Ni sawa kabisa unachosema mtaalamu wa masuala ya utalii

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
2,469
1,697

Ni sawa kabisa unachosema mtaalamu wa masuala ya utalii. Nimependa sana hoja yako.

Lakini kitu ambacho sisi hapa tunazungumzia au Mbunge Lema kumaanisha na wewe kupaswa kutuelewa ni kuwa je, lazima iwe Dreamliner ya $ 262 milioni katika kuboresha sekta ya anga? Je, isingetosha ndege ndogo za abira 50 mpaka 70 kwa safari zetu za ndani na majirani zetu? Kwa bei hiyo nafikiri tungeweza pata ndege hata mbili au tatu na kwa ujumla ndege nne au sita kwa Dreamliner mbili.

Ukichukua gharama za manunuzi ya hizo ndege mbili na gharama za uendeshaji sidhani kama faida za ajira zitakazo patikana na mafanikio ya hizo sekta ulizo zitaja zitaweza leta kipato kikubwa sana kwa taifa.

Usafiri wa anga humu ndani kama kwenye mbuga zetu za wanyama na tourist attractions nyingine nchini na labda nchi jirani kama Zambia, Zimbabwe, Burundi, Malawi na DRC, ni sawa kabisa tuna uhitaji usafiri wa anga, lakini sio kwa ndege kubwa za masafa marefu kama Boeing 787.

Kwa baadae kama uchumi wetu utakua zaidi na kupata fursa za kupiga masafa marefu kama Bombay, China, Europe na Amerika hapo sawa tutazihitaji hizo ndege.

Kwa hivi sasa, kwa mtazamo wangu, ni matumizi mabaya ya pesa za umma kwa vitu ambavyo havina faida kubwa sana.

Hizo hela angeweza kuzitumia katika miradi ambayo ingekuwa na direct impact kwa vijana wetu wasio na ajira ambao wanahangaika na biashara za umachinga.

$ 524 milioni za hizo ndege zingetosha kabisa kujenga mtambo wetu wenyewe mdogo wa kusindika gas yetu ya asilia LNG na kuwawezesha watu wengi hasa vijana kuwa na ajira katika usambazaji wa LNG ndani na nje ya nchi.

Vijijini kote watanzania wasinge kuwa wanaharibu mazingira kwa kukata miti kama energy source kwa matumizi ya kuni kupikia.

Ukiongeza na mitambo au furnaces za kuoka chuma yetu wenyewe na mabati yetu vijana wengi wangekuwa wanajishughulisha na ubunifu wa kutengeneza vitu kama majiko ya kutumia LNG yetu na hivyo kupanua ubongo wao katika kuongeza ujuzi na maarifa ya matumizi ya chuma na LNG.

Kwa hali hiyo wabobeajiaji wa material science and engineering profession na professions kama za Industrial Designers, Design Engineers zingeweza kuibuka kwa wingi. Design Engineers wanashirikiana au wanacollaborate na maengineer wote wengine kama; Process, mechanical, chemical, civil, electrical, textile, Aerospace na system Engineering

Kwa mtazamo wangu nchi zilizopiga hatua kubwa sana za maendeleo kwa haraka ulimwenguni ni zile ambazo ziliipa kipao mbele studies za Metallurgy na professions kama industrial designers na Design Engineers.

Bila hawa watu ni vigumu kuwa na watu wenye uwezo wa ku create consumer products na manufactering products.

Muda wote tunahangaika na structural na civil engineers. Na hata hivyo serikali haijaweza kuwa hamasisha watanzania kwenye professions ambazo zinaweza kutumia rasilimali zetu.

Wengi wetu ni matheoreticians ambao hawa jiamini katika kutenda bali katika kutendewa.

Natoa mfano; huyu kijana Benjamin Fernades
Serikali imechukua mipango au hatua gani kushirikiana naye katika kutekeleza ambitions zake ambazo zitawasaidia vijana kutumia uwezo na utaalamu wake?

Rais Magufuli anatumia hela nyingi kuwapeleka watanzania kusoma nje badala ya kumtumia huyu kijana.

Mnaona jinsi gani tulivyokuwa malimbukeni wa kuharibu resources zetu kama za huyu kijana?

Ni kitu cha kushangaza sana kuona Rais Magufuli amewaibua watengenezaji wa umeme kwa kutumia maji huko Ruvuma, lakini anashindwa kumwinua huyu kijana kuieneza technology yake ambayo itatuletea sisi umaarufu na vijana wetu kupata shughuli za kujiingizia mapato? Ni kitu cha kusikitika sana.

Kwa Magufuli ni afadhali kuwasifia matajiri kama akina Mohamed Dewj Enterprise ambao hawana mpango wowote wa kuwaendeleza watanzania kiteknolojia badala ya kuendeleza vijana wenye vichwa na mawazo mazuri ya kimaendeleo.

Serikali ilipaswa ku-invest kwa huyu kijana katika malengo yake badala ya kununua madudu ambayo anatumia kujitambia kwa Marais waliopita. Ya nini hayo?

Rais Magufuli, ndiyo yuko poa, lakini sijaona umuhimu wa kujigamba na ndege ambazo wametengeneza wengine na sisi ni watumiaji tu.

Ni aibu kubwa kuwahamasisha vijana wawe wachuuzi badala ya kuwahimiza katika uwezo wa product creation kwa kuwajengea misingi.

Rais Magufuli namuomba atambue kuwa hakuna sekta binafsi ambayo itakuwa na uwezo wa ku invest kwenye kitu ambacho hawajui out come yake.

Serikali inatakiwa katika mambo mengine ijitose tu. Mengineyo yote yatajulikana baadae. Chuma gas si yetu? Tatizo ni nini? Hakuna mtu atakuja kutudai.
 
Back
Top Bottom