Vinci Dayot Upamecano
JF-Expert Member
- Nov 11, 2020
- 522
- 1,272
Shikamoni Shimba ya Buyenze , Mshana Jr na Bujibuji Simba Nyamaume wengine wote hamjamboni?
Tofauti kidogo na Uzi wa mtaalam Kyambamasimbi hapa tutaangalia vijiji vizuri vyenye Amani, maziwa na asali.
Katika harakati za Maisha, suala la kutembea na kubadilisha makazi iwe ni kwa muda mfupi au kwa muda mrefu ni jambo lisiloepukika. Ndomaana hata mtu mzima mpwayungu village Juzi alikuwa Rwanda keshokutwa tutamkuta USA kisha atarudi tena kijijini kwao Mpwayungu.
Binafsi kwa sehemu yoyote ntakayoazimia kwenda iwe kikazi/kibiashara, kusalimia, mapumzikoni n.k Kipaumbele changu Cha kwanza kukiangalia ni Chakula na Maji mengine naweza kuvumilia hapa watoto wa kishua kina Bill Lugano wakae kwa kutulia kwanza.
Binafsi nimeshawahi kufika vijiji mbalimbali ndani na nje ya Tanzania na kwakweli zipo baadhi ya sehemu zimebarikiwa inshallah ukifika hutamani kutoka haraka na miongoni mwa vijiji ambavyo nilishawahi kukaa na angalau nikalamba asali ni pamoja na;
Malela - Karatu - Arusha. Mnamo mwaka wa 2019 nilikwenda huko kulangua Mbaazi na Ngano, aisee kule kumebarikiwa bwana maana Kuna Chakula Cha kutosha achilia mbali watoto weupe wa kimbulu. Maziwa fresh au mtindi 1ltr nilikuwa nanunua kwa Tshs 800 wakati mayai ya kienyeji naletewa kwa 200Tshs, hali ya hewa nzuri sanaa nilirudi nyumbani nmetakata, wanawake wa kule sio wachoyo, sijui kwa wanaume lkn pia ardhi yao ina rutuba sana.
Kyomu - Moshi (v) Kilimanjaro. Kama ilivyoada nilimsindikiza rafiki yangu Ukweni, bwana wee! Jua sio kali sana, msosi sio suala maana wanafanya kilimo cha umwagiliaji hususani mbogamboga na matunda. Mayai kienyeji 200, nyanya za 500 unapikia siku tatu Maziwa unaamua unywe ndo ukamue au ukamue ndo unywe. Msosi sio shida mabinti wa kushika mkono tu tena kama ndo mgeni hupati tabu ardhi imebarikiwa Ila tu Kuna vumbi kimtindo Na watu wake ni wakarimu sana.
Mto wa Mbu (kijiji nimekisahau jina) - Monduli - Arusha. Pazuri kuanzia ardhi, Hali ya hewa, huduma za kijamii, mzunguko wa hela upo Chakula sio tabu, Watu wake wakarimu na Mabinti pia wamo si mchanganyiko wa Wairaq na masai.
Bukuru - Kondoa - Dodoma. Huku bwana nilifanya kama kupita tu lkn baadae niliamua kurudi nipaone vizuri. Kuna amani ya Hali ya juu unaweza kulala hata nje maana warangi sio watu wa hila. Chakula, Hali ya hewa, ardhi na watoto wa kirangi ndiyo haswa walinishawishi nirudi kupaona vizuri nikanunua na eneo kabisa
Vipo vijiji vitatu ambavyo sitaviorodhesha lakini vilinikosha sana pia ila tu hivyo hapo juu vilinikosha zaidi.
Je na wewe ni Kijiji gani ulichowahi kufika na kukaa kwa muda wowote ule pakakukosha kwa namna moja ama nyingine? karibuni wapenzi.