Ni sawa wanafunzi kusimamishwa masomo kwa kutolipa ada?

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Ni haki kwa wamiliki wa shule kuwasimamisha masomo wanafunzi ambao hawajalipa ada kulingana na ratiba ya muhula (kabla mwaka haujaisha)?

Mfano:
Mtoto alitakiwa alipiwe 3,000,000 Tshs jumla kwa utaratibu huu: Muhula wa kwanza: 1,200,000, Muhula wa pili: 1,000,000 na Muhula wa tatu: 800,000. Akajikuta muhula wa pili unakaribia kuisha hajalipiwa hiyo 1,000,000 na kusimamishwa masomo. Mzazi anakaa mwezi mzima bila mtoto kwenda shule kwa sababu anatafuta ada, anakuja kulipa ada, na mpaka mwaka unaisha anakuwa amelipa yote 3,000,000.

Maswali:
1. Huo mwezi mmoja mtoto anafidiwa vipi na shule katika masomo aliyoyakosa na ada imelipwa yote?

2. Kwanini, kama wamiliki wanaruhusiwa na Mamlaka za Serikali (mfano Wizara ya Elimu) kumsimamisha masomo mwanafunzi kwa sababu ya deni ambalo anadaiwa lakini mwaka wa masomo haujaisha, wazazi wasikate pesa ya siku ambazo mtoto hakwenda shule, badala yake analipia hata siku ambazo mwanaye alisimamishwa (hakupata haki yake ya kufundishwa)?

3. Kama wamiliki hawaruhusiwi kumsimamisha mwanafunzi kabla mwaka wa masomo haujaisha, kwa nini wamiliki wasingekuwa wanaacha kuwakosesha watoto haki ya kufundishwa kwa lengo la kuwafanya wazazi wafanye haraka kulipa ada, na badala yake wawazuie kuendelea na madarasa ya juu hadi hapo watakapolipa ada (deni la mwaka wa masomo uliopita) ili watoto wapate haki yao?

Maoni:
Ili kuwalinda wamiliki, Wizara izuie kupokea mwanafunzi mgeni bila barua ya uhamisho toka shule anayotoka ili kuhakikisha mwanafunzi haachi deni.

Au Wizara iweke utaratibu mwingine ili mwanafunzi asisumbuliwe na mmiliki wa shule apate haki yake.

Mtu mwingine anaweza kusema kuwa, Kama mzazi hana uwezo, kwa nini alimpeleka au kwa nini aendelee kumpeleka mwanaye shule za gharama? Ieleweke kwamba, kuna wakati kipato cha mzazi huyumba lakini mzazi hufanya kila awezalo atimize mahitaji ya familia.
Kuwe na kuvumiliana, kujali haki za wazazi, wanafunzi na wamiliki wa shule.

Kusimamishwa kwa wanafunzi kuna madhara yafuatayo:
1. Mwanafunzi kuumia kisaikolojia.

2. Kushuka kwa uelewa wa mwanafunzi na kukosa kufundishwa baadhi ya vitu.

3. Shule kuwa na ufaulu wa jumla usioridhisha kutokana na kuwa na wanafunzi walioshuka kwa uelewa

4. Wazazi kutapeliwa fedha kwa malipo mengine ambayo watoto wao walisimamishwa masomo shule.

5. Taifa kuhujumiwa kwa kuwa na wanafunzi/ wananchi ambao kuna vitu walivikosa (hawakufundishwa)

Nashauri Wizara husika iliangalie hili.
 
Sisi Wakristo kuna neno alitwambia BWANA wetu na Mwokozi wetu, alisema hivi:

"maana ni nani katika ninyi kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema; mtu huyu alianza kujenga akawa hana nguvu za kumaliza". Luka 14:28-30

Nini maana yake? Ninachotaka kukwambia ni kwamba usikurupuke kupeleka watoto shule za gharama bila ya kwanza kujiandaa kiuchumi na kujipima uwezo wako kama utaweza au la.

Usisingizie sijui leo mambo mabaya, sijui uchumi umeyumba, hapana, maisha siyo bahati nasibu, maisha ni mipango endelevu. Jipime uwezo wako, peleka watoto shule pale unapoweza kupalipia bila kikwazo chochote hata kama uchumi utayumba au dharura itatokea.

Hizo shule za gharama ziko kibiashara zaidi, haziwezi kuwa na huruma kwa mtoto asiyelipa ada kwa wakati husika.
 
Kimsingi siyo haki. Asingelipa ndani ya mwaka, hapo sawa. Ila kama mwaka haujaisha, huo ni uonevu na pia ni ukosefu wa busara na uungwana kwa wamiliki wa hiyo shule.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom