Ni sawa mbunge wa Tanzania kuishi nje ya nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sawa mbunge wa Tanzania kuishi nje ya nchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, May 17, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Posted by EMT | May 14, 2012 (Baadae comments zikapotea wakati wa marekebisho ya server)

  Kulikuwa na thread hapa leo kuhusu kukamatwa kwa mbunge wa Chadema huko Marekani lakini imeondolewa baada ya Chadema kutoa tamko rasmi la kukanusha kuwa huyo mbunge hajakamatwa. Hata hivyo, kulikuwa na suala la msingi la kujadiliwa kwenye ile thread. Suala hili linahusu tuhuma za mbunge wa Tanzania kuishi nje ya nchi. Kwenye tamko la Chadema hawakugusia kabisa hili suala. Tuhuma za mbunge wa Chadema kuishi nje ya nchi zimekuwepo kwa muda sasa lakini Chadema hawajawahi kutolea tamko.

  Nimecheki Facebook profile ya huyo mbunge inasema anafanya kazi katika Bunge la Tanzania. Pia profile inasema anaishi Dar Es Salaam. Philosophy yake: she believes in God. Views zake za kisiasa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Favourate quotes yake: I'm not the victim of my mistakes, I take them and grow from them.

  Kama kweli anaishi Marekeni halafu anadanganya anaishi Dar Es Salaam huu si utakuwa ni uongo namba moja? Taratibu zinasemaje kuhusu mbunge kudanganya makazi yake? Kama ni Mbunge na kweli anaishi Marekani, taratibu zinasemaje kwa mbunge kuwa na makazi yake nje ya nchi? Kama ni mbunge wa CHADEMA na anaishi Marekani, chama chake kinasemaje kuhusu kuishi kwake nje nchi? Hivi karibuni Mh Mbowe na Mh Wenje walikuwa Marekani, je walikutana na huyu mbunge wa chama chake? Chadema inaweza kueleza walipa kodi ni kwa nini mbunge wao anaishi Marekani?

  Mei 27, 2012, Zitto, John Mnyika, Mh. Joseph Mbilinyi, Mh Ezekiel Wenje, na Mh, Peter Msigwa watafanya mkutano Maryland, Marekani. Kwenye mkutano huo pia atakuwepo Mh Leticia Nyerere. Je, kama hizi tuhuma ni za kweli, hawa washimiwa wa Chadema wanaoenda Marekani kwenye huo mkutano wanasemaje kuhusiana na makazi ya mbunge mwenzao kuwa Marekani na tuhuma nyingine za kuwa na kesi zinazomkabili mahakani huko Marekani?

  Huyu mheshimiwa mbunge ameshakuwa na kesi 7 Marekani, tano zimeshafungwa na mbili bado ni active. kwenye kesi zote yeye alikuwa ni defendant. Mnaweza kuangalia wenyewe hapa: Maryland Judiciary Case Search (Maryland Judiciary Case Search). Ingekuwa bora kama Chadema badala tuu ya kukanusha kuwa mbunge wao amekamatwa pia watoe tamko juu ya tuhuma za mbunge wako kuishi marekani.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sio sawa...
   
 3. e

  environmental JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Wewe ukiwa na watoto nje ya nchi.Hutaenda kuwaona???????????????????.Wewe una watoto au mgumba.Maana nataka kujua hili ndio nione kama una uchungu wa mtoto.
   
 4. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wamarekani wamejenga nchi yao ndo maana imeendelea hivyo.Na sisi tujenge Tanzania yetu kama hamjaona maisha mazuri bongo.Kwa hiyo kukimbilia kule ni ushamba kama sio mpenda starehe
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Haijakaa sawa vile Dr Slaa yumo humu jamvini atolee ufafanuzi tafadhali
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Afadhali akaaye mbali unajua 100% kuwa haibi mali za nch kwasabu ni shida kujiingiza kwenye Mipango walakini; kuliko yuke ambaye kupo hapa hana cha kufanya ila kuzunguka mitaani, mabenki na wizarani kutafuta deals za kufisadi nchi.
   
 7. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mie niliposoma tu hii post,wazo likanijia kwamba,pengine wanachukua mfano toka kwa Mkuu wa Kaya!
  Kweli kuna atakayesema (JK)anaishi Tanzania??
   
 8. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  COURT OF MARYLANDGo Back
  [TABLE]
  [TR]
  [TD][h=5]Case Information[/h][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Court System:
  [/TD]
  [TD]DISTRICT COURT FOR PRINCE GEORGE'S COUNTY - CRIMINAL SYSTEM[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Case Number:
  [/TD]
  [TD]0E00486934Tracking No:082001216290[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Case Type:
  [/TD]
  [TD]CRIMINAL[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  District Code:
  [/TD]
  [TD]05Location Code:01[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Document Type:
  [/TD]
  [TD]CITATIONIssued Date:03/26/2012[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Case Status:
  [/TD]
  [TD]CLOSEDCase Disposition:TRIAL[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [HR][/HR][TABLE]
  [TR]
  [TD][h=5]Defendant Information[/h][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Defendant Name:
  [/TD]
  [TD]NYERERE, LETICIA M[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Race:
  [/TD]
  [TD]BLACK, AFRICAN AMERICAN[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Sex:
  [/TD]
  [TD]FHeight:508Weight:175DOB:03/01/1959[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Address:
  [/TD]
  [TD]2212 BRIGHTSEAT RD #301[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  City:
  [/TD]
  [TD]LANDOVERState:MDZip Code:20785 - 0000[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [HR][/HR][TABLE]
  [TR]
  [TD][h=5]Charge and Disposition Information[/h][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  (Each Charge is listed separately. The disposition is listed below the Charge)

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Charge No:
  [/TD]
  [TD]001Description:TRESPASS: PRIVATE PROPERTY[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Statute:
  [/TD]
  [TD]CR.6.403Description:TRESPASS: PRIVATE PROPERTY[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Amended Date:
  [/TD]
  [TD]CJIS Code:2 2220MO/PLL:Probable Cause:[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Incident Date From:
  [/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]To:[/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]Victim Age:[/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [h=5]Disposition[/h][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Plea:
  [/TD]
  [TD]OTHER PLEA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Disposition:
  [/TD]
  [TD]NOLLE PROSEQUI
  Disposition Date:
  05/22/2012[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [TD]Fine:$0.00Court Costs:$0.00CICF:$0.00[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Amt Suspended:
  [/TD]
  [TD]Fine:$0.00Court Costs:$0.00CICF:$0.00[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  PBJ EndDate:
  [/TD]
  [TD]Probation End Date:Restitution Amount:$0.00[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Jail Term:
  [/TD]
  [TD]Yrs:Mos:Days:[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Suspended Term:
  [/TD]
  [TD]Yrs:Mos:Days:[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Credit Time Served:
  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [HR][/HR][h=5]Related Person Information[/h](Each Person related to the case other than the Defendant is shown)

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Name:
  APGAR, PFC[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Connection:
  COMPLAINANT/POLICE OFFICER[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Agency Code:
  [/TD]
  [TD]BWAgency Sub-Code:CGOfficer ID:0130[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [HR][/HR][h=5]Event History Information[/h][TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD]Event[/TD]
  [TD]Date[/TD]
  [TD]Comment[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]DOCI[/TD]
  [TD]04/25/2012[/TD]
  [TD]CIT ISSUED 120326[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  This is an electronic case record. Full case information cannot be made available either because of legal restrictions on access to case records found in Maryland rules 16-1001 through 16-1011, or because of the practical difficulties inherent in reducing a case record into an electronic format.


  Kwa wenye uelewa vizuri wa maswala ya uhamiaji Marekani. Ni kigezo gani kinatumika kuitwa Black, African American kwa wazaliwa au wahamiaji nchini Marekani kama ilivyo kwenye hili faili la iliyokuwa kesi ya Leticia Nyerere
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,065
  Trophy Points: 280
  ..Monica Mbega wa CCM alikwenda nje kusoma wakati akiwa mbunge.

  ..Martha Mlata mbunge wa CCM viti maalum naye nimepata kusikia kwamba yuko Uingereza kwa muda mrefu.

  ..kuna mabalozi kama Dr.Pius Ngwandu na Emmanuel Mwambulukutu walituwakilisha nje ya nchi huku wakiwa ni wabunge wa kuchaguliwa.
   
 10. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Black African American? Tayari tushapitisha sheria ya uraia wa nchi mbili?
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Yalishajadiliwa sana kwenye hii thread lakini baadae comments zikapotea wakati wa marekebisho ya server.
   
 12. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna uhalisia - kwa nini tunawachagua? wana lipi la ziada watu wa aina hii?
   
 13. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu Mh. baada ya kupata mikasa ya sasa akavamia suala la kuhamasisha Chadema, lakini hata passport imeshikiliwa na Uhamiaji na hatoweza kusafiri bungeni. Bunge litamlipa tu bila kufanya kazi
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Angekuwa wa CCM anaishi nje!!!!! Pangechimbika!!! Kupenda kubaya!!
   
 15. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Na wewe unatafuta kushtakiwa eh?

  Leticia Nyerere kushitaki waliomkashifu

  MBUNGE wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA), ametishia kuwashitaki watu waliotoa taarifa katika vyombo vya habari, zikidai kuwa alikuwa amekamatwa na polisi kuhusiana na makosa aliyotenda nchini Marekani. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Leticia alieleza kusikitishwa kwake na taarifa hizo, akidai kuwa zimemdhalilisha na kumkashifu mbele ya jamii inayomheshimu na kumthamini, na hivyo atachukua hatua za kusafisha jina lake.

  Alisema tuhuma hizo zilizosambazwa katika moja ya mitandao hapa nchini na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, Mei 14, mwaka huu, zilikuwa za kutungwa, na zilizolenga kumchafua mbele ya Watanzania waishio Marekani na hapa nchini. Mbunge huyo alisema tayari ametoa taarifa kwa mamlaka za kisheria nchini Marekani, na tayari uchunguzi utaanza kuwanasa wale wote waliohusika kusambaza uzushi huo.

  Mei 14, mwaka huu, mtu aliyejitambulisha kama Amos Cherehani, akidai kuwa Katibu wa CHADEMA, tawi la Marekani, alisambaza taarifa za kukamatwa kwa mbunge huyo jijini Washington DC, kwa tuhuma za kutenda makosa mawili ya jinai, likiwemo la kujipatia kadi ya kijani (Green Card) kwa njia ya udanganyifu.

  Aidha, Cherehani ambaye alikuwa akiwaomba Watanzania kumchangia mbunge huyo fedha za kukabiliana na kesi hiyo, alisema anatuhumiwa kufanya kosa la kuvunja masharti ya dhamana, kwa kutofika mahakamani hapo Februari 10, mwaka huu, katika kile kilichosemwa ni kesi ya kutapeli dola 15,000 toka kwa mtu aliyetajwa kama dada Cooper.

  Hata hivyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na Leticia mwenyewe, na baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA, ambao walimtaka atoe maelezo ya kujisafisha kwa Watanzania. Wakati huo huo, mbunge huyo, amesema kuwa, uzinduzi wa tawi la CHADEMA katika mji wa Maryland nchini Marekani, utafanyika Mei 27.

  Leticia Nyerere kushitaki waliomkashifu
   
Loading...