Ni sahihi kusoma Economics katika mazingira haya?

Tingitane

Senior Member
Apr 18, 2012
116
130
Habari za leo wakuu,

Ni imani yangu kuwa mko wazima na mnaendelea na shughuli zenu za kila siku, niende kwenye mada nina kijana wangu wangu amemaliza HGE kidato cha sita na alikuwa anatamani sana kusoma ECONOMICS katika ngazi ya chuo.

Ombi langu kwenu ni kupata mawazo yenu kama ni sahihi kusoma uchumi na je ni chuo gani kwa sasa hapa Tanzania ambacho unashauri akasome kwa sasa.

Pia, nakaribisha mawazo mbadala na hayo aliokuwa nayo huyo kijana wangu.
 
Kama ni mtoto wa mkulima aachane na huo uchumi.

Kwa mtu wa hge nashauri akasome accountancy (akimaliza asome cpa kabisa) au land valuation (ipo ardhi).

Ila kama anajiweza kihesabu na kama alisoma phy olevo mwambie akasome building economics, gis, archtecture (kama bado wanapokea watu wa hge).
 
Kama ni mtoto wa mkulima aachane na huo uchumi.

Kwa mtu wa hge nashauri akasome accountancy.

Ila kama anajiweza kihesabu na kama alisoma phy olevo mwambie akasome building economics, gis, archtecture (kama bado wanapokea watu wa hge) au land valuation pale ardhi.
yes hata mimi nilitaka kumshauri hivyo aende pale ardhi kuna hizo kozi za land management,land valuation,building economics,facility management.

Kuna marafiki zangu wa HGE walisoma hizi kozi wanakula maisha. Uzuri wa hizi kozi hata asipoajiriwa ni rahisi kupiga dili nyinginyingi binafsi za mjini na zingine zinahusiana na real estate.
 
Ndio awe kasoma Physics Olevo, kama hakusoma apambane na uhasibu. Ila atafute muongozo wa TCU hata wa mwaka jana asome entry requirements wenda zimebadilika..
 
Back
Top Bottom