Ni sehemu gani Dar affordable kuanzisha maisha ukiwa na familia yako?

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Wanandugu ninataka wa kuanzisha maisha nikiwa na familia yangu nikiwa na mke wangu na pamoja na mtoto wangu

Hivyo ningependa kufahamu ni sehemu gani hapa Dar kuanzisha maisha ambapo ninaweza kupanga vyumba viwili at affordable price na eneo nitakaloishi lisiwe la gharama hivyo naomba kufahamu ni wapi nitaanzia maana mwanamke wangu saivi ana ujauzito hivyo nataka kumtoa kwao nianze kuishi nae
 
wana ndugu ninataka wa kuanzisha maisha nikiwa na familia yangu nikiwa na mke wangu na pamoja na mtoto wangu

hivyo ningependa kufahamu ni sehemu gani hapa dar kuanzisha maisha ambapo ninaweza kupanga vyumba viwili at affordable price na eneo nitakaloishi lisiwe la gharama hivyo naomba kufahamu ni wapi nitaanzia maana mwanamke wangu saivi ana ujauzito hivyo nataka kumtoa kwao nianze kuishi nae
Una kipato gani kwa mwezi?
 
Kama huna shughuli maalumu kama ajira ya kukufanya lazima uishi sehemu fulani karibu na kazi yako.. nakushauri nenda yombo buza na maeneo jirani na huko sababu vyumba bei rahis na nyumba bado hazijachoka zina upya upya na usafiri kwenda sehemu nyingi za muhimu Dar ni bus moja tu. Ama nenda Kitunda pia napo ni hivyo hivyo.. pia Manzese na Tandale maisha ni nafuu ila changamoto yake nyumba zake ni za zamani bati full kuvujaaa na mitaa hailali usiku
 
Wanandugu ninataka wa kuanzisha maisha nikiwa na familia yangu nikiwa na mke wangu na pamoja na mtoto wangu

Hivyo ningependa kufahamu ni sehemu gani hapa Dar kuanzisha maisha ambapo ninaweza kupanga vyumba viwili at affordable price na eneo nitakaloishi lisiwe la gharama hivyo naomba kufahamu ni wapi nitaanzia maana mwanamke wangu saivi ana ujauzito hivyo nataka kumtoa kwao nianze kuishi nae
Kwa kipato chako njoo Kimara
 
Inategemea na mishe zako unafanyia wapi.

Angalia sana eneo ambalo kwenda kazini haikulazimu upande gari. Kama unataka bei rahisi ya kumudu panga nyumba isiyo na umeme, zipo nyingi sana katikati maeneo ya Magomeni, Ilala Bomba, Mchikichini, ila tu hakikisha kuwa maeneo hayajai maji kipindi cha mvua, ni rahisi kujua maeneo yanayojaa maji na kufurika.

Vyumba ni kuanzia 25000 kama hakina umeme, mimi ninasubiri kumalizia nyumba yangu nimepanga sehemu haina umeme hapa Magomeni Mapipa kwa 35000 na ninafurahia maisha ninayoishi na familia ya mtoto mmoja.

Kama unahitaji nitafute nikuoneshe vyumba vizuri vya bei hiyo niliyotaja na mahali ambapo hamna usumbufu.

Utafunga sola ya mkopo wa ZOLA kila mwezi unalipa 10,000 kwa miezi 14. Sola yao inachaji simu mbili kwa siku pamoja na kuwasha taa tano, ila ukitumia taa mbili zinatosha sana.
 
Back
Top Bottom