chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Kumekuwa na utaratibu wa vyombo vya habari kutoa taarifa rais akienda kanisani na alichoongea kanisani, mfano juzi alienda kusali Singida misa ya Krismasi
Mi nadhani Rais kwenda kanisani ni jambo la kiimani na binafsi sana, na mambo atakayosema huko kuhusiana na imani yake hayatakiwi kuchukuliwa kama ya kitaifa
Na ukizingatia nchi yetu ina watu wenye imani tofauti na wana hisia na imani zao sio bora mambo ya imani ya dini ya Rais yakachanganywa na kazi yake kama Rais
Nimeandika haya baada ya kuibuka utata Rais aliposema Rozari ndio ilimsaidia kushinda urais, kauli hii nadhani aliimaanisha kwa wakatoliki wenzake kama mkatoliki na sio kwa umma wa watanzania ila kwa sababu ya kuripoti masuala binafsi kuwa ya kitaifa utata ukaibuka
Pia kwenye account ya YouTube ya Ikulu wameweka video ya misa hiyo, hii nadhani pia haijakaa sawa sababu inafanya Tanzania kuonekana kama taifa la kikristo ili hali sivyo
Na hapa sizungumzii hii ya krismas tu, zipo nyingi