Ni sahihi kumuacha mchumba au kumuoa kufuata wapambe wanavyosema licha ya kuona sifa ulizopanga kazikidhi? Ipo nafasi ya washauri kwa mpenzi wako?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Kila anayechumbia anakuwa na malengo na mipango yake na sifa alizojiwekea kuwa lazima nioe au nioelewe na mtu mwenye sifa kadhaa!!

Je unaweza kumuacha mtu wako kisa maneno ya wanaosema hata kama amekidhi vigezo vyako?

Mfano wakwambie
Ni mwizi
Ni malaya
Ana mtoto usioe mwenye mtoto
Kwao wanafiki
Au wachawi

Je utamuacha!!!

Je ipo nafasi ya washauri kwenye maamuzi yako ya mpenzi umpendaye?
 
Uamuzi wa kuoa/kuolewa ni utashi wa mtu binafsi. Yes watu wanao kuzunguka wanaweza wakawa na nafasi ya kukushauri kabla ya kuingia kwenye ndoa, ingawa hii hutegemea na pia unapo changanya za kuambiwa na zako.

Kuoa/kuolewa sio kwaajili ya wengine, hii ni wewe na mwenza wako kwa manufaa ya maisha yenu kama mlivyo panga ninyi wawili. Mke/mume sio wa familia bali ni mke wako/mume wako wewe peke yako.

Na hakuna aliye mkamilifu, hivyo tunapaswa kuvumiliana hasa tunapo amua kuingia kwenye ndoa.
 
Bhana eeeh we moyo Kama umemdondokea na ana tutabia tuzuripo vuta jiko Hilo,

Nadhani Una mchumba mwenye mtoto Sasa ukiunganisha kejeli za humu kuhusu masingo mama nafsi ikutukuta,,
Hahaha Noeliaaaaa
 
Haiwezi au inaweza kuwa sahihi kutegemeana na muktadha wako.

Nafasi ya watu ni ushauri.

Lengo la ushauri wowote ni kukuongezea machaguo (options) ukiwa unafanya uamuzi, siyo kukuamulia.

Fanya maamuzi sahihi kwa kutumia ushauri unaopewa pamoja na akili yako.
 
ushauri wa kupewa changanya na akili zako aswa kwenye taasisi nyeti ya mapenzi ukikosea kuoa itakukosti sana mkuu
 
Nafasi ya watu kwenye mahusiano yako ni ushauri tuu, uamuzi wa kuufata au kuacha unabaki kwako.
 
Uchumba na Ndoa vinahitaji akili komavu. Ya kusikia na kuona ni mengi inahitajika utimamu kuchagua na kushinda.
 
Kila anayechumbia anakuwa na malengo na mipango yake na sifa alizojiwekea kuwa lazima nioe au nioelewe na mtu mwenye sifa kadhaa!!

Je unaweza kumuacha mtu wako kisa maneno ya wanaosema hata kama amekidhi vigezo vyako?

Mfano wakwambie
Ni mwizi
Ni malaya
Ana mtoto usioe mwenye mtoto
Kwao wanafiki
Au wachawi

Je utamuacha!!!

Je ipo nafasi ya washauri kwenye maamuzi yako ya mpenzi umpendaye?
Watu tunashindwa kuelewa kuwa sio eti kwa kuwa ni mshauri basi akushauri kila kitu.

Kwanza kabisa ukiona mtu anakushauri kuoa na wewe ukaoa basi ujue umeoa kwa sababu ya mshauri wako yuko tayari wewe uoe na sio unaoa kwa sababu uko tayari wewe kuoa.

Sasa kuoa unatakiwa wewe mwenyewe ndo ujishauri na uone kuwa upo tayari.suala a kutaka kuoa halina ushauri.

Pili suala la mwanamke wa kuoa hutakiwi kupata ushauri wa yeyote.

Unachotakiwa kupata ni data za huyo mwanamke wako mtarajiwa kama ana tabia njema ama hana na sio vinginevyo.

Sio kuwa eti ana sifa uzitakazo ila watu wanakuambia usioe kwa sababu wao hawajampenda,kwani wewe ndugu zako wote waliooa wanawake zao ukiwaangalia alafu imagine wewe ndo ungekuwa unawachagulia wake je ungewachagulia wake hao waliokuwa nao ?

Lakini unaishi nao hao wake zao na hamna shida aliyempenda ni mume.

Nafasi ya washauri ni kukuhabarisha mwenendo wa binti kama ana sifa anazotaka,mbali na hapo labda wakuambie kuwa kwa sasa usioe kwa sababu ya kadhaa wa kadhaa.

Laikini uko tayari kuoa eti unaambiwa huyu usimuoe eboh.

Hao washauri wataondoka utabaki wewe na mkeo.

Nyie ndo mnatakiwa mpendane kwanza.
 
Back
Top Bottom