Ni sahihi kwa mtumishi wa bwana/mlokole kutusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sahihi kwa mtumishi wa bwana/mlokole kutusi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LadyGaga, Mar 23, 2010.

 1. L

  LadyGaga New Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jamani nina swali, Hivi na sahihi kweli kwa mtumishi wa Bwana ama mlokole kuwa anatukana hovyo kwa kudhamiria tena majitusi makubwa kama vile m***** we, mbwa na kusema maneno kama natamani ufe?,
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  si sahihi kabisa si kwa watumishi atakwa yeyeto aliyeokoka ata ambaye ajaokoka
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  si sahihi hata kidogo ingawa na yeye ni Binadamu lakini kila kitu kina mipaka
   
 4. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  jibu rahisi ni kuwa hakuna aliye sahihi atukanapo hata kama hajaokoka
   
 5. L

  LadyGaga New Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nawashukuru wote kwa michango yenu, nilikuwa nalielewa hilo sema nimeshangaa sana, kwani huyu mtu alianza kutoa matusi hayo baada tu ya kutoka kwenye ibada tena nje ya kanisa moja kubwa sana hapa jijini, na kwe status yake sema ana tabia hiyo sana. ikabidi niwaulize na wengine nijue mnaonaje hili.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ni kwamba hana hekima tangu mwanzo huyo!
  Kutukana ni tabia mbaya ya mtu, na wala haifutiki saaana kwa mtu kuokoka!, inahitaji Neema ya Mungu!
  Ungemwambia LIVE broda, ungekuwa umemsaidia sana raia huyo!
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Hata yule anayejiita mzee wa upako(sijui wa uji au tope)alitoa maneno machafu kwenye press conference yake ya karibuni...
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sio sahihi kabisa.kwani vipi? imetokea nini?
   
 9. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kutoa matusi au kutumia lugha ya matusi hadharani au mafichoni sio sahihi na ni kosa kwa yeyote awe ni mtumishi wa bwana/mlokole au awe ni mpagani
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Utawajua kwa matendo yao......................
  Galatia 5: 16-22

  16 Basi, nasema hivi: mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia.

  17 Maana, tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamwezi kufanya yale mnayotaka ninyi wenyewe.

  18 Kama mkiongozwa na Roho, basi, hamko tena chini ya Sheria.

  19 Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati, ufisadi;

  20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano;

  21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo. Nawaambieni tena kama nilivyokwisha sema: watu wanaotenda mambo hayo hawatakuwa na nafasi yao katika ufalme wa Mungu.

  22 Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,
  23 upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.
   
 11. nzalendo

  nzalendo JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,875
  Likes Received: 2,681
  Trophy Points: 280
  Yeye pia ni mwanadamu hukosea lakini hatuna haki ya kumhukumu.
  So kinachotakiwa ni staha
   
 12. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Amekosea.. ALIYEOKOKA au HAJAOKOKA hatutakiwi kutukana.. Hata kisheria ni kosa..
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mmh !
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  watu wengi wameokoka ila awajafunguliwa ila aipendezi kabisa nimewai kushuudia live mtumishi akiwatukana watu wa vyombo kanisani kisa vyombo vilisumbua alitoka mbele akaenda studio akaanza kuporomosha matusi namaanisha matusi kweli kweli atakuyataja hapa siwezi vidole vitasikia ukakasi kilichotokea wakati anaendelea ghafula mitambo ikarudi hewani na yy bado anaporomosha matusi yakaenda hewani kabla awajawai kuzima ilikuwa soo
   
 15. L

  LadyGaga New Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kuna mtu kauliza imekuwaje, ngoja nimwagie mchapo. Habari za kusadikika ni kwamba huyu mama mtu mzima ambaye ni mtumishi wa bwana, amekwazika na issue ni kwamba, ana mwanae ambaye amekatiliwa na mchumba ambaye alizaa nae, kisa ni kwamba huyo mchumba(alyekuwa awe mkwewe) amerudiana na mpenzi wake wa zamani na wote wanalifahaumu hilo.Sasa huyo mama amekuwa na jazba anatukana hovyo tu, tena matusi makubwa mpaka amefikia kusema maneno ya uongo ili huyo mkewe aachane na mpenzi wake. Sasa cha kushangaza ni kwamba kwanini aruhusu hiyo hali imtolee kuuona uzima wa milele?, ni kituko hapa mtaani kwetu.
   
 16. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  si sahihi kwa mtu yeyote hata kama si mlokole!kwa mlokole ni mbaya zaidi maana anawachafua wenzie wenye imani hiyo!
   
 17. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe ndo umetukanwa au vipi, mbona unawajadili watumishi wa bwana tu, kwani kwa mtu yeyote yule ni sahihi kutukana? so why should the definition be only to watumishi wa Bwana? kwa kifupi, sisi sote si malaika, huwa tunakosea wakati mmoja au mwingine, so are the watumishi wa Mungu,na bado tu ni watumishi wa Mungu. inategemeana, siwezi kumjaji mtumishi yeyote hapa, ila kinachotakiwa kujadiliwa ni JE NI SAHIHI MTU YEYOTE KUTUKANA? SI WATUMISHI TU, WATU WOTE, labda kama una interest au bifu na watumishi hao, au labda wewe ndo ulitukanwa. angalia unaweza kuwa unatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio kumbe kwako kuna boriti/ubao mzima na wewe hauuoni, kwa kwanza anayejiona ni msafi na awe wa wakwanza kurusha jiwe.
   
 18. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Halafu wa watumishi wa Mungu huwa wana matusi makali utadhani wameyasomea na kupata digrii ya uzamili. Haifai kwa kweli.
   
 19. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hii ni vita dhidi ya watumishi wa mungu au?
   
 20. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kumcha Bwana Mungu ni chanzo cha maarifa, Mithali 1 : 7.
  Ni rahisi mtu kujiita ameokoka, lakini roho na tabia zake zisiokoke,
  Kila alitajaye jina la BWANA na aache kutenda uovu.
  Na limtokalo mtu kinywani mwake ndilo lililoujaza moyo wake.
   
Loading...