Ni sawa kumkopesha mchumba pesa ya kufanyia biashara ili apate hela ya kulipa mahari?

Hakuna kosa kubwa utakalofanya humu duniani kama kumkopesha hizo pesa. Acha kabisa,na ukimkopesha hatakuja tena kukuoa,na ndio utakuwa umemfukuza,maana hutaweza kuja kumdai,na biashara isipofanikiwa mtaji ukafa hatathubutu kurudi kwako na ndio utakuwa umempoteza mazima.

Acha hiyo biashara ya kumkopesha mchumba.
 
Sio sahihi kabisa kwa maelezo yako tu inaonyesha Huyo mchumba hana lengo zuri nawe

Kumpenda isiwe sababu ya kuutumia upendo wako kujinufaisha,narudia tena kwa mkazo "Usijaribu kumkopesha hela" Huyo

Kama ana malengo apambane kama hataki hela za ndugu,marafiki je?,bila shaka anao wamkopeshe au mwambie akope TALA
Yaap ameanza hizo inshu baada ya kuona nimekolea akajua siwezi chomoka,ilitokea kuna siku aliniambia yupo vibaya, hana hata pesa ya kula nikamsaidia, Naona Sasa imekuwa Mazoea.
mwambie huwezi kukopa sababu ndugu zako wana masimango pia.
Hili nalo neno
 
Ukimpa hiyo hela trust me,disemba ikifika atakuambia biashara sio nzuri wala haina faida..halafu kitu kingine ukimpa ni sawa na "umejioa" hapo katumia neno biashara lakini ukitafakari ni wazi anakuambia ujilipie mahali mwenyewe,.na ukimpa tuu jua umejioa bibie..

tuliza kizazi,.kama anakupenda kweli utaona juhudi..
Hahah Asante kwa ushauri,
 
Kuomba kupunguziwa mahari ni swala la muoaji namshenga mwambie uhusiki kwa hilo.

Kuhusu kumkopesha hela ya biashara sio sahihi mara nyingi hawarudishi kwa kisingizio cha mahusiano
 
Kumkopesha mchumba ambaye anajulikana kwemu afanye biashara kwa manufaa yenu siyo jambo baya, ubaya ni kumpa pesa mtu ambaye hajulikan kwenu... Hata hvyo, hela ya mahari kutoa mwanamke ni kukaribisha mikosi
 
Acha kuingia katika majaribu ambayo hutayaweza, huyo mmeo mtarajiwa ameanza kuwa tegemezi hatua za mwanzo hivyo ikifika katika malezi ya watoto na usomeshaji usitegemee mabadiliko.

Nina mtu wangu wa karibu alipewa posa na mchumba wake wa kike na kupeleka kwao kilichofuata yule binti analalamika hadi leo.

Hebu acha kuhangaika nae uone atafanya nini.
Nimeipenda hii aache kuingia kwy majaribu ambayo hatayaweza
 
uki sahih maisha n kusaidiana na tayar mtu ameshaonesha nia napata gagaziko labsa hawana muda mref ndio mana anahofia hata hivo kama ulivyosema uko sahihi mapenzi ni kujitoa hasa pesa zikiliwa bas bwana lakini akifanikisha s ndio kaipata ndoa na yeye
Yeah ndio inatakiwa hio, wengine tunachukuaga mpaka 2 millions tukiyumba sembuse laki 5 tu! Na maisha yanaenda tu
 
Kuwa makini Dada...huyo anakutumia kama ngazi yake ya kufikia malengo..hapo ukishamkopesha ataanza mauzauza Mara ooh biashara imekuwa mbaya..Mara hela hionekan...Mara utanidaije hela mm chumba wako n.k...mwisho anakupotezea mazima...yeye anadai hawez kukopa kwa ndugu maana wana masimango kwan wewe ndo unapenda kukopa kwa ndugu?? Kwani ndugu zako ndo hawana masimango?....acha kabisa sikushauri kumkopesha hiyo hela
Kama kweli yeye n mwanaume anayejielewa na mwenye nia ya dhat ya kukuoa basi akomae atafute hela ya kufanya hiyo biashara yake akalipe hiyo mahari...ukijichanganya hapo utajuta baadaye.
 
Wanaonijua wachache tu!
bora wewe mimi hakuna anaenijua kwao wala kwetu hakuna anayemfahamu. Na kuna siku tulipanga kukutana sehemu, mimi Ndio nilianza kufika eneo husika,alipofikka yeye kwa mbali akaniona nimekaa na dada mmoja nilisoma nae ila tulikutana Hapo Hapo, yeye hakujua hilo akadhan nimeenda na ndugu Yangu, uweZi amini alinitumia SMS Kali saana, Kwamba yy anaondoka hawez kuonana na mm nimeenda na ndugu na kwamba yy hataki kujulikana kwa wakati huu, anachonishanaza anataka ndoa mwez wa nne.
 
bora wewe mimi hakuna anaenijua kwao wala kwetu hakuna anayemfahamu. Na kuna siku tulipanga kukutana sehemu, mimi Ndio nilianza kufika eneo husika,alipofikka yeye kwa mbali akaniona nimekaa na dada mmoja nilisoma nae ila tulikutana Hapo Hapo, yeye hakujua hilo akadhan nimeenda na ndugu Yangu, uweZi amini alinitumia SMS Kali saana, Kwamba yy anaondoka hawez kuonana na mm nimeenda na ndugu na kwamba yy hataki kujulikana kwa wakati huu, anachonishanaza anataka ndoa mwez wa nne.
Duh, basi jamaa analeta mashaka, kwanini hayupo free ama anakusanii! Mlianzaje hayo mahusiano?
 
Nyumbani hajulikani sasa hiyo mahari katajiwa na nani? na kajuaje kubwa ? Kwa nini we ndio umkopeshe? Hapo hakuna muoaji huyo ni marioo anataka ahongwe nae eti haamini kwenye kuajiliwa anakutengeneza tu huyo hakuna mjasiliamali hapo wala nini anataka mtelezo tu
 
Mmmmmmmm pole sana huyo ni mzigo achana nae, kabla ya kutuma ujumbe uwe unasoma kwanza ili kurekebisha makosa.
 
Nyumbani hajulikani sasa hiyo mahari katajiwa na nani? na kajuaje kubwa ? Kwa nini we ndio umkopeshe? Hapo hakuna muoaji huyo ni marioo anataka ahongwe nae eti haamini kwenye kuajiliwa anakutengeneza tu huyo hakuna mjasiliamali hapo wala nini anataka mtelezo tu
Haha jamaa kashajipangia na mahari kabisa eti nimwambie mzazi atatoa kiasi fulani, nikamwambia siwezi mwambia mzazi wangu atanambia nataka kujioa
 
Thanxs kwa ushauri dear, nandivo nilivo mjibu kwamba ananambia nikaongee na wazazi wangu wampunguzie mahali kama nampenda,ili tuoane mapema, nikamwambia siwezi mzazi wangu ataona najioa akaanyamaza kimya
Baadhi ya wanaume wa siku hizi bhana..... Kichefuchefu....!!!!
 
Back
Top Bottom