Ni sheria ipi ilifuta fao la kujitoa?

Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
248
Points
225
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
248 225
Wakuu,

Leo kwenye gazeti la Nipashe kulikuwa na habari iliyoripoti yaliyojiri bungeni na kuandika kuwa Naibu Spika amesema "TAYARI NCHI INA SHERIA ILIYOFUTA FAO HILO" (soma habari kamili hapa chini). Sasa swali ni HIYO SHERIA NI IPI? ILIPITISHWA LINI?

Dk. Tulia alitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu mwongozo ulioombwa kwake na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), kuhusu fao hilo baada ya serikali kueleza bungeni jana kuwa bado inalifanyia kazi. Mifuko ya hifadhi ya jamii iliyopo nchini ni pamoja na NSSF, PSPF, GEPF, PPF na LAPF.

Katika kujenga hoja yake, Waitara alisema kuwa wakati Ofisi ya Waziri inajibu swali bungeni kuhusu suala hilo jana asubuhi, ilisema mchakato wa fao la kujitoa unaendelea kufanyika na kwamba, uamuzi wake haujafanyika.

"Jambo hili limekuwa na mkanganyiko mkubwa sana,” alisema Waitara na kuongeza:

“Wapo watu waliostaafu kazi hawajapewa mafao yao, wapo watumishi ambao wanafanya kazi kwa mkataba, mkataba ukiisha anaambiwa mafao yako usubiri mpaka ukifikia umri wa miaka 55.

"Wapo watu wanafanya kazi katika mazingira magumu, wanataka waache kazi wapate mafao yao waanzishe shughuli mbalimbali za maendeleo kulingana na kipato, waweze kujikimu.

"Na wapo watu ambao kimsingi Mheshimiwa Naibu Spika, ni wagonjwa…wanahitaji mafao yao ili wajitibu na wasomeshe watoto wao. Hili zoezi limeshindikana.

"Sasa naomba mwongozo wako kwa sababu kama Naibu Waziri anasema kwamba jambo hilo lipo kwenye mchakato na wabunge wanaulizwa na wananchi wao kwa nini hawapewi fedha zao, wanaambiwa serikali imeelekeza mpaka ufikishe miaka 55."

Waitara alidai sheria hiyo hajawahi kuiona, mjadala haujawahi kufanyika na kwamba, jambo hilo halijawahi kupitishwa na bunge.

Alishauri wafanyakazi waendelee kupata haki zao na kama kuna mchakato, kauli ya serikali itoke ili wapate haki zao mafao yao
yawasaidie kufanya shughuli za kuwaingizia kipato.

"Mchakato utakapokamilika kwa ujumla wake, Watanzania watapata maelezo mengine. Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wako katika jambo hili muhimu sana," alisema.

Akijibu mwongozo huo, Dk. Tulia ambaye jana aliongoza kikao cha Bunge kwa mara ya kwanza tangu mkutano wa tisa wa Bunge la 11 lianze Jumanne ya wiki iliyopita, alisema kuna sheria iliyofuta fao la kujitoa na iliwasilishwa bungeni na kuridhiwa na chombo hicho cha kutunga sheria.

"Waheshimiwa wabunge, huu mchakato ulianza muda mrefu na hata hapa bungeni sheria iliwahi kuletwa… sheria ilishatungwa. Na mpaka sasa tunapozungumza sheria ya mwisho kabisa iliyopitishwa na Bunge hili inakataza fao la kujitoa," Dk. Tulia alisema.

"Kwa hiyo, mchakato maana yake ni mazungumzo sasa ya kuangalia namna ya kubadilisha tulikotoka, lakini sheria iliyopo mpaka ninapozungumza inakataza fao la kujitoa."

Dk. Tulia aliongeza kuwa mifuko ya hifadhi za jamii imeweka utaratibu wa ziada ukiacha yale mafao ambayo yako kisheria.
Alisema utaratibu huo unaipa mifuko huo fursa ya kuamua kujitengenezea utaratibu, lakini sheria iliyopitishwa na bunge inakataza fao la kujitoa.

"Kwa hiyo, mwongozo wangu katika hilo, kwamba mchakato gani unaendelea, ni kwamba sheria tunayo tayari," Naibu Spika huyo alisema, "kama kuna mchakato unaendelea basi pengine ni wa mazungumzo kati ya serikali na wafanyakazi na waajiri kuona namna bora ya kulifanya hilo jambo.

"Na mimi nadhani kwa namna lile swali lilivyokuwa limeulizwa, ni vizuri kujiridhisha na tafiti zilizofanywa kuhusu fao la kujitoa kama ni jambo ambalo kama nchi ambao tumesaini mikataba mbalimbali kuhusu wafanyakazi, kuhusu waajiri na serikali, ni jambo ambalo tunataka kuliendea?

"Kwa hiyo, kama kuna mchakato wowote ambao unaendelea serikalini, basi mfanye haraka ili tuseme tunasimama wapi."

Awali, hoja ya fao la kujitoa iliibuka asubuhi wakati wa kipindi cha maswali baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Sonia Jumaa Magogo, kutaka kauli ya serikali kuhusiana na fao hilo.

Akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia vijana na ajira, Antony Mavunde, alisema serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hilo ikishirikiana na wadau kuona njia bora ya kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wadau wote.

Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mkakati gani dhidi ya waajiri ambao hawaandikishi watumishi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwasababishia kukosa stahiki zao.

Katika majibu yak kuhusu swali hilo, Mavunde alisema mkakati wa serikali katika kuhakikisha waajiri wote wanaandikisha wafanyakazi wao ni kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii Na. 8 ya mwaka 2008 kifungu cha 30.

Alisema kifungu hicho kimeweka utaratibu unaomtaka mwajiri kuwaandikisha watumishi wake katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
"Mwajiri anayekiuka matakwa ya kifungu hicho anastahili adhabu ya kulipa faini ya kiasi kisichozidi Sh. milioni 20 kwa mujibu wa kifungu cha 55 cha Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii," alisema Mavunde.

Aliongeza kuwa katika kuimarisha usimamizi wa sheria za kazi, serikali kupitia bunge ilifanya marekebisho ya Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya mwaka 2004 ili adhabu ya papo kwa papo itolewe kwa waajiri wanaokiuka matakwa ya sheria ikiwa ni pamoja na kutosajili wafanyakazi katika mifuko ya jamii.

Source: Nipashe (15/11/2017)
 
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
248
Points
225
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
248 225
Maana hili suala la fao la kujitoa limekuwa kama kaa la moto kwa wafanyakazi waliofukuzwa kazi.
 
msomi kutoka znz

msomi kutoka znz

Senior Member
Joined
Sep 18, 2017
Messages
157
Points
500
msomi kutoka znz

msomi kutoka znz

Senior Member
Joined Sep 18, 2017
157 500
Taifa linapata dhambi kubwa kukataa kulipa stahiki za watu

Shida sio kufuta fao la kujitoa, unaleta mbadala gani?! At least sheria ingepitishwa mtu badala ya kupewa fao la kujitoa apewe bima,apewe free transport katika kutafuta ajira mpya,etc etc

Kodi mnakusanya.tumieni Kodi kufanya maendeleo,tengenezeni na njia nyingne za mapato.
 
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
248
Points
225
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
248 225
Taifa linapata dhambi kubwa kukataa kulipa stahiki za watu

Shida sio kufuta fao la kujitoa, unaleta mbadala gani?! At least sheria ingepitishwa mtu badala ya kupewa fao la kujitoa apewe bima,apewe free transport katika kutafuta ajira mpya,etc etc

Kodi mnakusanya.tumieni Kodi kufanya maendeleo,tengenezeni na njia nyingne za mapato.
Mkuu kufuta hili fao nako kuna ukakasi, mimi sikumbuki kabisa kama kuna sheria ilifuta hili fao! kwa wanaojua tafadhali ebu tupeni vifungu.

Mbadala watakaouleta utakuwa wa ajabu lazima. Yale mambo ya kuambiwa ukachukue elfu ishirini kila mwisho wa mwezi kama fao la kukosa ajira baada ya kuachishwa kazi hayana maaana kabisa.
 
kilambimkwidu

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Messages
5,045
Points
2,000
kilambimkwidu

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2017
5,045 2,000
Mabadiliko ya sheria za Hifadhi ya Jamii (Social Security Laws Amendment), 2012 yaliondoa kipengele cha uwepo wa fao la kujitoa kwenye sheria ya kila mfuko (maana kila mfuko wa pensheni unayo sheria yake inayotaja mafao yanayotolewa na mfuko husika).

Hivo bas, wabunge walipitisha mabadiliko yale na hivyo automatically vipengele vilivyokua vinataja FAO LA KUJITOA (withdraw) viliondolewa.

Nasikitika kusema kwamba inawezekana kabisa kwamba mabadiliko yalipitishwa bila kujua haswa ni KITU KIPI HASA KINABADILISHWA na matokeo yake wakajikuta wame -repeal vifungu vilivyokua vinasema " mafao yanayotolewa na mfuko chini ya sheria hii ni......(FUTA -Withdraw)

Haikutungwa sheria kama sheria ya kusema FAO LA KUJITOA LISITOLEWE...bali kwa mabadiliko yale kurekebisha vipengele vya mafao na kutokutaja fao la kujitoa (withdraw) automatically mfuko hauwezi kulipa kwakua mfuko unalipa mafao YALIYOTAJWA TU na kila fao limewekewa utaratibu namna linavotolewa.

Sheria za mifuko yote pamoja na hao wasimamizi wa SSRA zilirekebishwa mwaka 2012 na copy ya sheria ambazo ziko embeded zinataja sheria kua ni [R.E 2015] ~maana yake ni kwamba shwria husika ni TOLEO LA 2015 (ambalo ndilo linayo hayo marekebisho ya 2012.

ONA VIELELEZO
1. Kitabu cha sheria za Hifadhi ya Jamii Toleo 2015.

2. Sheria za mifuko mmojammoja zinajieleza (hii ni NSSF)

3. Mafao ya NSSF (angalia kwa hautaona WITHDRAWAL ikitajwa, iliondolewa)

Naenda Zim.
 
Haikutungwa sheria kama sheria ya kusema FAO LA KUJITOA LISITOLEWE...bali kwa mabadiliko yale kurekebisha vipengele vya mafao na kutokutaja fao la kujitoa (withdraw) automatically mfuko hauwezi kulipa kwakua mfuko unalipa mafao YALIYOTAJWA TU na kila fao limewekewa utaratibu namna linavotokewa.

Naenda Zim.
Asante mkuu kwa darasa! Daah! Kumbe mambo yalianzia enzi za JK!
 
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
248
Points
225
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
248 225
Mabadiliko ya sheria za Hifadhi ya Jamii (Social Security Laws Amendment), 2012 yaliondoa kipengele cha uwepo wa fao la kujitoa kwenye sheria ya kila mfuko (maana kila mfuko wa pensheni unayo sheria yake inayotaja mafao yanayotolewa na mfuko husika).

Hivo bas, wabunge walipitisha mabadiliko yale na hivyo automatically vipengele vilivyokua vinataja FAO LA KUJITOA (withdraw) viliondolewa.

Nasikitika kusema kwamba inawezekana kabisa kwamba mabadiliko yalipitishwa bila kujua haswa ni KITU KIPI HASA KINABADILISHWA na matokeo yake wakajikuta wame -repeal vifungu vilivyokua vinasema " mafao yanayotolewa na mfuko chini ya sheria hii ni......(FUTA -Withdraw)

Haikutungwa sheria kama sheria ya kusema FAO LA KUJITOA LISITOLEWE...bali kwa mabadiliko yale kurekebisha vipengele vya mafao na kutokutaja fao la kujitoa (withdraw) automatically mfuko hauwezi kulipa kwakua mfuko unalipa mafao YALIYOTAJWA TU na kila fao limewekewa utaratibu namna linavotolewa.

Sheria za mifuko yote pamoja na hao wasimamizi wa SSRA zilirekebishwa mwaka 2012 na copy ya sheria ambazo ziko embeded zinataja sheria kua ni [R.E 2015] ~maana yake ni kwamba shwria husika ni TOLEO LA 2015 (ambalo ndilo linayo hayo marekebisho ya 2012.

ONA VIELELEZO
1. Kitabu cha sheria za Hifadhi ya Jamii Toleo 2015.

2. Sheria za mifuko mmojammoja zinajieleza (hii ni NSSF)

3. Mafao ya NSSF (angalia kwa hautaona WITHDRAWAL ikitajwa, iliondolewa)

Naenda Zim.
Upo fresh mkuu! Naona Darasa la NSSF limeeleweka. HIVI hakuna ambao walisahau kulitoa fao la kujitoa kweli? PPF vipi?
 
Amalinze

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Messages
6,715
Points
2,000
Amalinze

Amalinze

JF-Expert Member
Joined May 6, 2012
6,715 2,000
Fao la kutokuwa na ajira Lipo wapi?
 
Allency

Allency

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
2,996
Points
2,000
Allency

Allency

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
2,996 2,000
Hivi wale wa buki 7 nao huwa wanawekewa fao huko?
 
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
248
Points
225
Natania

Natania

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
248 225
Upo fresh mkuu! Naona Darasa la NSSF limeeleweka. HIVI hakuna ambao walisahau kulitoa fao la kujitoa kweli? PPF vipi?
Nimeipata hii act ya PPF toka kwenye website yao. Naona imeandikwa kiaina ila nimeona withdrawal benefit kwenye section 22 (d) page 16. Ebu ngoja nitulie niisome vema.
 
Attachments:

mbarouk mkali

mbarouk mkali

Member
Joined
Jun 28, 2017
Messages
50
Points
125
mbarouk mkali

mbarouk mkali

Member
Joined Jun 28, 2017
50 125
Sheria hii ya kuzuia fao la kujitoa ingekua nzuri sana kama serikali ingekua na uwezo wa kutoa ajira kwa raia wake lakini kutokana na serikali kushindwa kutoa ajira kwa wananchi wake na kutegemea zaidi sekta binafsi ni tatizo kwa ujuli
Pili swala hili lina faida kwa serikali kwasababu wakati mwengine serikali kwa kushindwa kutekeleza shughuli za kimaendeleao kutokana na kutokua na vyanzo vya mapato na wakati mwengine huwa wanategemea kukopa kwenye hii mifuko ya hifsdhi ya jamii hii hutokana na kuwa na serikali isiyojali raia wake ni tatizo kwa ujumla sisi wenyewe tuna miezi saba sasa tunafuatilia pesa zetu ppf tunasimbuliwa tu bila sababu za msingi
 
Pole mkuu, sasa PPF wanatoa sababu gani ya msingi?
 
mbarouk mkali

mbarouk mkali

Member
Joined
Jun 28, 2017
Messages
50
Points
125
mbarouk mkali

mbarouk mkali

Member
Joined Jun 28, 2017
50 125
Hawana sababu ya msingi wanatusumbua tu mara njoeni kesho mara wiki ijayo huku siku zinakwenda
 
mbarouk mkali

mbarouk mkali

Member
Joined
Jun 28, 2017
Messages
50
Points
125
mbarouk mkali

mbarouk mkali

Member
Joined Jun 28, 2017
50 125
Nssf wanatoa nina rafiki yangu amechukua mwezi mmoja uliopita
 
Forum statistics

Threads 1,285,875
Members 494,778
Posts 30,877,121
Top