Ni sahihi kuwa na taasisi zisizo na misingi ya ujamaa na kujitegemea Tanzania?

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kijamaa inayotokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hii imeelezwa katika ibara ya 3 ya Katiba ambayo inasomekana kama ifuatavyo:

3.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Kwamba licha ya kwamba ni nchi ya kidemokrasia lakini ni ya kijamaa (Inaishi kwa misingi ya kanuni za kijamaa).
Maana ya Jamhuri ni kwamba Tanzania ni nchi au dola ambalo mamlaka makuu (supreme power) yanashikiliwa na watu (wananchi) sambamba na wawakilishi wao wa kuchaguliwa na wale walioteuliwa kwa mamlaka ya Rais (Rejea Ibara ya 36 ya Katiba) na kutekeleza mamlaka na madaraka hayo kwa niaba ya watu (Rejea Kaldellis, 2015) tofauti na Ufalme ambapo mamlaka hushikiliwa na mtu mmoja kwa niaba ya watu wote (Rejea Harris, 2005).

Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania neno Jamhuri linapatikana katika ibara ya 8 [1(a)] ambayo inasomeka kama ifuatavyo:

8 .-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) _Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;_

Kwa muktadha huu wa maelezo ya Katiba ni kwamba wananchi wa Tanzania wana kariba, tajiriba na wanaishi kwa falsafa za kijamaa (Rejea Kanuni za Azimio la Arusha, 1967).

Kwa hivyo basi utekelezaji wa mamlaka na madaraka ambayo yanatokana na wananchi ni yale yanayoshadihisha misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea na si kukinzana nayo. Ni kweli au si kweli?
Hili linathibitishwa na ibara ya 9 ya Katiba ambayo inasomeka kama ifuatavyo:

9. Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano.

Kwa kukazia hilo dira ya Taifa ya Maendeleo (Vision 2025) imesisitiza pia kuenenda na kanuni zilizomo kwenye Azimio la Arusha la mwaka 1967 ili kufikia ujenzi wa taifa la uchumi wa kipato cha kati mwaka 2025.

Changamoto iliyopo ni kwamba, kama Katiba inaelekeza kwamba chombo chochote kinachoundwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni sharti kifuate (kitekeleze) misingi ya siasa za ujamaa na kujitegemea.

Je hizi taasisi au vyombo mbalimbali vya kisiasa na kiraia ambavyo havina misingi au kanuni za kijamaa na kujitegemea havikinzani na Katiba ya nchi?
Je hakuna haja kwa vyombo hivi kulitazama hili kwa mapana?
Wasomi mtuelimishe.
 
Back
Top Bottom