Ni sawa Benki Kuu kutumia bilioni 5.8 kulipia Bima ya Afya?

Nini kifanyike?

Sheria ya Manunuzi ya Umma ina kidhi viwango vya mahitaji ya uhalisia kitaifa?

Taasisi za umma zenye matumizi ya anasa ya fedha za watanzania zifanyweje?
 
Nchi yetu bado inajikongoja kutoka katika lindi la umaskini {Kijamii,kiuchumi,kisayansi}.Viongozi wetu wazalendo wanajitahidi kunyoosha yaliopinda ili kujenga taifa lenye neema.

Mahitaji ya kuijenga nchi ni makubwa sana kila iitwapo leo {Afya,Elimu,Miundombinu,n.k}.Jitihada za kukusanya kodi ,mapato,tozo zinafanywa kwa jitihada kubwa sana...Kilio cha mzunguko wa fedha kupungua kinasikika kila kona.Riba kubwa katika taasisi za fedha ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wetu.

Utafutaji wa masuruhisho kupitia mipango kitita na mipango mikakati kuondoa kero ya umaskini wa kipato bado changamoto kubwa sana kwa viongozi wetu wa sasa na baadae.Ni sahihi kwa BOT kutenga na kutumia kiasi cha Tsh Bilion 5.82 Kulipia huduma za bima ya Afya {2016} ?Tena kwa kampuni binafsi {Jubilee Insurance}?..
 
..hawa jamaa utadhani tume wa import kumbe woote wana asili ya ikalinzi,igominyi,kishimundu,mwitongo,mkoka,buselasela,kolandoto,dongodesh,katelelo....hey few to mention
 
Pesa kama hizo ndizo zimetumika kuinunua UDA na kuitoa mikononi mwa Wananchi wa Dar kwenda kwenye umiliki wa Mtu mmoja. Ama kweli nchi hii yabela mitwe!
 
Yale yale! Mbona wafanyakazi wa Tanesco wapatao 6,000 hawalipii umeme? Nani aliota wendawazimu huu????
 
Kwa kuongezea mleta mada, sio tu BOT bali ni karbia mashirika yote ya umma kama vile mifuko ya hifhadhi ya jamii, bima, TIRA, TRA, TPA, TANAPA n.k. Wafanyakazi wa haya mashirika wanaishi kama malaika. Pamoja na kula mishaara mikubwa lakini bado wanakopeshwa bila riba, wanapewa kadi ambazo kila mwezi wanawekewa ela ya mafuta na maposho kibao. Ndo uone watanzania hatupendani kabisa. Ndo mtu unajiuliza wafanyakazi wengine kama walimu walimkosea nini mwenyezi Mungu, wanaishia kuona watu wengine wafaidi keki ya taifa.
 
Hao NHIF wanabebwa tu na shinikizo la kisheria, ukifungulia taasisi za umma ziwe na uhuru wa kuchagua mfumo wa bima ya afya kwa kuzingatia taratibu za manunuzi ya uma utashangaa kitakachotokea..
 
Nchi yetu bado inajikongoja kutoka katika lindi la umaskini {Kijamii,kiuchumi,kisayansi}.
Mahitaji ya kuijenga nchi ni makubwa sana kila iitwapo leo {Afya,Elimu,Miundombinu,n.k}.

Jitihada za kukusanya kodi ,mapato,tozo zinafanywa kwa jitihada kubwa sana...Kilio cha mzunguko wa fedha kupungua kinasikika kila kona.Riba kubwa katika taasisi za fedha ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wetu.

Utafutaji wa masuruhisho kupitia mipango kitita na mipango mikakati kuondoa kero ya umaskini wa kipato bado changamoto kubwa sana kwa viongozi wetu wa sasa na baadae.

Ni sahihi kwa BOT kutenga na kutumia kiasi cha Tsh Bilion 5.82 Kulipia huduma za bima ya Afya {2016} ?Tena kwa kampuni binafsi {Jubilee Insurance}?..

Sina neno na mchakato wa zabuni, sihoji kwanini bima husika haikununuliwa Shirika la bima la taifa wala kwanini BOT haikujiunga na NHIF
Bila kupepesa macho hiyo si sawa, Kwa nini wanatumia pesa zote hizo kuifahidisha kampuni binafsi, tena la kigeni wakati lipo shirika la serikari NHIF linalo toa huduma hiyo hiyo?
Hivi ni lini watanzania watathamini vya nyumbani hasa mashirika ya uma?, hatujifunzi tu kutoka kwa wachina walivyo thamini mashirika yao ya uma ambayo leo hii ndio yanayo ongoza kwa kufanya biashara na uwekezaji ulimwenguni kote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom