Annina
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 437
- 57
Kuna tabia kwa baadhi ya wazee wetu hasa waishio mijini kufanya mambo ya ajabu yasiyoendana na umri wao kama vile kuwa na mahusiano na vijana wadogo kwa kisingizio cha kukemea uzee! Nina mifano kadhaa, kuna mzee mmoja pale mikocheni huwa hakosekani bills anadai muziki wa sasa ni mtamu sana na anausikia mpaka kwenye damu! Pia ana kazi ya kuvimaliza vibinti vya sekondari anasema vinampa joto sana na anajisikia bado anadai - anakemea uzee!
Si ajabu tena siku hizi kukuta mama mtu mzima amejichuna ngozi, kichwani kajitwisha kichaka cha nguvu, kapiga kimini au top inayoacha sehemu kubwa ya mwili nje huku pembeni akiwa na kaserengeti boy katika harakati za kukemea uzee! Kuna mama mmoja alipoulizwa juu ya tabia yake hii alisema uzee unaanzia chalinze Dar hakuna mzee!
Sasa najiuliza, hakuna njia nyingine ya kukemea uzee (kama uzee ni lazima ukemewe) zaidi ya hii inayoenda kinyume na maadili yetu?