Ni Sahihi Kuapa kwa Kutumia Vitabu vya Dini Kwamba Utalinda Katiba ya Jamhuri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Sahihi Kuapa kwa Kutumia Vitabu vya Dini Kwamba Utalinda Katiba ya Jamhuri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibavu, May 6, 2011.

 1. kibavu

  kibavu Senior Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Umekua ni utaratibu kwa viongozi mbalimbali wa kuteuliwa na kuchaguliwa kuapishwa kwa kushika vitabu vya dini/madhebu yao na kuapa kwamba watailinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini watu hao hao wakifanya makosa na kukiuka kiapo chao hushitakiwa kwa mujibu wa sheria zilizotungwa kulingana na katiba ya Jamhuri. Hoja yangu ni kwamba kuna haja gani ya kuapa kwa kutumia vitabu vya dini, na watu wanapokosa wanashitakiwa kwa kutumia sheria za jamhuri? Na je ni kwa nini wasiape kwa kutumia katiba ambayo wanaahidi kuilinda? Najua kuna watu wanaapa kwa kutumia katiba, Kwa nini isingekua hivyo kwa wote kwakua wote wanatumikia katiba ya Jamhuri na si madhehebu/dini zao?

  Nawasilisha.
   
 2. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa dhambi zao hawataki na katiba imtaje Mungu, wanaogopa hilo ili waikiuke vizuri!
   
 3. w

  warea JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara zote watu huapa kwa kitu kilicho juu yao ili waonekane kuwa wanamaanisha wanachosema.
  Watu wote wanajua ndani ya mioyo yao kuwa Mungu ni mkuu kuliko wao, na sio katiba. Katiba zinatungwa na zinaondolewa. Katiba sio kitu kilicho juu ya mwanadamu, ni Mungu pekee.

  Wanaposema tofauti na ukweli wanajivunia dhambi na mshahara wa hizo dhambi ni mauti, wasipotubu.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii hoja ni nzito. Serikali haijui dini lakini viongozi wake wanatumia vitabu vya dini wakati wanaapa kuitumikia serikali!! Hoja inahitaji tafakuri jadidi.
   
Loading...