Ni sahihi kufanya maendeleo ya Kiuchumi na mpenzi wako?

Nandinii

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
2,573
2,808
Habari wakuu,

Je, ni sahihi kufanya MAENDELEO ya kiuchumi na mpenzi wako ambaye hajulikani nyumbani wala hajawahi kufika nyumbani kwao, hutambuliki, bali tu kwa marafiki baadhi?

Haijalishi mahusiano yenu yamedumu kwa muda mrefu au kwa muda mfupi? Mfano, kujenga nyumba pamoja, kununua viwanja pamoja, kuanzisha miradi mbalimbali pamoja, ni sahihi na unaweza kufanya hivyo na mpenzi wako? Na je hiyo ni ishara kuwa unampenda na kumuamini mpenzi wako Kwamba mnaaminiana?

Binafsi, Mimi siwezi kabisa kufanya miradi na mpenzi ambae hata nyumbani hatambuliki wala sitambuliki. Hata angekuwa anatambulika, mimi siwezi. Maana siku ya siku mmetengana inakuwaje?,

Na yaweza kuwa hata ulichukua mkopo kwa ajili ya huo mradi na hati ya hizo Mali mliandika jina la mpenzi wako. Je utavumilia aondoke na hizo Mali kweli?. Binafsi sijawahi kuwaza kufanya MAENDELEO na mpenzi, bali nimewahi kuwaza kufanya miradi mbali mbali na mume.
 
Sio mpenzi tu, hata kujenga ukweni ni kujitoa muhanga, yaani ukipewa kiwanja ukweni utajenga?! Siku mmeachana nyumba itakuwa ya nani ?! Na kiwanja ni chakupewa na wakwe?! Wakidai kiwanja chao?! Labda ujenge tu kuwasaidia wakwezo lakini jua sio chako asilani!

Kuna mambo lazima ujiongeze, hayafanyiki na mwenye akili timamu, kama kufanya biashara na mpenzi (bila ndoa), kumsomesha mpenzi, kumkopesha mpenzi/ mkwe! Kujenga kwa mpenzi, mkwe.

Labda ufanye hayo yote kama zawadi au kwa upendo tu.
 
Never do that, siku mkiachana kila mtu anabaki na ressentment.. hakuna mfano... yaani muachano wenu hautakua smooth..
 
Back
Top Bottom