Ni sahihi mke kukaribisha ndugu zake nyumbani bila kushirikisha mume?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,809
15,059
Habari jf.
Kuna kesi moja hapa nimeshindwa kuisolve,jamaa angu analalamika kuwa mkewe ana tabia ya kukaribisha ndugU zake nyumbani bila kumshirikisha.

Anasema hapo kwake saiv kuna ndugu wa mke kama watatu ambao wapo tu wamekaa bila kazi yoyote.

Kilichomuuma zaid ni leo kuna katoto ka dada wa mke wake kameletwa eti kaje kusomea hapo kwao,jamaa hakutaarifiwa huo ugeni anashangaa tu mkewe anamuambia huyo dogo atakuwa hapo.

Tatizo la jamaa angu anaogopa kuhoji asije akaonekana mchoyo.

So wakuu case kama hii mnaweza kushauru nini?

Note:wote mume na mke ni waajiriwa, so suala la pesa ya chakula sio tatizo.
 
Haya mambo yapo nchi za mbali lakini kwa malezi yetu ni tofauti na yatanishangaza kama ntarudi nyumbani KWANGU na kukuta wageni aliowaalika bila kuniomba ruhusa
Huyu itakuwa kazaliwa Argentina au Mexico

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mkuu si useme ni wewe kwani kuna shida gani.
Habari jf.
Kuna kesi moja hapa nimeshindwa kuisolve,jamaa angu analalamika kuwa mkewe ana tabia ya kukaribisha ndugU zake nyumbani bila kumshirikisha.

Anasema hapo kwake saiv kuna ndugu wa mke kama watatu ambao wapo tu wamekaa bila kazi yoyote.

Kilichomuuma zaid ni leo kuna katoto ka dada wa mke wake kameletwa eti kaje kusomea hapo kwao,jamaa hakutaarifiwa huo ugeni anashangaa tu mkewe anamuambia huyo dogo atakuwa hapo.

Tatizo la jamaa angu anaogopa kuhoji asije akaonekana mchoyo.

So wakuu case kama hii mnaweza kushauru nini?

Note:wote mume na mke ni waajiriwa, so suala la pesa ya chakula sio tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom