Ni siri kubwa....

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
925
NDOA INA SIRI KUBWA

KWA WALE WALIO KATIKA NDOA WANAWEZA KUSHUHUDIA HAYA:

Kama umegombana na una hasira kali dhidi ya mwenzio, mara zote inapofikia kwenye hitaji la "ndoa", hasira huwa zinachukua likizo ya muda na pengine kupelekea hitima ya ugomvi....mpaka leo bado sifahamu siri iliyomo kwenye maisha ya ndoa.

Na pengine hata mkigombana ugimvi mkubwa, mkapishana , wewe sebuleni yeye chumbani, au yeye kwenye meza ya kujipodolea (dressing table) na wewe bafuni, lakini inapofikia kwenye suala la mwenzio anahitaji msaada wako, roho yako inaweza kukuuma sana na kujisikia kumsaidia japo pengine hata ukiwa hujisikii hata kumsemesha.. utafanya tu na kuona kabisa mwenzio hapaswi kuumiza,

.....Unawaza mwenzio anapokuwa mbali nawe, labda atakuwa ana fanya jambo fulani ambalo wewe hungependa afanye, lakini hata kama hakufanya jambo hilo, akiwa karibu nawe unajaribu kudadisi, na pengine kwa hisia unaweza kujaribu upate nafasi hata ujue kwenye simu yake ya kijanjani nani aliyempigia au kumtumia ujumbe wa maandishi (SMS)...

'....Hata kama mlikuwa katika makubalinao ya kutogusa simu ya mwenzio, ghafla unapoisikia ikitoa mlio wa kuita au ikiwa pahala, moyo unakusukuma kujua ni nani anamtafuta, na unaweza kuichukua tu kwa kificho ili ujue mawasiliano yake na mtu ambae unahisi anaweza kuwa ana husina nae kama wewe (..) na ukiona ujumbe usiouelewa, utauliza kwa kalui ya kuonyesha makubalinao ya kutogusa simu ya mwenzio hayana maana..ukidai unamlinda ..pengine chokochoko na hisia zinaweza kupelekea ugomvi (ukiwa na maana ya wivu juu ya mwenzio) hili linaweza kusababisha mpaka mahusiano kuvunjika. Lakini ukichiunguza kisa, unabaini kuwa ilikuwa ni kujaribu kuhakikisha mnadumisha mahusiano ila athari ya staili iliyotumika ikapelekea mahusiano hayo kuvunjika bila wenyewe kufahamu.
 
Sasa ule usemi wa ........Settle your differences before going to bed...unaapply wapi hapa? Maana ninavyosoma (sijui ni huu ukilaza) ninaona kama vile unasema tendo lifanyike no matter what!? Nyway kila la kheri wenye changamoto
 
Ni kweli kwamba lau tendo au ngono itahitajika au kutokea ktk kipindi cha ugomvi, nyoyo hulegea na iwavyo vyovyote sharti shahwa zitulizwe. Utafiti wangu binafsi sijui wengine, lau mutamaliza tendo kwa kufika kilele basi munaposhuka nazo hasira hutoweka mkajipata mwachezacheza kitandani.
 
Ni bahati sana kuna hiyo kitu hapo for instant reconciliations. hata kama ugomvi utaendelea baadae, at least najua bado ananipenda, ni hasira tu ya muda. kwanza baada ya mambo ndio mnaanza kuongea sasa na kutatua matatizo... lol
 
Siri gani?

Ni siri kubwa:

Upo wakati unaweza kukimbiwa na wote ambao waliwahi kudhani na kujigamba wanakupenda sana kwa damu (nduguzo, mama, dada, kaka, baba, nk) lakini ijapo siku au saa unapofikwa na shida nzito ya kukufanya ushindwe kujimudu ikiwemo maradhi ya kufisha, mwenzio katika ndoa yenye uaminifu, kamwe hataweza kukuacha...haya huwezi kuyategemea uwapo na kimada au hawara. Ni siri kubwa, hata kama unamatatizo ya kimaumbile, una sumbuliwa na jambo la aibu kuliweka wazi katika jamii, na hata kama mwenzio huwa wanaonekana ni mtu asiejua kutunza siri katika mambo mengi kwenye jamii, lakini katika ndoa timilifu, ni nadra sanaaa kusikia mume au mke akimuumbua mwenzio kwa kumwaga taarifa za siri ya mwenzie...

.....Hujarejea nyumbani, hata kama mwenzio mtakuwa hamzungumzi, lakini moyoni ataumia na kutaka kujua ulipo, pengine anaweza kukutafuta hata kwa kumtumia mtu mwingine akuulizie ulipo...atafurahi moyoni akikuona japo machoni atakuwa akuonyeshi furaha hiyo.

ataumia wakati wakisikia unatetwa au umefanyiwa jambo baya, anaweza kutafuta hata mbinu ya kulipisa kisasi ..hii hata kwa kujitoa maisha yake kwa ajili yako. (hili ni nadra sana hata kwa mzazi kumfanyia mwanae).
 
Matatizo ya kamba za usiku ndio haya. Yaani mtu anaapply live yale yalomsibu mchana kutwa na kuyatupilia humu!
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom