Ni Sheria ipi inamlinda mtumishi aliyehamishwa kutokwenda kituoni kwake hadi alipwe?

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,096
9,216
Kumekuwa na Utaratibu wa watumishi wa Umma kuhamishwa bila kulipwa stahili zao. Hivi hakuna Sheria inayomlinda Mtumishi kama huyu? Nakumbuka Rais aliwahi kutamka jukwaani kuwa Mtumishi asihame hadi alipwe.

Je, hii ipo kisheria?
 
Tafuta definition ya neno: Mtumishi. It simply means going extra mile, uvumilivu etc! It may take 1 year hujapewa na usipo report kazini ni issue! CCM Oye!
 
Mtumishi=Mwana Kondoo

Inabidi awe mpole tu mpk pale Mchungaji wa kondoo hao atakapoamua hatma ya kondoo wake.
 
Nenda idara ya utawala alaf waambie wakupe haki za mtumishi usihame mpaka wakupe hela ikishindikana nenda Tamisemi dodoma usikubali kunyanyasika.
 
Kumekuwa na Utaratibu wa watumishi wa Umma kuhamishwa bila kulipwa stahili zao. Hivi hakuna Sheria inayomlinda Mtumishi kama huyu? Nakumbuka Rais aliwahi kutamka jukwaani kuwa Mtumishi asihame hadi alipwe.

Je, hii ipo kisheria?
Hebu fafanua mkuu.
sasa Huko kituo kipya unatumia hela ipi kwenda kama hujalipwa. mbona maajabu.
unatakiwa uwezeshwe ndo uende
 
Kuna Mwalimu mdogo wangu kahamishwa Sasa alimiuliza hivo...Ila jibu lako Ni jibu tosha
Haya Mambo ya kienyeji yapo mengi Sana LGA Wizarani na Taasisi zingine hakuna vurugu hizi!
 
Endelea kuripoti na kufanya kazi hapohapo ulipo,ukishalipwa ndio uondoke.
 
Hebu fafanua mkuu.
sasa Huko kituo kipya unatumia hela ipi kwenda kama hujalipwa. mbona maajabu.
unatakiwa uwezeshwe ndo uende
Yaani huu ujinga unafanyika sana kwenye LGA na mbaya zaidi watumishi wenyewe wanauendekeza na kuubariki ionekane ndio mazoea (good practice), unahamishwa halafu unatumia fedha yako kwenda kuripoti na kusafirisha mizigo yako..ukihoji unaambiwa si unalipwa mshahara, tumia huo halafu utalipwa baadae.
 
Kumekuwa na Utaratibu wa watumishi wa Umma kuhamishwa bila kulipwa stahili zao. Hivi hakuna Sheria inayomlinda Mtumishi kama huyu? Nakumbuka Rais aliwahi kutamka jukwaani kuwa Mtumishi asihame hadi alipwe.

Je, hii ipo kisheria?
Ni waraka wa namba 2 wa 2018 wa Katibu Mkuu (Utumishi), unakataza mtumishi wa umma kuhamishwa (kulazimishwa kuripoti kituo kipya) kabla ya kulipwa stahiki zake.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom