Jalema
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 593
- 856
Habari zenu wakuu bila kuzunguka acha niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Mimi ni muajiriwa katika taasisi moja hapa nchini.Miaka miwili iliyopita nilichukua mkopo katika benki moja maarufu tu.Baada tu ya mkopo kuingia kwenye account yangu mwezi uliofuta nilianza kukatwa mshahara.
Katika kukagua kiasi cha fedha ninayotakiwa kubaki nayo baada ya kukatwa kila kitu pamoja na deni ninalodaiwa niligundua kuna mapungufu ya fedha zaidi ya elfu 50 ambayo huwa inakatwa baada ya kukatwa makato yote ikiwa ni pamoja na deni la benki. Nikasema embu nisubiri baada miezi mitatu nione.
Bàada ya huo muda ilinibidi niende benki kwa afisa mikopo nkamuuliza inakuaje nnakatwa fedha ya kulipa deni lenu mara mbili? Akanitolea bank statement akakagua akuta ni kweli jibu alilonipa ni kwamba nisiwe na wasiwasi fedha yote ninayokatwa inaenda kulipa deni.
Wiki iliyopita nimejaribu kupiga calculation ya miezi yote niliyoliopa deni nikalinganisha na fedha ninayodaiwa ili kumaliza deni pamoja na jumla ya fedha ninayotakiwa kulipa yoote pamoja na riba kwa kile kiasi ninachokatwa mwanzo ambacho ni halali hesabu zinakubali
Shida inakuja kwamba nikijumuisha ile elfu hamsini naa inayo katwa mara ya pili baada ya kukatwa kila kitu hesabu zinakataa ambayo afsa mikopo ndio aliniambia inakwenda kufidia deni
Hivyo ninaomba ushauri na kujuzwa je ni sahihi kiutaratibu na kisheria mtu kukatwa mkopo mara mbili kwa wakati mmoja kabla ya mshahara kuingia na baada ya mshahara kuingia.Karibuni wadau kwa msaada