Ni sawa kwa mawaziri kusherehekea baada ya bajeti zao kupitishwa?

Rwey

Senior Member
Jul 11, 2008
121
23
Wapendwa ndugu zangu,
Majuzi nilikuwa Dodoma kwa jamaa yangu mmoja, akawa amealikwa kwenye sherehe ya wizara fulani baada ya bajeti yao kupitishwa na bunge. Niliambiwa kulikuwa na waalikwa takribani 300.
Je gharama zote hizo zinabebwa na akina nani. Tuelezana bandugu
 
Wapendwa ndugu zangu,
Majuzi nilikuwa Dodoma kwa jamaa yangu mmoja, akawa amealikwa kwenye sherehe ya wizara fulani baada ya bajeti yao kupitishwa na bunge. Niliambiwa kulikuwa na waalikwa takribani 300.
Je gharama zote hizo zinabebwa na akina nani. Tuelezana bandugu

Fedha zinazotumika hapo huwa ni yale mabaki yote ya fedha za mwaka wa fedha unaoisha. Kwa hiyo badala ya kuzirudisha hazina zote zinakusanywa kwenye kapu moja na kuliwa, mwenye kunywa pombe sawa, mwenye kufisasdi baadhi ya hizo fedha na kuziochota twende. Yaani hapa ni kufuru tupu ni kula, kunywa na kuiba kwa kwenda mbele. Si ajabu sherehe uliyoshuhudia ya watu takribani 300 ukakuta matumizi yanasema walikuwa 500 au zaidi. Wajinga ndi tuliwao!!!
 
Kusherehekea sawa kwa fedha zao... lakini please waache fedha zetu!

Unaota wewe, fedha zao?halafu taxpayer's money atumie nani?unadhani wanamuachia rostam,karamagi,chenge na lowassa zote?naaaaaaah ndio hizo marupurupu kibao na fedha za kujichomea nyama na jack daniels mara mojamoja na matumbo ya wanaume makubwa kama wana mwanandani
 
Wakati mwingine huwa ninasema kwamba sioni sababu ya kuwa na bajeti kwa kuwa waziri anaweza kufanya maamuzi mengine kinyume na jinsi alivyopangiwa kwenye bajeti. Wizara zingekuwa ziko strict na matumizi kulingana na bajeti hizi fedha za shughuli zisizo rasmi wala zisingepatikana.

Zama zile za "JK Boys" (Taifa Stars) ilipotoka Burkina Faso ikatua Dodoma, Chenge akiwa Wizara ya Miundombinu aliwakatia fedha kutoka kwenye wizara yake (sikumbuki zilikuwa bei gani), wakati hayo yanafanyika barabara hazipitiki na hao JK Boys hawako chini ya wizara ya miundombinu. Kama hilo fungu lingetoka kwenye wizara inayohusika na hayo mambo ya michezo ningeona ni swala la kawaida.

No wonder kunakuwa na sherehe kama hizo ambazo zinatumika kufuja fedha za walipa kodi. Wanapongezana nini wakati ni sehemu ya majukumu yao? Sijawahi kusikia haya mambo kwenye nchi zilizo makini, ni Tanzania tu ambapo kila kitu tunapongezana kwa ushajaa wa kuwadanganya watanzania. No wonder Chenge na Mamvi walipokewa kama mashujaa huku wakiwa wamezungukwa na tuhuma za ufisadi.
 
Rwey,

..Watanzania ni watu wazuri sana ktk kuwasoma viongozi wao.

..sasa hivi watu wameona huu uongozi unapenda pati-pati na tafrija.

..bajeti ya wizara ikipitishwa na halafu msisherehekee kwa namna yoyote ile mtaonekana ni watu wa ajabu kidogo, na zaidi tishio.
 
hawa watajuwa wachuro hawa mawaziri, itakuwa ni short sightedness ya akili hii!
 
Wapendwa ndugu zangu,
Majuzi nilikuwa Dodoma kwa jamaa yangu mmoja, akawa amealikwa kwenye sherehe ya wizara fulani baada ya bajeti yao kupitishwa na bunge. Niliambiwa kulikuwa na waalikwa takribani 300.
Je gharama zote hizo zinabebwa na akina nani. Tuelezana bandugu

Rwey, gharama zinabebwa na wewe na mimi.
Hawa Mawaziri wana kila sababu ya kusheherekea maana wanajua wazi kuwa kama Bunge na Wabunge wako makini basi hawawezi kupitisha hizo Bajeti zao maana huwa wanajua wazi kuwa zina mapungufu mengi mno.

Kufanya sherehe baada ya bajeti kupitishwa inaashiria kuwa Pesa zilizopitishwa mwaka ulioisha hazikutumika zote na mambo mengi hayakutekelezwa kwa hiyo kulikuwa na uwezekanao Wabunge wagomee hizo bajeti zao.

Sijui kwa nini Wabunge hawamuulizi hilo swali lako Waziri Mkuu kwenye maswali ya moja kwa moja kila Alhmisi! Zitto, Mama Malecela, Dk. Slaa, Hamad Rashid, Zambi mko wapi? Hilo ndo swali!

Je, Mawaziri wanatoa wapi pesa za kusheherekea bajeti zao kupitishwa?
 
Hii sasa kali wanajipongeza ili iweje???Huu ni ufisadi tu hakuna kingine tulisha sema hapa Tanzania hatuna viongozi wote ni wasanii tu hakuna kitu kwenye vichwa vyao kazi kujaza matumbo yao kwa fedha zetu walalahoi.
 
wanafanya tafrija kwa sababu gani, wengi wao hata hawajui nini hasa kimo kwenye zile bajeti, wengi wao bajeti zao ni uchwara.
Tatizo la mawaziri wa Tanzania Kila kinapofika kipindi cha bajeti hujifua kama mwanafuzi anayeenda kwenye mtihani, na mwanafunzi huyo akifaulu hufanya sharehe, kesha sahau kama kufaulu ilikuwa wajibu wake, ni sawa na hawa mawaziri wetu NJAA KALI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom