Ni sahihi kumkalisha chini mzazi au ndugu aliyekuzidi umri ukamwambia mapungufu yake?

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,704
Imezoeleka mtoto au ndugu wakikoseana au ukifanya mambo ya hovyo kuitana na kuwekana sawa kulingana ni rika za wahusika.

Nimetakiwa nimweleze kaka yangu ambaye amenizidi umri niongee naye jinsi baadhi ya mambo anayofanya haiwapendezi wazazi wanamtaka abadilike, nimejaribu kukataa wamenabia wamenichagua mimi nimwambie.

Pamoja na mapungufu yake lakini namheshimu sana kaka na tunaelewana nimejikuta nimeshindwa kumwambia niliyo agizwa na wazazi!

Waliowahi kuwarekebisha waliowazidi umri nipeni uzoefu wenu mliwezaje.

Ahsante.
 
Ulichokosea ni kutaka kumchana makavu ndugu yako bila kutumia ile dawa ya kujaza ujasiri wakati una ma aibu sana. 😁😁😁

Tafta kinywaji kikali upige shots kadhaa, utamuona bro wako kama aki na ukwa tu!!!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Aisee bahati mbaya sio mlevi.
 
Ulichokosea ni kutaka kumchana makavu ndugu yako bila kutumia ile dawa ya kujaza ujasiri wakati una ma aibu sana. 😁😁😁

Tafta kinywaji kikali upige shots kadhaa, utamuona bro wako kama aki na ukwa tu!!!
Punguza ukauzu mkuuπŸ˜…πŸ˜…
 
Kumbe kaka sasa kwanini usimchane tena kama anazingua wazazi sio tu kumchana unamkata kata kabisa.
 
Muite kaka yako, kaeni sehemu tulivu ukiwa na bashasha zote, baada ya maongezi ya hapa na pale mwambie una jambo zito unataka kumueleza, atakua makini kusikiliza, mtake radhi kwanza kisha mwambie ulikaa na wazazi wakawa wanasikitika kuhusu tabia zake kadhaa, wewe kama ndugu na mwenye mapenzi kwake ukaona si vema kunyamaza wakati wazazi wenu wanasononeka hivyo umeamua umwambie na ajirekebishe ili apate radhi za wazazi wenu,

Muhimu; usioneshe kama umetumwa na wazazi au mtu yoyote, onesha kua umeguswa na masononeko ya wazazi hivyo umeamua umwambie na kumtaka akawaombe radhi wazazi wake.
 
Ulichokosea ni kutaka kumchana makavu ndugu yako bila kutumia ile dawa ya kujaza ujasiri wakati una ma aibu sana. 😁😁😁

Tafta kinywaji kikali upige shots kadhaa, utamuona bro wako kama aki na ukwa tu!!!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ati aki na ukwa..
 
Ni kawaida sanaa, inategemea na aina ya familia unayotokea, mimi ni kijana mkubwa wa kiume kwenye familia yetu. Walionitangulia ni wanawake wakubwa watu wazima wapo kwenye early 40's lakini wakikosea, au bi mkubwa akikosea huwa nawaweka chini vizuri tu nakuwaeleza. Uzuri wananisikiliza/tunasikilizana vizuri kabisa.

Let's meet at the top, cheers πŸ₯‚
 
Jana night mdogo wangu wa mbaali sana kiumri kaniwakia kisa nimechelewa kuja home na naendesha nimelewa, kidogo nimtoenduki kwangu ila nikajua nimezingua..

back to your Q yes, inawezekana ila changua lugha ya kuzungumza nae
 
Muite kaka yako, kaeni sehemu tulivu ukiwa na bashasha zote, baada ya maongezi ya hapa na pale mwambie una jambo zito unataka kumueleza, atakua makini kusikiliza, mtake radhi kwanza kisha mwambie ulikaa na wazazi wakawa wanasikitika kuhusu tabia zake kadhaa, wewe kama ndugu na mwenye mapenzi kwake ukaona si vema kunyamaza wakati wazazi wenu wanasononeka hivyo umeamua umwambie na ajirekebishe ili apate radhi za wazazi wenu,

Muhimu; usioneshe kama umetumwa na wazazi au mtu yoyote, onesha kua umeguswa na masononeko ya wazazi hivyo umeamua umwambie na kumtaka akawaombe radhi wazazi wake.
Hii Point naichukua nikaifanyie kazi.
 
Back
Top Bottom