Ni tabia gani hii

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
2,314
5,138
Kuna hii tabia ya rafiki au mpenzi,anakuja kukutembelea nyumbani/geto kwako,kisha kuanza kutamani vitu vyako hii imekaaje?

Utasikia mara jiko lako zuri, kampuni gani hili,au mara hii tv nimeipenda naomba,usoni haonekani kutania kadhamiria kweli.

Mwaka fulani Kuna mwanamke alikuja magetoni,akavikuta viatu fulani ambavyo sikuwa navivaa Sana,basi aling'ang'ania nimpe.

Nikawaza mbali Sana maana viatu vya kiume pia si saizi yake ye vya nini.cha ajabu nilimuona navyo mdogo wake wa kiume kapigilia

Pia Kuna manzi yeye aliondoka na redio zile za tape sijui kaseti,eti anaipenda anataka akasikilize RTD kipindi hicho.mbaya zaidi radio haikuwa yangu ilikuwa ya mshua.

Vitu vingi mno,hii imekaaje wanabodi
 
Wabongo tulivyo mkuu
Uwe unakunja sura na kusema hupendi kuombwa
 
Kuuliza na kutaman sio vibaya ila mambo ya kuanza kuombaomba au kukosoa kitu sio vizuri na apo ndo tatizo
 
Back
Top Bottom