angelita
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 3,017
- 2,431
Ni kweli umempenda kwa dhati? Wakati mwingine watu huanzisha mahusiano kwa kuwa wamezoea kuonana tu kila siku ofisini, kupeana lunch na zawadi ndogo ndogo hivyo huhisi kuwa amempenda.
Kuchanganya mapenzi na kazi ni sawa na kuchanganya maji na mafuta. Kuwa na mpenzi sehemu ya kazi kwa namna moja ama nyingine huzorotesha ufanisi wa kazi.
Wakati mwingine kunaweza kufanya ukawa na mahusiano mabaya na wafanyakazi wenzako, pale utapohisi ama kujua kuna mtu anamtaka ama ana mahusiano ya kimapenzi na mpenzi wako.
Kuna baadhi ya vitu wakati mwingine hupaswa kuwa siri, mfano umechacha, kama mwanaume vitu kama hivi ni vizuri kuwa siri, lakini kama upo ofisi moja na mpenzi wako lazima atajua na kama ndo mumecheleweshewa mishahara wote mnakuwa na hali mbaya mnaishia kutazamana tu.
Mfano umekosea kazini ukapewa adhabu au kufokewa mbele ya mpenzi wako? Unadhani ni kiasi gani atajisikia aibu mbele za wafanyakazi wenzake?
Ni vyema ukatafakari kwa kina athari za mahusiano ya naamna hii kabla hujayavaa.