Ni swali ninalojiuliza, tusaidiane majibu

Fene

JF-Expert Member
May 4, 2021
2,442
3,403
Inakuwaje wakuu.....

Wakuu ukweli ni kwamba hakuna binaadamu alietaka kuja duniani lakin tunajishtukia tu tumeshakuja duniani

Swali ssa linalonifanya kila siku nitafakari

Kwanini watu tunaogopa sana kifo ukizingatia hatujawahi kukiexperience

Yani hata mtoto wa miaka minne tu akiona hatari tu mbio kujiepusha nayo, yote hiyo kuepuka kifo

Wajuzi watujuze............

Jf kisima cha maarifa
png-transparent-question-mark-question-mark-s-text-question-check-mark.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufa hakuumi ila kinachokupelekea kufa ndio kinaumiza inaweza kuwa maradhi, ajali au kitu chochote bahati mbaya wakati unazaliwa hukufeel hayo maumivu kwa sababu yalibebwa na mama yako. Bahati mbaya kifo kinaogopwa kwa sababu hatujui baada ya kifo tunaenda wapi! Zaidi ya nadharia ambazo tumeaminishwa na dini zetu kwamba kuna pepo na jehanamu hivyo ndio vinavyotuogopesha
 
Wewe kuzaliwa, ni matokeo ya starehe (makatiko ya baba na mama yako). Na hata wao ukiwauliza watakujibu kwamba, hawakuwai kuoanga kukuzaa.
Hofu ya kifo ni matokeo ya kufichwa waoi tutaenda baada ya kufa. Na ubaya zaidi hakuna mtu mwenye alirejea toka kukufa na akatusimulia maisha ya huko kifoni.
Tunahofu na kifo sababu, hatujui tukikufa tunaenda wapi.
 
Binafsi hili jambo linanipa hofu sana ya kuleta mtoto nami huku duniani maana mimi mwenyewe sioni faida ya kuwepo hapa. Kama kweli Mungu anatupatia free will na sio dikteta ingebidi atuulize huko huko kama tutahitaji kuja duniani. Mimi nisingependa kuja huku, kwakua mimi sipendi basi sitaki mtoto aje anilaumu na kujilaumu kwanini alizaliwa.
 
Dah.. imagine maisha haya machungu hivi.. alafu umlete mwanao nae aje ateseke, ahangake shida kibaaaao. Aiseee..
 
Inakuwaje wakuu.....

Wakuu ukweli ni kwamba hakuna binaadamu alietaka kuja duniani lakin tunajishtukia tu tumeshakuja duniani

Swali ssa linalonifanya kila siku nitafakari

Kwanini watu tunaogopa sana kifo ukizingatia hatujawahi kukiexperience

Yani hata mtoto wa miaka minne tu akiona hatari tu mbio kujiepusha nayo, yote hiyo kuepuka kifo

Wajuzi watujuze............

Jf kisima cha maarifaView attachment 1872148

Sent using Jamii Forums mobile app
una hakika hakuna aliyetaka kuja duniani? hii mada unaijadili kiroho ama kisayansi?
 
Wengi wetu kulingana na imani za dini zetu tunaamini kuwa kuna Peponi/ paradiso/ mbinguni na Jehanamu. Na sifa za mtu kwenda mojawapo ya sehemu hizo zinajulikana, kwa kuwa tumekuwa tunafundishwa na viongozi wetu kupitia vitabu vya dini.

Mimi nafikiri hofu ya kifo inasababishwa na mambo yafutayo:-

1. Maisha ya dhambi. Kwa kuwa tunajua kuwa mtu akifa na dhambi anakwenda Jehanamu, kwenye mateso makali ya kuungua na moto. Sidhani kama mtu anayeishi maisha matakatifu atakuwa na hofu ya kufa kwa kuwa anajua kuwa akifa anakwenda Paradiso au peponi, ambako hakuna dhiki wala mateso.

2. Jambo jingine ni kwamba duniani tumepazoea, mazingira yake tumeyazoea. Sasa kuhama mazingira uliyoyazoea na kwenda kuishi sehemu nyingine ambayo hata hujawahi kufika inaleta hofu. Fikiria hata mazingira ya kawaida unapohama au kuhamishwa kwenda mahali ambapo hujapazoea huwa kuna hofu fulani inaingia- kuhusu huko unakohamia. Unakuwa na mawazo mengi jinsi utakavyoanza maisha mapya ugenini.

3. Vilevile hofu ya kifo inaweza kusababisha na mtu kuwa na mipango na ndoto mbalimbali za kukamilisha hapa duniani, ambayo angependa kuikamilisha kabla ya kufa. Hivyo akifikiria kuwa kifo kinaweza kuzima mipango hiyo- hofu inaingia. Kuna majukumu pia ya kifamilia. Mtu ana watoto wanaomtegemea kwa kila kitu. Hivyo kifo kinampa hofu ya kuwaacha watoto wakiteseka.

Ngoja niishie hapa kwa leo.
 
Acheni hizo wakuu mbona life good tu..Cha msingi tubuni na ombeni mjazwe Imani hofu iondoke
 
Kufa hakuumi ila kinachokupelekea kufa ndio kinaumiza inaweza kuwa maradhi, ajali au kitu chochote bahati mbaya wakati unazaliwa hukufeel hayo maumivu kwa sababu yalibebwa na mama yako. Bahati mbaya kifo kinaogopwa kwa sababu hatujui baada ya kifo tunaenda wapi! Zaidi ya nadharia ambazo tumeaminishwa na dini zetu kwamba kuna pepo na jehanamu hivyo ndio vinavyotuogopesha
Ahsante mkuu, I think it reflect reality

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kuzaliwa, ni matokeo ya starehe (makatiko ya baba na mama yako). Na hata wao ukiwauliza watakujibu kwamba, hawakuwai kuoanga kukuzaa.
Hofu ya kifo ni matokeo ya kufichwa waoi tutaenda baada ya kufa. Na ubaya zaidi hakuna mtu mwenye alirejea toka kukufa na akatusimulia maisha ya huko kifoni.
Tunahofu na kifo sababu, hatujui tukikufa tunaenda wapi.
Ahsante mkuu kwa mawazo yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi hili jambo linanipa hofu sana ya kuleta mtoto nami huku duniani maana mimi mwenyewe sioni faida ya kuwepo hapa. Kama kweli Mungu anatupatia free will na sio dikteta ingebidi atuulize huko huko kama tutahitaji kuja duniani. Mimi nisingependa kuja huku, kwakua mimi sipendi basi sitaki mtoto aje anilaumu na kujilaumu kwanini alizaliwa.

Sasa huwa hugongi ngozi??
 
Wewe kuzaliwa, ni matokeo ya starehe (makatiko ya baba na mama yako). Na hata wao ukiwauliza watakujibu kwamba, hawakuwai kuoanga kukuzaa.
Hofu ya kifo ni matokeo ya kufichwa waoi tutaenda baada ya kufa. Na ubaya zaidi hakuna mtu mwenye alirejea toka kukufa na akatusimulia maisha ya huko kifoni.
Tunahofu na kifo sababu, hatujui tukikufa tunaenda wapi.
Wazazi wako uliwauliza au una jumlisha wazazi wa wote wamejibu hivi
Ahsante Nuzulati kwa msaada wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi hili jambo linanipa hofu sana ya kuleta mtoto nami huku duniani maana mimi mwenyewe sioni faida ya kuwepo hapa. Kama kweli Mungu anatupatia free will na sio dikteta ingebidi atuulize huko huko kama tutahitaji kuja duniani. Mimi nisingependa kuja huku, kwakua mimi sipendi basi sitaki mtoto aje anilaumu na kujilaumu kwanini alizaliwa.
Huwezi jua Da'Vinci wenda mwanao atayafurahia maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante mkuu kwa mawazo yako, vp kwa watoto wadog? dhambi bado hawana, dunia sidhani kama wameshaizoea, mipango ya maisha bado hawana, inakuwaje hapo sasa?
 
Ahsante mkuu kwa mawazo yako, vp kwa watoto wadog? dhambi bado hawana, dunia sidhani kama wameshaizoea, mipango ya maisha bado hawana, inakuwaje hapo sasa.............?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa kwa watoto nafikiri wataalamu wa saikolojia ya binadamu na tabia za binadamu wanaweza kutusaidia. Mimi si mbobezi katika eneo hilo.
 
Binafsi hili jambo linanipa hofu sana ya kuleta mtoto nami huku duniani maana mimi mwenyewe sioni faida ya kuwepo hapa. Kama kweli Mungu anatupatia free will na sio dikteta ingebidi atuulize huko huko kama tutahitaji kuja duniani. Mimi nisingependa kuja huku, kwakua mimi sipendi basi sitaki mtoto aje anilaumu na kujilaumu kwanini alizaliwa.
Nilijua niko mwenyewe ninayewaza hivi aisee ...bora nisingezaliwa tu
 
Back
Top Bottom