Ni sahihi kwa msafara wa viongozi wa vyama vya siasa kusindikizwa na king'ora cha polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sahihi kwa msafara wa viongozi wa vyama vya siasa kusindikizwa na king'ora cha polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CPA, Apr 17, 2011.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Jana nikiwa ubungo mataa trafic alizuia magari, kisa msafara viongozi wapya wa ccm wanapita huku wakisindikizwa na pikipiki ya polisi huku ikipiga king'ora ikifuatiwa na Landcruiser V8 Kama 6 (new model toleo la 2008) nyeupe, kila moja likipeperusha bendera ya ccm, yakiwa limewabeba, nape, makamba, msekwa, mukama. Wakiwa wanatoke kibaha wanaelekea manzese. Je ni sahihi kwa msafara wa viongozi wa vyama vya kisiasa ambao sio viongozi wa serikali, kusindikizwa na polisi huku wakipigawa ving'ora na huku raia tukiwa tumepigwa folen mpaka msafara upite? Ni nani anayewalipa posho hao polisi na kwasabu ipi?
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Kwa kupewa pikipiki ni maombi tu kwa jeshi polisi kwa chama cha siasa maana wana haki kupata ulinzi na hata kupata msafara wa sweeper moja kwa hilo halina shida sana ingawa najua CDM wana haki kama hiyo kuomba ila watasumbuliwa sana kupewa....labda nao wakiwa madarakani
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  CCM ndio serikali yenyewe, wewe unasema hayo tu wakati wa kampeni??? Ndio maana katiba mpya inahitajika ASAP kupiga stop haya maovu yote yanayoendelea.
   
 4. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Ok kama wanahaki kisheria haina tatizo. Asante kwa kunielewesha
   
 5. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli hata mie niliona ule msafara itv ukitokea morogoro, nilijiuliza swali hilihili; maana sijawai kuona cdm wakisindikizwa vile!! Ila hivi vyote vinapokea ruzuku zetu,iweje ccm pekee ndio ipewe msafara wa polisi vile??

  Je jeshi la polisi nayo ni taasisi ya kampeni za ccm?? Naona wanaendelea kudhihirisha tokea maandamano ya arusha,ila wajue nao siku zao zinahesabika; wajifunze kutenda haki mapema hii. Kwakweli katiba mpya inahitajika leo hii
   
 6. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hawana haki kisheria,ila wanajichukulia sheria mkononi. Ndo maana inakuwa vigumu kutenganisha mambo ya ccm na vyombo vya dola, na hili ni ukiukwaji wa sheria za nchi. Sheria za zuio zipo, ila zi hafifu, na hakuna utashi wa kutekelezwa kwa sheria hizo.
   
 7. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sehemu kubwa ya viongozi kutoka wizara na taasisi za serikali huchaguliwa toka chama tawala ndiyo maana lazima wawe mstari wa mbele na kukifever chama tawala na asilimia kubwa ni wanaccm.
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Kisheria ni haki ya kila penye mkusanyiko wenye kubeba itikadi yoyote ile kuhita ulinzi na taratibu zipo za kupata ulinzi huo! Tatizo la tz nikuwa vyombo vya usalama vimeshinikizwa kuingia ktk siasa, vimekuwa sehemu ya makampeni meneja wa chama cha mafisadi (ccm)
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  siku zao zina hesabika wala msijali wapambanaji na ukizingatia waliowekwa saizi ndio vilaza zaidi hata ya makamba
   
 10. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Niliumia sana jana, nimekaa kwenye folen napigwa nakujua, nikujua mkuu wa nchi anapita, kumbe ni msafara wa gamba jipya! Kweli nimeamin wanasiasa ni wabinafsi.
   
 11. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  hii ni utumiaji mbaya wa madaraka, haitofautiani sana na misafara inayomsindikiza mke wa rais. ni ufujaji wa mali ya umma pasipo ridhaa wa wavuja jasho. mwisho wa yote ni kupata ikatiba mpya itakayo weka bayana uchafuzi wa aina hii.:director:
   
 12. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Sio sahihi, kwani wao ni viongozi wa chama na sio serikali.
   
 13. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,978
  Likes Received: 20,359
  Trophy Points: 280
  Ninakuelewa unaposema ni utumiaje mbaya wa madaraka lakini ukiomba upate escort ya polisi inaruhusiwa kabisa na wala si tatizo sema mapungufu yaliyopo ndani ya jeshi letu hasa linapokuja suala la siasa, ccm hupendelewa zaidi ya vingine na hii ni kwa sababu hiki ni chama dola lakini haiwazuii cdm au cuf kuomba polisi wafagie njia wakiwa na msafara mkubwa kama ilivyokuwa kwa ccm jana pale viwanja vya bakhresa-manzese.
  Kilichonishangaza jana, magari makubwa makubwa V8 na hapa tunadai tumejivua gamba!!!:yawn:
   
 14. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 812
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Uliuliza na umeeleweshwa. Labda uyapinge majibu ya Skills ili kuongea hivi vinginevyo utakuwa ni mlalamishi, mkuu...
   
 15. J

  Joshua Bukuru Member

  #15
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Hii si sahihi hata kidogo. Ni ile dhana kuwa nchi yetu haiwezi kwenda mbele bila mabavu kutumika. Hakuna ndani ya katiba yetu na hata sheria za nchi zinasema kuwa misafara ya viongozi wa vyama vya siasa kusindikizwa na king'ora cha polisi. Ni udikteta unatumika tu. Na iwapo tumeamua kufanya hivyo, basi vyama vingine vya siasa navyo vifanyiwe kwa kigezo cha fair play. We should not base on one party and that is ruling party. Limetokea hilo na sasa nini kifanyike? Washtakiwe jeshi la polisi? au serikali kwa maana ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi?
   
 16. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  @bepari, nimelewa ila nilikuwa natoa machungu yangu ya kupigwa na jua kwenye fole kisa msafara wa viongozi wa vyama vya siasa, ambao wananesema wapo kwa ajili ya kutusaidia cc wananchi.
   
 17. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  wananchi tunayaona na kuyatafakari hayo ,hizo ni moja ya sababu za ccm kudondoka,yaani hawaoni tofauti kati ya chama na serikali ndio maana hata katiba wanataka kutunga wao wakati ni ya wananchi wote
   
Loading...