkuu wa kaya) yatasahaulika mara moja.
 
Tuwe na shukrani katika lipi? yaani unataka tuseme asante baada ya kukatwa 15%, baada ya kukosa nyongeza ya mshahara, baada ya kutolipwa madai yetu? Kila mtu ana namna ya kufikiri, si lazima tufikiri kama makada wa ccm, kupenda kujipendekeza kwa wenye madaraka
 
Kawaida anaye kosoa inatoa mwanga kwa msikilizaji. Anaye kosolewa. Ila kuna mipaka ya kukosoa.
Ikiwa kukosowa kunaambatanishwa na unazi wa chama hana mpango. Lakini ikiwa ni kosa kweli hapo sawa kabisa
 
Na ni tabia mbaya zaidi kukosoa juhudi zinazofanywa na taasisi binafsi kwa kusema vyuo vikuu vyao ni vya hovyohovyo
 
We unafikiri kuna alternative gani ya kumshauri mtu ambaye hashauriki? Ameshasema kuwa hakuna anayempangia cha kufanya. We acha apingwe tu maana hakuna namna.

Ifike wakati aruhusu vyama vya siasa vimshauri (awaruhusu waongee).

Hakuna kitu kibaya kama kumnyima mtu uhuru wa kuongea maana siku akipata ka upenyo hataongea tu bali atabwatuka. Na ubwatukaji huo unaweza kuzaa outcomes kubwa. Mazuri yake yote (Mkuu wa kaya) yatasahaulika mara moja.

Kweli awaache tu wapinzani wamshauri tu Mfano ni Zitto anayetaka tuluhusu tu mchanga wa madini uende tu.
Huu ndo ushauri wa wapinzani wa Tz
 
serikali iachie madaraka tujiendeshe wenyewe, yaani ww unataka tusifie kila kitu hata upuuzi
Kuna uzi umeanzishwa kuhoji kwamba kweli zile hostel za UDSM rais kazijenga kwa 10billions?

Huu ndio moja ya upuuzi anaomaanisha mleta mada.
Watanzania tumekua watu wa kupinga na kukosoa kila kitu hata kiwe kizuri sisi ni kupinga na kukosoa tu.
 
Kama ambavyo tunapenda kusifiwa na kupambwa ndivyo tuwe tayari kukosolewa. Labda nikukumbushe tu kipimo cha juu zaidi cha uzalendo ni kukubali kutofautiana mawazo na misimamo tukienda hivo tutaishi kwa harmony ila kuanza kukimbizana na wanaokukosoa haitoleta tija yoyote kwa taifa zaidi ya kutekana na kuuana!!!
Tatizo ni kupinga kila kitu kuonyesha hakuna kitu.
 
Ndugu zangu na watanzania wenzangu tuamke kutoka usingizini. Tuache tabia ya kukosoa kila jambo linalofanywa na serikali. Tupongeze serikali yetu kwa mazuri inayofanya. Tuwaombee viongozi wetu. Tuwatie moyo na pale panapohitajika kukosoa tukosoe kwa kujenga. Tutoe alternative siyo kuishambulia na kuikatisha tamaa serikali.

Ebu jiulize umekuwa wewe ungefanya nini? Je usingefanya makosa?

Tumepata rais anayepinga ufisadi kwa vitendo. Nchi yetu imeanza kupata heshima kimataifa. Watanzania tumeanza kuaminika. Wavivu wameanza kuchapa kazi. Mlitaka rais afanye nini?

Nimepitia facebook page ya rais Museveni nikafurahishwa Sana na namna ya wananchi wanavyomuunga mkono. Why not us?

Imefika wakati inakera sana. Kila kinachofanywa na serikali kibaya tu. We are we heading? Serikali ifanye nini ili tuwe na shukurani? Ndiyo maana rais amesema yeye ni kama dereva hivyo anaangalia tunafika salama hivyo hatasikiliza kelele za abiria.

Binafsi yangu nimebadilika sana. Nunamuunga mkono rais wangu na serikali yetu. Nawe ubadilike.

Kama mmepata heshima kimataifa si inatosha huku mkigeuza wa ndani mashetani. Hata mwenzenu dimond anapiga show za nje tu.
 
Back
Top Bottom