Ni sahihi maji ya mvua kutumika kunywa?

Kijijini watu tunakinga kwenye nyumba za nyasi, unakuta yapo kama chai ya rangi,basi una aweka pembeni yana jitenga uchafu wote unatuwa chini ya ndoo,ukiyanywa ni mepesi mdomoni,tatizo yanakuwa na viluilui haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ninachojua hayana chumvi wala magadi ni maji ambayo hayajagusa laana ya ardhi ukinywa ni burudani kabsaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
ardhi ina laana gani zinazoweza kufanya maji yasiwe mazuri kwa matumizi?

kijiografia: maji ya mvua yanatokea wapi na kabla ya kufika kwetu yanapitia nini na nini huko hewani? hapo ukiacha hizi bati na gata tunazo tumia kukusanya maji ya mvua!
 
Kwa kifupi maji ya mvua kutumika tumboni si salama kiafya labda kama kuna uwezekano wa kuyafanyia namna kitaalamu yakidhi vigezo. Ukiachilia mbali mapungufu yaliokwisha tajwa na baadhi ya wanauzi, hali ya anga na maezekeo huchangia kwa kiasi kikubwa kuathiri usalama wa maji ya mvua. Miji iliyokithiri kwa uchafuzi wa mazingira, kuna wakati mvua ikinyesha maji yanakuwa machavu kabisa. Maezekeo pia huathiri maji haya, mfano, baadhi ya materials kama asbestos huwa ina kemikali zinazoweza kuathiri maji yako yanapotiririka juu yake.
 
ardhi ina laana gani zinazoweza kufanya maji yasiwe mazuri kwa matumizi?

kijiografia: maji ya mvua yanatokea wapi na kabla ya kufika kwetu yanapitia nini na nini huko hewani? hapo ukiacha hizi bati na gata tunazo tumia kukusanyi maji ya mvua!

Mimi nilimuelewa kwa mtazamo usio wa kisayansi. Wengi wetu tunaongozwa na ladha zaidi katika vyakula kuliko virutubisho ama usalama wake. Ninakumbuka sisi tuliokulia vijijini,baadhi ya maeneo maji ni shida sana. Yale mnayopata ya visimani si ajabu yakawa na chumvi sana ama machafu sana. Hivyo, maji ya mvuo yalikuwa ni mkombozi. Hapo usitushangae tukisema mvua ni pepo au baraka na yale ya ardhini/ardhi ni laana.

Kumbuka hapo si kisayansi, ukianza kuchambua utakuta hayo ya mvua pia yametoka ardhini, kwa maana ya ule mzunguko.
 
Aisee kwa maeneo yeye pollution kama dar sio salama kabisa kunywa maji ya mvua..kwanza yanakuwa na carbonic acid bado vumbi na uchafu mwingine mwingi..
 
Mimi nilimuelewa kwa mtazamo usio wa kisayansi. Wengi wetu tunaongozwa na ladha zaidi katika vyakula kuliko virutubisho ama usalama wake. Ninakumbuka sisi tuliokulia vijijini,baadhi ya maeneo maji ni shida sana. Yale mnayopata ya visimani si ajabu yakawa na chumvi sana ama machafu sana. Hivyo, maji ya mvuo yalikuwa ni mkombozi. Hapo usitushangae tukisema mvua ni pepo au baraka na yale ya ardhini/ardhi ni laana.

Kumbuka hapo si kisayansi, ukianza kuchambua utakuta hayo ya mvua pia yametoka ardhini, kwa maana ya ule mzunguko.
Evapolation
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom