Ni sawa kwa mawaziri kusherehekea baada ya bajeti zao kupitishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sawa kwa mawaziri kusherehekea baada ya bajeti zao kupitishwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rwey, Jul 16, 2008.

 1. R

  Rwey Senior Member

  #1
  Jul 16, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wapendwa ndugu zangu,
  Majuzi nilikuwa Dodoma kwa jamaa yangu mmoja, akawa amealikwa kwenye sherehe ya wizara fulani baada ya bajeti yao kupitishwa na bunge. Niliambiwa kulikuwa na waalikwa takribani 300.
  Je gharama zote hizo zinabebwa na akina nani. Tuelezana bandugu
   
 2. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2008
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Fedha zinazotumika hapo huwa ni yale mabaki yote ya fedha za mwaka wa fedha unaoisha. Kwa hiyo badala ya kuzirudisha hazina zote zinakusanywa kwenye kapu moja na kuliwa, mwenye kunywa pombe sawa, mwenye kufisasdi baadhi ya hizo fedha na kuziochota twende. Yaani hapa ni kufuru tupu ni kula, kunywa na kuiba kwa kwenda mbele. Si ajabu sherehe uliyoshuhudia ya watu takribani 300 ukakuta matumizi yanasema walikuwa 500 au zaidi. Wajinga ndi tuliwao!!!
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kusherehekea sawa kwa fedha zao... lakini please waache fedha zetu!
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unaota wewe, fedha zao?halafu taxpayer's money atumie nani?unadhani wanamuachia rostam,karamagi,chenge na lowassa zote?naaaaaaah ndio hizo marupurupu kibao na fedha za kujichomea nyama na jack daniels mara mojamoja na matumbo ya wanaume makubwa kama wana mwanandani
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2008
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wakati mwingine huwa ninasema kwamba sioni sababu ya kuwa na bajeti kwa kuwa waziri anaweza kufanya maamuzi mengine kinyume na jinsi alivyopangiwa kwenye bajeti. Wizara zingekuwa ziko strict na matumizi kulingana na bajeti hizi fedha za shughuli zisizo rasmi wala zisingepatikana.

  Zama zile za "JK Boys" (Taifa Stars) ilipotoka Burkina Faso ikatua Dodoma, Chenge akiwa Wizara ya Miundombinu aliwakatia fedha kutoka kwenye wizara yake (sikumbuki zilikuwa bei gani), wakati hayo yanafanyika barabara hazipitiki na hao JK Boys hawako chini ya wizara ya miundombinu. Kama hilo fungu lingetoka kwenye wizara inayohusika na hayo mambo ya michezo ningeona ni swala la kawaida.

  No wonder kunakuwa na sherehe kama hizo ambazo zinatumika kufuja fedha za walipa kodi. Wanapongezana nini wakati ni sehemu ya majukumu yao? Sijawahi kusikia haya mambo kwenye nchi zilizo makini, ni Tanzania tu ambapo kila kitu tunapongezana kwa ushajaa wa kuwadanganya watanzania. No wonder Chenge na Mamvi walipokewa kama mashujaa huku wakiwa wamezungukwa na tuhuma za ufisadi.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jul 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  Rwey,

  ..Watanzania ni watu wazuri sana ktk kuwasoma viongozi wao.

  ..sasa hivi watu wameona huu uongozi unapenda pati-pati na tafrija.

  ..bajeti ya wizara ikipitishwa na halafu msisherehekee kwa namna yoyote ile mtaonekana ni watu wa ajabu kidogo, na zaidi tishio.
   
 7. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mi nilishasema hatuna bajecti tuna mchezo wa redio.
   
 8. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hawa watajuwa wachuro hawa mawaziri, itakuwa ni short sightedness ya akili hii!
   
 9. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hii wanafanya kwasababu tunawapenda sana..??
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Rwey, gharama zinabebwa na wewe na mimi.
  Hawa Mawaziri wana kila sababu ya kusheherekea maana wanajua wazi kuwa kama Bunge na Wabunge wako makini basi hawawezi kupitisha hizo Bajeti zao maana huwa wanajua wazi kuwa zina mapungufu mengi mno.

  Kufanya sherehe baada ya bajeti kupitishwa inaashiria kuwa Pesa zilizopitishwa mwaka ulioisha hazikutumika zote na mambo mengi hayakutekelezwa kwa hiyo kulikuwa na uwezekanao Wabunge wagomee hizo bajeti zao.

  Sijui kwa nini Wabunge hawamuulizi hilo swali lako Waziri Mkuu kwenye maswali ya moja kwa moja kila Alhmisi! Zitto, Mama Malecela, Dk. Slaa, Hamad Rashid, Zambi mko wapi? Hilo ndo swali!

  Je, Mawaziri wanatoa wapi pesa za kusheherekea bajeti zao kupitishwa?
   
 11. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kusherekeha uku maana yake ni kwamba
  Wizara inajua kabisa madudu yaliyomo kwenye bajeti zake jamani, sasa wanapofanikiwa kuwadanganya Wabunge na wengine kupewa hongo ili mradi bajeti zao za kishenzi zipite ndio maana wanaenda kusherekea wakijua kuwa wamefanikiwa kutupiga chenga tena watanzania

  Nina swali tofauti kidogo please mtanisamee bandugu

  Mwaka 2006 baada ya JK kuingia Madarakani kila siku ya Mungu magazeti yalikuwa yakitoa mambo ambayo Jk amekuwa akifanya kila siku takriban kwa mwezi mmoja hivi!! tena watu wakawa wanasema huyu ndiye rais moto wa kuotea mbali

  Hivi sasa hivi mbona kawa bubu, maana sidhani kama hata yuko kabisa, kafunikwa na Mafisadi?
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii sasa kali wanajipongeza ili iweje???Huu ni ufisadi tu hakuna kingine tulisha sema hapa Tanzania hatuna viongozi wote ni wasanii tu hakuna kitu kwenye vichwa vyao kazi kujaza matumbo yao kwa fedha zetu walalahoi.
   
 13. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  wanafanya tafrija kwa sababu gani, wengi wao hata hawajui nini hasa kimo kwenye zile bajeti, wengi wao bajeti zao ni uchwara.
  Tatizo la mawaziri wa Tanzania Kila kinapofika kipindi cha bajeti hujifua kama mwanafuzi anayeenda kwenye mtihani, na mwanafunzi huyo akifaulu hufanya sharehe, kesha sahau kama kufaulu ilikuwa wajibu wake, ni sawa na hawa mawaziri wetu NJAA KALI.
   
Loading...