Ni sahihi watumishi wa umma kumiliki simu mbili au zaidi kila moja ikiwa na thamani ya zaidi ya milion mbili?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Mishahara ya watumishi wa Umma nimikubwa kiasi gani? Unatembelea ofisini kwa mtu unamiuta anasimu tatu smartphone zenye thamani ya si chini ya milioni mbili kila moja, unajiuliza haya mafedha wanayatoa wapi?

Je, huu ni utajiri au nikukosa elimu ya matumizi za fedha? Inaweza kuwa tunashangaa V8 za wakurugenzi kumbe tatizo linaanzia huku chini ambapo badala yakufanya Mambo yanayogusa jamii wamejikita kwenye anasa zisizofaa.

Kama mtu anamiliki simu za milioni nane hadi kumi unategemea huyu ukimpa madaraka makubwa atawajali wananchi wachini au atazidi kujilimbikizia Mali?

Hawa wenye masimu kibao ukiwafuatilia huko walipotoka wapo ndugu zao hawana ada na kwa wao kushindwa kugawanya vipato vyao wamepelejea nchi kuendelea kuwa na tatizo kubwa la umaskini.

Yamkini angeacha kununua simu hizi zisizo na kazi angewekeza kwenye biashara na angeajiri watu kadhaa tatizo la ajira lingepungua.

Hapa najadili simu ila vipo vingi vyakujadili ambavyo tusipovikemea tunatengeneza taifa la walafi wakati nchi yetu umezaliwa kwenye ujamaa.
 
Wivu tu, kupanga ni kuchagua. Mtu akope benki anunue sim kwa 10 mill wewe inakuhusu nini? Kama hatumii fedha ya umma mwache afurahie maisha yenyewe mafupi haya. Lakini kama anatumia Pesa ya serikali hapo achukuliwe hatua.
 
Humo ofisini ukikuta computer (desktop) ya milioni 10 hushangai lakini mtumishi akishika simu ya mkononi ya milioni 10 unashangaa!!! Hiyo simu ya mtumishi inafanya kazi sawa na hiyo computer ya mezani na imenunuliwa na ofisi. msiwatoe roho ndugu zenu kisa simu ya milioni nane! Mvon huhoji V8 anayotumia?
 
Hakuna pumbafu kama huyu jamaa anataka wamiliki cm ya bei gani sasa.

Au basi aiambie serikali igawe vitochi bure
Yaani pumba squared
 
Sasa kuna tatizo gani mkuu kama mtu kabaingaiza kapata simu zake mna taka tupangiane tena? Mbona masau bwire anazo nyingi tu
 
Kuna kitu kinaitwa "scale of preference". Nina rafiki yangu humwambii kitu kuhusu magari. Hana nyumba, hana mradi wowote, lakini kubadili magari ndio hobby yake. Hashauriki. Kazini kwake ana mkopo, CRDB, sijui vikoba. Ana madeni kila kona. Haachi fulsa yoyote ya hela mbele yake. Hata kama gari kanunua leo hii.

ghafla anapata mnunuzi wa bei nzuri kuliko aliyonunulia, honestly, anauza papohapo!
 
Punguza wivu na fitna zitakugharimu acha kufuatilia maisha ya watu.
 
Jamani inatosha naona ameelimika.
Hata hivyo yeye sio wa kwanza kuna watu walishasema mawaziri wanaweza kupanda farasi kwenda job.

Wengine sio lazima utumie sukari asali inatosha n.k kwao hawa jamaa wako sahihi sasa mtu wa aina hii akipata uongozi itakuwa balaa
 
Mishahara ya watumishi wa Umma nimikubwa kiasi gani? Unatembelea ofisini kwa mtu unamiuta anasimu tatu smartphone zenye thamani ya si chini ya milioni mbili kila moja, unajiuliza haya mafedha wanayatoa wapi?

Je, huu ni utajiri au nikukosa elimu ya matumizi za fedha? Inaweza kuwa tunashangaa V8 za wakurugenzi kumbe tatizo linaanzia huku chini ambapo badala yakufanya Mambo yanayogusa jamii wamejikita kwenye anasa zisizofaa.

Kama mtu anamiliki simu za milioni nane hadi kumi unategemea huyu ukimpa madaraka makubwa atawajali wananchi wachini au atazidi kujilimbikizia Mali?

Hawa wenye masimu kibao ukiwafuatilia huko walipotoka wapo ndugu zao hawana ada na kwa wao kushindwa kugawanya vipato vyao wamepelejea nchi kuendelea kuwa na tatizo kubwa la umaskini.

Yamkini angeacha kununua simu hizi zisizo na kazi angewekeza kwenye biashara na angeajiri watu kadhaa tatizo la ajira lingepungua.

Hapa najadili simu ila vipo vingi vyakujadili ambavyo tusipovikemea tunatengeneza taifa la walafi wakati nchi yetu umezaliwa kwenye ujamaa.
Tuonyeshe huyo mfanyakazi wa serikali na hizo simu zake tuzitafakari, tutakupa jibu. Usiwe kama Trump, tunataka ushahidi hapa.
 
Tuwekee hapa hizo simu za milioni nane hadi kumi na tupe mifano ya hao watumishi na vyeo vyao wanaomiliki hizi simu ili tuweze kufanya comparison, maana haya mambo ya kuweka kila kitu kwenye kapu moja yanatuchanganya.
 
Mishahara ya watumishi wa Umma nimikubwa kiasi gani? Unatembelea ofisini kwa mtu unamiuta anasimu tatu smartphone zenye thamani ya si chini ya milioni mbili kila moja, unajiuliza haya mafedha wanayatoa wapi?

Je, huu ni utajiri au nikukosa elimu ya matumizi za fedha? Inaweza kuwa tunashangaa V8 za wakurugenzi kumbe tatizo linaanzia huku chini ambapo badala yakufanya Mambo yanayogusa jamii wamejikita kwenye anasa zisizofaa.

Kama mtu anamiliki simu za milioni nane hadi kumi unategemea huyu ukimpa madaraka makubwa atawajali wananchi wachini au atazidi kujilimbikizia Mali?

Hawa wenye masimu kibao ukiwafuatilia huko walipotoka wapo ndugu zao hawana ada na kwa wao kushindwa kugawanya vipato vyao wamepelejea nchi kuendelea kuwa na tatizo kubwa la umaskini.

Yamkini angeacha kununua simu hizi zisizo na kazi angewekeza kwenye biashara na angeajiri watu kadhaa tatizo la ajira lingepungua.

Hapa najadili simu ila vipo vingi vyakujadili ambavyo tusipovikemea tunatengeneza taifa la walafi wakati nchi yetu umezaliwa kwenye ujamaa.
Watu wasifanya biashara?
Kumbuka wewe kama ni masikini sio lazima kila mtu awe maskini
 
Back
Top Bottom