Bailly5
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 16,402
- 35,083
Habari wana MMU, natumaini mko poa kabisa.
Kuna swala kidogo naomba tujadili. Ni hivi kwenye mahusiano kuna changamoto nyingi ila uvumilivu na upendo ndo inatufanya tuendelee kuwa pamoja.
Swala ni hili je ni sahihi kumwambia mwenza wako udhaifu wake au usimwambie? Najua Kila mtu ana udhaifu wake. Mfano una mpenzi na udhaifu wake unajua kabisa labda ni mchafu katika sekta Fulani. Je utamwambia au utamrekebisha kimya kimya?
Maana Kila mtu yuko tofauti katika mapokeo ya kitu fulani anachoambiwa na mwingine. Maana hapa kuna udhaifu wa kimwili na udhaifu wa kitabia. Hii kimwili kidogo ni ngumu ila kuna vingine vinarekebishika hali kadhalika kitabia huku ndo mazito zaidi.
Je ni sahihi kwa wenza kuambiana madhaifu yao au warekebishane kimya kimya?
Nawasalisha