Ni sahihi wabunge wa Zanzibar kukaa Bungeni wakati hoja za Wizara zisizo za Muungano zikijadiliwa?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Je, ni sahihi wabunge wa Zanzibar kukaa Bungeni wakati hoja za wizara zisizo za muungano zikijadiliwa kwenye bajeti nk

Na je Ni sahihi wao kuwemo kamati za bunge za mambo yasiyo ya muungano?

Wanatakiwa wahudhurie vikao tu vinavyohusu Mambo ya muungano tu sio yote. Yanayotuhusu watanganyika wasihudhudhurie warudi kwao Zanzibar sababu Sisi bara huwa hatuendi kuhudhuria vikao vya Baraza la wawakilishi na kuwemo kamati zao za Baraza la wawakilishi hii Ni kero ya Muungano.
 
Kwenye Bunge la katiba upinzani walipopolewa matusi kwa hii hoja.
Sio swala Wala la katiba mpya hi iliyopo inatosha wabunge wa Zanzibar wanakaaje Bungeni wakati hoja za wizara zisizo za muungano zikijadiliwa?

Huku Ni kuvunja katiba wanatakiwa wakae kujadili za muungano tu zikiisha wapande meli ya Azam warudi kwao Zanzibar napendekeza wizara za muungano ndio ziwe zinaanza kijadiliwa zikiisha wapande boti warudi kwao Zanzibar
 
Tanzania bara au Tanganyika huwa hatuhudhuri vikao vya Baraza la wawakilishi na Wala huwa hatuko kamati zao za Baraza lao kwa Nini wao wawepo kamati za bunge za wizara zisizo za muungano na wahudhurie vikao vya bunge vya wizara zisizo za muungano?
 
Katiba iliyopo ndiyo inaelekeza uwepo wao maana hatuna Bunge la Tanganyika Ndugu yangu.
 
Sio swala Wala la katiba mpya hi iliyopo inatosha wabunge wa Zanzibar wanakaaje Bungeni wakati hoja za wizara zisizo za muungano zikijadiliwa?

Huku Ni kuvunja katiba wanatakiwa wakae kujadili za muungano tu zikiisha wapande meli ya Azam warudi kwao Zanzibar napendekeza wizara za muungano ndio ziwe zinaanza kijadiliwa zikiisha wapande boti warudi kwao Zanzibar
Toka lini katiba ikaheshimiwa?

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania bara au Tanganyika huwa hatuhudhuri vikao vya Baraza la wawakilishi na Wala huwa hatuko kamati zao za Baraza lao kwa Nini wao wawepo kamati za bunge za wizara zisizo za muungano na wahudhurie vikao vya bunge vya wizara zisizo za muungano?
Bunge la Tanganyika liko wapi? Mkuu ndiyo maana nimesema kwanza Katiba itakayo tambua uwepo wa Tanganyika kama Jamuhuri huru na Zanzibar kama Jamuhuri huru.

Kisha sasa tuje na mfumo wa Muungano ambao utatoa nafasi kwa nchi zote mbili kila moja kujadili mambo yake yasiyo ya Muungano katika Bunge lao. Yale ya Muungano yatajadiliwa katika Bunge la Muungano kwa kuwa na utaratibu wa wabunge kutoka pande zote.

Kwa katiba hii ya sasa huwezi kupata hicho unachotaka.
 
Naona akili imeanza kukurudia but jua kabisa tatizo ni katiba
Katiba iliyopo haijawahi tamka kuwa wabaki mjadala wa wizara zisizo za Muungano

Wanzanzibari hujifanya wapiga Kelele sanaa na kuchonga mdomo Sana mambo ya muungano Sasa zamu yetu .Ewe mtanganyika wake up .Ongea bila woga usiachie tu wazanzibari wachonge mdomo wajue kuwa usimwamshe aliyelala akiamka utalala wewe
 
Je ni sahihi wabunge wa Zanzibar kukaa bungeni wakati hoja za wizara zisizo za muungano zikijadiliwa kwenye bajeti nk

Na je Ni sahihi wao kuwemo kamati za bunge za mambo yasiyo ya muungano?

Wanatakiwa wahudhurie vikao tu vinavyohusu Mambo ya muungano tu sio yote.Yanayotuhusu watanganyika wasihudhudhurie warudi kwao Zanzibar sababu Sisi bara huwa hatuendi kuhudhuria vikao vya Baraza la wawakilishi na kuwemo kamati zao za Baraza la wawakilishi hi Ni kero ya muungano
Mkuu YEHODAYA , wabunge wote ni sawa kabisa ndani ya Bunge, na wana hadhi sawa!. Mbunge baada ya kuapishwa, haijalishi aliingiaje Bungeni, kwa kuchaguliwa, kuteuliwa au viti maalum, au ni Mbunge wa chama tawala au upinzani, ni Mbunge wa Zanzibar, mule ndani ni kitu kimoja, hivyo wako huru kuchaguliwa mawaziri wizara yoyote, au Kamati zozote.

Wazanzibari ni Wazanzibari at the same time pia ni Watanzania, wana haki zote za Mtanzania, ikiwemo kuteuliwa kuwa mawaziri wa wizara zisizo za muungano.
P
 
Mbunge yoyote, au wabunge wote ni sawa kabisa ndani ya Bunge, na wana hadhi sawa!. Mbunge baada ya kuapishwa, haijalishi aliingiaje Bungeni, kwa kuchaguliwa, kuteuliwa au viti maalum, au ni Mbunge wa chama tawala au upinzani, ni Mbunge wa Zanzibarn
Naomba ukae mbali na huu mjadala uko zaidi ya uwezo wako ulishaona wabunge wa Zanzibar wakiteuliwa uwaziri wizara zisizo za muungano?

Pascal hiyo digrii yako ya sheria inabidi chuo kilichokutunuku wakunyanganye huitendei Haki hufai kuwa Alumni wa chuo ulichohitimu
 
Pascal Mayalla sikuizi hana tofauti na mbumbumbu ambaye hajaenda shule anatetea upumbavu sijui amekumbwa na madhila gani
Binadamu ndie Commander in Chief wa ubongo wake akiamrisha ulale utalala akiamrisha uamke utaamka Pascal kauamurisha Ulale na umelala kweli unakoroma hasa beyond kukoroma
 
Naomba ukae mbali na huu mjadala uko zaidi ya uwezo wako ulishaona wabunge wa Zanzibar wakiteuliwa uwaziri wizara zisizo za muungano?

Padcal hiyo digrii yako ya sheria inabidi chuo kilichokutunuku wakunyanganye huitendei Haki hufai kuwa Alumni wa chuo ulichohitimu
Prof. Mbarawa alikuwa wizara ya Mawasiliano na sio ya Muungano!. Humu jf tuna mijitu mijinga ajabu!. Kila Mzanzibari ana haki zote za Mtanzania!. Acha ujinga!.
P
 
Prof. Mbarawa alikuwa wizara ya Mawasiliano na sio ya Muungano!. Humu jf tuna mijitu mijinga ajabu!. Kila Mzanzibari ana haki zote za Mtanzania!. Acha ujinga!.
P
Katiba ilivunjwa for the first time na ndio maana alipata shida kuwa mgombea Uraisi Zanzibar . wazanzibari wakasema huyu mbara huyu angekuwa mzanzibari asingepewa wizara isiyo ya muungano wakasema Magufuli anataka kutuletea mtu wa bara hatutaki Ilimgharimu Sana tu.Wanzanzibari walihoji uzanzibari wake kuwa siyo!!! Kuwa Kama Ni mzanzibari ilikuwaje akapewa wizara isiyo ya muungano? Wakampiga chini!!!

Pascal hoja huna
 
Raisi Samia uvunje Muungano ili kila mtu apambane kivyake vyake,hizi chokoa chokoa zinaweza kusababisha utindio wa ubongo kwa wabongo wa ccm maana akili zao zipo kigwajimagwajima.
 
Back
Top Bottom