Mwanamke kumtongoza mwanaume na tamaduni za Kiafrika

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
552
Hey wana JF,

Katika utamaduni wetu kama waafrika/ watanzania, mwanaume ndio wa kwanza siku zote kueleza hisia zake kwa binti kama anamuhitaji kimahusiano. Hivi sasa imekuwa tofauti kidogo, kuna baadhi ya wasichana wanaanza kueleza hisia zao kwa mvulana/Mwanaume kama anampenda au anahisia nae kimapenzi.

Lakini hapa nchini kwetu inaonekana kama vile msichana anayemtaka kimapenzi mwanaume ni muhuni/ mapepe/malaya, majina yote hayo anapewa. Hii tabia ya msichana kumtongoza mwanaume hapa Tanzania kwa sasa bado watu wanaona kama msichana mwenye tabia hiyo ni muhuni au malaya, imekuwa tofauti na developed country hao hii tabia ni ya kawaida tu na wal si ajabu.

Je wewe kama mwanaJF na Mtanzania unalionaje hili, je ni sawa kwa msichana kumtongoza mwanaume? Au bado tubaki na mila/utamaduni wetu wa mwanaume kumtongoza mwanamke?
 
Ni jambo jema mtu kueleza hisia zake kwa yule anayemfeel, hivyo Kisura jisikie huru kuweka hisia zako bayana kama kuna Mkaka amekuvutia..

Hii kasumba ya kuonekana malaya itategemea na kiwango cha uelewa alicho nacho mwanaume husika au njia anayotumia mwanamke kuwasilisha hisia zake. Kwa mfano kama mwanamke anampenda mwanaume, huonesha dalili za kujirahisisha kwake ili kumweka aware jamaa na matokeo yake ndiyo hayo ya kuonekana malaya.

Hivyo Mamaa piga moyo konde, jipe ujasiri na mfuate jamaa na mweleze bayana hisia zako juu yake au mtumie mtu ambaye ataweza kukuwasilishia hisia zako bila ya pande yoyote kuathirika, i mean either rafiki yake wa karibu au rafiki yako wa karibu..

Ila sipati picha jamaa akilitolea nje ombi lako, manake sisi wanaume tumeshazoea kupigwa vibuti hivyo huwa tunachukulia powa tu, wewe utaweza kukivumilia lakini?

All the best.
 
Hii ni maada/mjadala tu, haimanishi hivyo kama ulivyofikiri.
 
Pretty,

Huo utamaduni au mazoea siyo Tanzania tu. Sehemu nyingi (at least nilizotembelea mimi) mwanaume ndiyo huwa ana tegemewa kumapproach mwanamke. Mimi sioni ubaya yoyote mwanamke kumtongoza mwanaume. Kumkosa mwanaume umpendae kisa unangoja akutongoze mimi naona ni ujinga.

Nadhani tatizo ni kwamba wanawake wengi wanaona wakitongoza mwanaume wataonekana malaya au kuonekana kuwa wana shida sana na kuwa na mwanaume. Kwangu mimi iswezi kumfikiria tofauti mwanamke yoyote anayemtongoza mwanaume.

I think it is time mindset kama hizi zichange.
 
Last edited by a moderator:
Ni jambo jema mtu kueleza hisia zake kwa yule anayemfeel, hivyo Kisura jisikie huru kuweka hisia zako bayana kama kuna Mkaka amekuvutia..

Hii kasumba ya kuonekana malaya itategemea na kiwango cha uelewa alicho nacho mwanaume husika au njia anayotumia mwanamke kuwasilisha hisia zake. Kwa mfano kama mwanamke anampenda mwanaume, huonesha dalili za kujirahisisha kwake ili kumweka aware jamaa na matokeo yake ndiyo hayo ya kuonekana malaya.

Hivyo Mamaa piga moyo konde, jipe ujasiri na mfuate jamaa na mweleze bayana hisia zako juu yake au mtumie mtu ambaye ataweza kukuwasilishia hisia zako bila ya pande yoyote kuathirika, i mean either rafiki yake wa karibu au rafiki yako wa karibu..

Ila sipati picha jamaa akilitolea nje ombi lako, manake sisi wanaume tumeshazoea kupigwa vibuti hivyo huwa tunachukulia powa tu, wewe utaweza kukivumilia lakini?

All the best.

Nimeshapata ujumbe...mambo yote mswano
 
Pretty tuko 2009 na na siyo mwaka 47. Kwanini uendelee kuteseka roho kila siku iendayo kwa Mungu kutokana na kumpenda mwanaume ambaye ungependa kuwa naye kwa uhusiano wa karibu?

Rusha tu ndoano yako anaweza kabisa kunasa ha ha ha ha lakini wanaume wengi hupenda kujua kama una kawaida ya kuwapigia speed wanaume mara kwa mara na wengi watakuwa na wasi wasi kwamba unaweza kuona njemba nyingine ikakuacha hoi na wewe kwa mara nyingine tena ukairushia ndoano.

Kwa maoni yangu sioni kama ni tatizo lolote. Maana hata hapa JF tumeshaona wanawake wakitangaza kutafuta wachumba kitu ambacho miaka ya nyuma kilikuwa hakipo kabisa katika mila zetu za Kitanzania.
 
Last edited by a moderator:
Pretty tuko 2009 na na siyo mwaka 47. Kwanini uendelee kuteseka roho kila siku iendayo kwa mungu kutokana na kumpenda mwanaume ambaye ungependa kuwa naye kwa uhusiano wa karibu? Rusha tu ndoano yako anaweza kabisa kunasa ha ha ha ha lakini wanaume wengi hupenda kujua kama una kawaida ya kuwapigia speed wanaume mara kwa mara na wengi watakuwa na wasi wasi kwamba unaweza kuona njemba nyingine ikakuacha hoi na wewe kwa mara nyingine tena ukairushia ndoano.

Kwa maoni yangu hakuna sioni kama ni tatizo lolote. Maana hata hapa JF tumeshaona wanawake wakitangaza kutafuta wachumba kitu ambacho miaka ya nyuma kilikuwa hakipo kabisa katika mila zetu za Kitanzania.

Hebu mwacheni Pretty bana...nshaongea naye miye...
 
Jamani hii mada tu nimeeileta hapa jamvini, sijamaanisha kwamba mie nataka kuaproach mwanaume.
 
Siku za kisasa inawezekana....mdada anatafuta number yako ana kutafuta...bila wewe kujua...anakupa detail zake na zako anakuwa anazifahamu vyema.Humjui yeye anakujua kwa kuwa ndio mwenye nia....anakutumia sms,anapiga,credit anatuma yaani kama men akiwa kwenye mawindo.

Once anakutoa out....japo huwa tunajikakamua kwa kulipa bill kwa kuwa hatutaki kuonekana boya.So ya women out there see men follow him.Nimeuliza couple of women wanasema njia ingine badala ya kumtongoza mwanaume huwa wanajilengesha ili wapate antension yake na kutongozwa...basi hukubali.Hii ni kwa sababu kuwa utamaduni haujatulea kutongozwa na wadada.
 
Matokeo yake ndo yale mambo ya kumegwa na kuachwa kisha kuoneana kicheche.. Mi naona bora wawe wawazi tungu mwanzoni ili jamaa mapema kabisa ajue kuwa lengo nini haswa. Kwa sababu kwa hulka yetu wanaume, mwanamke akijilengesha hata kama huna feelings naye utammega tu kumbe mwenzako yeye ana ndoto za kuwa na wewe forever ila hakuziweka bayana tangu mwanzoni.

Hiyo ndiyo huwa inapelekea wanawake kutuona wanaume kama wakatili, hatujali hisia zao pale wanapoonesha kutupenda, lakini ukweli ni kuwa njia wanayokuwa wametumia kumtokea mtu ndiyo jamaa naye anaitumia kama advantage ya kummega. Sidhani kama demu ambaye simfeel akija siriaz kunambia kuwa anataka anipe moyo wake nitakubali kumchezea ilhali najua anachokifeel. Nitamwambia tu ukweli ili asipoteze muda wake kwangu. Ila kama atakuwa anajirahisisha tu bila kuweka bayana lengo, nammega kisha nasepa..
 
Vijana wanaoanza uhusiano kwa mara ya kwanza tu huwa wanaongelea ndoa kweli? yaani kuishi pamoja forever kama ulivyosema? Mmh, siamini! Mi ninachoamini ni kuwa - wengi -wanaanza taratibu kama marafiki na baadaye uhusiano unapochanganya ndipo wanapoanza kuzungumzia mambo mazito ya kuishi pamoja forever, au?
 
Pretty, hata kwa kuitoa mada kwa njia moja au nyingine umeshajieleza! uzuri kaka Nyani amekuelewa na ujumbe umefika...wadau sisi tubariki bwana! na mwenye wivu ajitoe koromeo!
 
Back
Top Bottom