ni sahihi kurudiana na kuoa mwanamke aliyekwenda kuolewa na mtu mwingine akaachika??

Zekidon

JF-Expert Member
May 29, 2013
1,903
566
Yamemkuta Rafiki yangu anahitaji ushauri.

Ipo hivi!!!!

Alikuwa na mwanamke wake kwa kipindi cha miaka mitatu. Akawa akimpa huduma zote.

Kwa kiburi chake, mwanamke akamuacha rafiki yangu, akakimbia kuolewa na mwanaume wake wa zamani.

Baada ya miezi mitatu tu ya ndoa, huko alikokuwa ndoa ikamshinda. Wakawa wamerudi katika mahusiano tena ( yule mwanamke aliyeachika na rafiki yangu) hapo kumbuka bado alikuwa hajaachika. Wameendelea katika mahusiano kipindi chote mpaka wakati wanatengana yule mwanamke na mumewe.

Sasa tatizo lipo kwa rafiki yangu kuwa, anaona sio sahihi kumuoa huyo mwanamke kwani alichomtenda awali haikuwa sahihi.

Mwanamke alimdhalilisha sana jamaa kwa kuolewa na mtu mwingine, ila huko nako akashindwa .

Je ni sahihi kurudiana na hatimaye kuoana na mtu ambaye hapo awali alikutendea mabaya??

Tumsaidieni huyu ndugu yetu.
 
Huyo sio mwanamke ni shetani, akimrudia siku nje pakitiki ataondoka tena, mwanaume kamili unarudianaje na mwanamke mshenzi wa hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ndo ipo apo maana mwanamke alipokua kwa mumewe mshikaji akarudisha majeshi kwa bi Dada kwaio nae akawa anatembea na mke wa MTU...sasa bi Dada kaachika ndo anaanza kujiuliza vimaswali uchwara kama ivo kama anaona si sawa asinge rejesha majeshi angemwacha aende mazima....amelikologa na alinywe

am better here
 
Hamna mapenzi hapo ushauri aendelee kupiga mechi tu kula mzigo akishikwa na ham anamuita huyo sio mwanamke wa kuweka ndani hafai kuolewa
 
Shida ndo ipo apo maana mwanamke alipokua kwa mumewe mshikaji akarudisha majeshi kwa bi Dada kwaio nae akawa anatembea na mke wa MTU...sasa bi Dada kaachika ndo anaanza kujiuliza vimaswali uchwara kama ivo kama anaona si sawa asinge rejesha majeshi angemwacha aende mazima....amelikologa na alinywe

am better here

Mwanamke pia alishindwa kulinda ndoa yake huyo kicheche wengine ni wakuchezewa tu ipo hivyo
 
hawana confidence kwenye maamuzi yao both mwanamke na huyo mshikaji wako
 
Mambo mengine mazee, sio ya kuomba ushauri .

Mara mia nioe mwanamke nlomkuta ana mtoto/watoto na baba yao simjui .....

Lkn sio kuoa janamke lilokua lipenzi lako ,, likakukimbia, likaenda kuolewa na ukajua limeolewa nauko liliko linapigwa miti....

Kisha likashindwa. Lirudi kwako alafu ulioe ??????

Sikia katika kumfundisha Mtu Maana halisi ya Maisha, Mambo km haya mbigu huyaruhusu kabisaaa, ili liwe funzo, kwake mwenyewe na kwa wengine .

The Devil puts a spoonful of honey into neighbor's Wife
 
Back
Top Bottom