Ni sawa Benki Kuu kutumia bilioni 5.8 kulipia Bima ya Afya?

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
887
705
Nchi yetu bado inajikongoja kutoka katika lindi la umaskini {Kijamii,kiuchumi,kisayansi}.
Mahitaji ya kuijenga nchi ni makubwa sana kila iitwapo leo {Afya,Elimu,Miundombinu,n.k}.

Jitihada za kukusanya kodi ,mapato,tozo zinafanywa kwa jitihada kubwa sana...Kilio cha mzunguko wa fedha kupungua kinasikika kila kona.Riba kubwa katika taasisi za fedha ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wetu.

Utafutaji wa masuruhisho kupitia mipango kitita na mipango mikakati kuondoa kero ya umaskini wa kipato bado changamoto kubwa sana kwa viongozi wetu wa sasa na baadae.

Ni sahihi kwa BOT kutenga na kutumia kiasi cha Tsh Bilion 5.82 Kulipia huduma za bima ya Afya {2016} ?Tena kwa kampuni binafsi {Jubilee Insurance}?..

Sina neno na mchakato wa zabuni, sihoji kwanini bima husika haikununuliwa Shirika la bima la taifa wala kwanini BOT haikujiunga na NHIF
 
Nchi yetu bado inajikongoja kutoka katika lindi la umaskini {Kijamii,kiuchumi,kisayansi}.
Mahitaji ya kuijenga nchi ni makubwa sana kila iitwapo leo {Afya,Elimu,Miundombinu,n.k}.

Jitihada za kukusanya kodi ,mapato,tozo zinafanywa kwa jitihada kubwa sana...Kilio cha mzunguko wa fedha kupungua kinasikika kila kona.Riba kubwa katika taasisi za fedha ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wetu.

Utafutaji wa masuruhisho kupitia mipango kitita na mipango mikakati kuondoa kero ya umaskini wa kipato bado changamoto kubwa sana kwa viongozi wetu wa sasa na baadae.

Ni sahihi kwa BOT kutenga na kutumia kiasi cha Tsh Bilion 5.82 Kulipia huduma za bima ya Afya {2016} ?Tena kwa kampuni binafsi {Jubilee Insurance}?..

Sina neno na mchakato wa dhabuni,sihoji kwa bima husika haikununuliwa Shirika la bima la taifa..Wala kwa nini BOT haikujiunga na NHIF...
Habari yako haijitoshelezi a imekaa kichochezi,..kwani kwa kawaida ilipaswa watenge kiasi gani kwa shughuli hiyo?? Umefanya mlingamisho a mashirika mengine umeona utofauti gani?
 
Kinachonishangaza ni unafiki mkubwa wa mawaziri na makatibu wakuu kukubali kulipwa mshahara mdogoooooo kuliko ule wanaopata mabosi wa mashirika ya umma wanayoyasimamia!! Lakini imegundulika kuwa wanayatafuna hayo mashirika kwa mgongo wa nyuma.

Wafanyakazi wa serikali kuu ambao ndio guardian wa mashirika hayo wanaishi maisha ya dhiki na ofisi zao kinyaa. Lakini shida hii huwa haiwahusu wakuu wa wizara husika.
 
Magufuli anatakiwa aingilie kati kuzuia haya matumizi holela. Kwa nini wafanyakazi wa BOT, TRA na TANESCO hawajiungi NHIF kama watumishi wengine wa umma? Kwani wao wana uspesho gani? Nadhani Magufuli alikuwa hana taarifa hizi na naamini atachukua hatua. Ama vinginevyo na sisi tuambiwe kama kujiunga NHIF ni hiari ama vipi. Hizi ni double standards.
 
BOT 2014/2015 REPORT:
The Bank of Tanzania is an equal opportunity employer with a total of 1,389 staff as at 30 June 2015
(2014: 1,320) out of which 60.0 per cent (2014: 59.2 per cent) were male and 40.0 per cent (2014:
40.8 per cent) were female.
 
TZS 5,824,940,169 Ukigawanya na idadi ya wafanyakazi 1389 unapata wastani wa premium ya TZS 4,193,621 kwa kila mfanyakazi na wategemezi stahiki.

Ikumbukwe gharama za mirahaba ya bima huwa ni asilimia 1 mpaka 4 {Wabobezi wanaweza fafanua} ya gharama za uhalisia.

Mathalani gari yenye thamani ya milioni 15 bima yake yaweza kuwa asilimia 4 ya thamani yaani Tzs 600,000 {VAT Exclusive}.

Hatuna budi kujitafakari hasa katika matumizi yasio na tija kwa taifa.Uzalendo uwekwe mbele dhidi ya matakwa binafsi.Tanzania ni yetu leo,kesho na keshokutwa.
 
Back
Top Bottom