Ni Sahihi Kisheria, Kanuni na Katiba Mtumishi wa Umma kuwa Mwanachama wa Chama cha Siasa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
MOD HUU NI UTAFITI UNAFANYIKA NA UTAWEKWA GAZERINI NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI NAOMBENI MSIFUTE THREAD HII
----------

Habari za Leo wadau wa Jf

Naomba rujadili kwa mapana na Marefu kuhusu Mtumishi wa Umma kuwa Mwanachama wa chama cha siasa je ni sahihi kwa nchi? Wananchi wake au hata nje ya Nchi. Nini hadhari zake kiuchumi kisiasa... Je kwa sasa hivi vyama vya upinzani kutokuwekewa wigo sawawa siasa je mtumishi wa umma akiwa mwanachama wa chama tawala je kunausawa?
 
Mtumishi wa umma ana haki ya kuchagua chama chochote cha siasa lakin anapaswa kuitii serikali iliyopo madarakani,

Na serikali imeundwa na chama cha Mapinduzi kwa hyo unapaswa kuitii chama cha Mapinduzi ambayo ndo iliyounda serikali

Hope umenielewa.......
 
MOD HUU NI UTAFITI UNAFANYIKA NA UTAWEKWA GAZERINI NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI NAOMBENI MSIFUTE THREAD HII
----------

Habari za Leo wadau wa Jf

Naomba rujadili kwa mapana na Marefu kuhusu Mtumishi wa Umma kuwa Mwanachama wa chama cha siasa je ni sahihi kwa nchi? Wananchi wake au hata nje ya Nchi. Nini hadhari zake kiuchumi kisiasa... Je kwa sasa hivi vyama vya upinzani kutokuwekewa wigo sawawa siasa je mtumishi wa umma akiwa mwanachama wa chama tawala je kunausawa?
Huu ni mwandiko wa mtumishi au mwandiko wa mfanyakazi??

Msaada tafadhali
 
Sasa hapo ndio umesema nini? Eti utafiti, utafiti gani unauliza 'the obvious?'

Mnajifanya kujua mpaka unajidhalilisha sasa, hoja zimeisha, ajenda hakuna, kutetea na kukaribisha wezi mpaka mnaona aibu mumebaki kutapatapa eti hadhari, hadhari ndio mini? Dawa imekuingia mpaka unaongea kichaga, dadeki
 
Sheria hii inawabeba zaidi ccm. Embu ajaribu wa CdM tuone kama atabaki salama
 
Sasa hapo ndio umesema nini? Eti utafiti, utafiti gani unauliza 'the obvious?'

Mnajifanya kujua mpaka unajidhalilisha sasa, hoja zimeisha, ajenda hakuna, kutetea na kukaribisha wezi mpaka mnaona aibu mumebaki kutapatapa eti hadhari, hadhari ndio mini? Dawa imekuingia mpaka unaongea kichaga, dadeki
Haya yote Ni kwa mada hii au wewe una mengine zaidi!! Tusubiri wajuzi wa Mambo wajadili na wengine wengi tunufaike. Nafikiri Kakosea neno kwa watumiaji wa smartphone Ni kawaida sana.
 
Sasa hapo ndio umesema nini? Eti utafiti, utafiti gani unauliza 'the obvious?'

Mnajifanya kujua mpaka unajidhalilisha sasa, hoja zimeisha, ajenda hakuna, kutetea na kukaribisha wezi mpaka mnaona aibu mumebaki kutapatapa eti hadhari, hadhari ndio mini? Dawa imekuingia mpaka unaongea kichaga, dadeki
Hujaelewa chochote hadi naona aibu !
 
Mtumishi kuwa mwanachama,mkeleketwa na kiogonzi wa CCM ni haki kabisa ila kuwa mwanachama tu wa chama chochote cha upinzani unahesabika kama MUHAINI kwa mjibu wa nadharia ya serikali ya Tanzania.
 
ninachofahamu sheria inakataza baadhi ya watumishi hususani wa vyombo
vya ulinzi na usalama.
Ila watumishi wengine wanaruhusiwa kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila
wanakatazwa kufanya siasa wakati wa kazi au kutoa huduma kwa misingi ya itikadi za kisiasa.
Sheria inakataza watumishi wa umma kuwa viongozi wa kisiasa tu.
Ila ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watumishi wa umma ni viongozi wa kisiasa mfano nawajua walimu wengi vijijini
ni wenyeviti wa vijiji ambacho ni cheo cha kisiasa. kitu ambacho hakitakiwi lakini kwa kuwa ni wenyeviti kupitia ccm
wamachuniwa.
Na hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya watumishi wa umma mfano kuna das, ma dc,ma rc eg mnyeti, amepitishwa kuwa mnec (CCM) kupitia wilaya au mikoa yao.
Tusubiri vikao vya juu vya ccm kama vitawapitisha, kimsingi wakipitishwa watakuwa wamekosa sifa za kuwa watumishi wa umma.
Ila kwa mkumbo , just kuwa mwanachama kwa kazi yake ya ukatibu mkuu sio kosa kisheria
 
Mtumishi wa umma ni mtu yeyote anayetoa huduma kwa wananchi kwa niaba ya Serikali.

Mtumishi wa umma kwa wadhifa wake anahudumia jamii nzima ya watanzania,hivyo haruhusiwi kutoa huduma kwa upendeleo au unyanyapaa kwa yeyote yule haijalishi dini yake,chama chake au rangi yake.

Kwahiyo utaona ni kwanini kanuni za Serikali zinakataza mtumishi kuwa na cheo cha kisiasa,ila usiwepo mgongano wa kimaslahi kati ya majukumu yake kwa kundi dogo la wanachama wenzake na kundi kubwa la umma wa watanzania walio wa vyama vingine au wasio na vyama kabisa.

Ila kwa Tanzania hii ni tofauti hasa ukiangazia asili na tabia zote za mfumo wa Ujamaa,mfumo huu lengo lake kubwa ni la Chama kinachotawala kujipenyeza kila eneo hata Serikalini ili kujiakikishia usalama na mafanikio yake

Na hii ndiyo inayopelekea kuwepo kwa ile dhana ya Chama Dola.

Ni kinyume cha taratibu na sheria,ila ndiyo njia pekee iliyobaki kwa Chama Dume kubaki hai na kuendelea kuongoza hatamu zote za Dola.
 
Mtumishi wa UMMA asiyeruhusiwa KUJIUNGA na chama cha SIASA ni askari POLISI, askari JW, ASKARI UHAMIAJI, ASKARI MAGEREZA NA MAOFISA WA TISS
 
Ni suala zito kwa watawala ndio mana mjadala wa Katiba mpya umezimwa. Lakini tangu ukoloni mtumishi wa umma hakuruhusiwa kujihusisha na siasa kumbuka Mwalimu J.K. Nyerere alivyolazimia kuacha kazi ili aimarishe TANU. Mtasema oh huyo ulikuwa ukoloni, lakini mbona mnavunja nyumba za watu kwa sheria walizoacha wakoloni?
Pili ikiwa Katiba inamruhusu Spika kuendelea kuwa mwanachama wa chama cha siasa, halafu Rais kuwa "sehemu ya Bunge"; kuna mantiki gani kumkataza mtumishi wa umma kuwa mwanachama wacchama cha siasa?
Nirudie usemi wangu was kawaida (bahati mbaya ni was kiingereza naomba radhi):
Hallmarks of bad governance:
1. Arbitrariness
2. Ambiguity
3. Capriciousness
David Baldacci kwenye kitabu chake 'Saving Faith' anasema: "to seek accolade from the great and ignorant public is the vice of a fool". Baldacci ananikumbusha msemo wa mitaani kwamba: "mtaka sifa haogopi hasara"
 
Salaam
Naomba kuuliza hivi mtumishi wa umma anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Kama ndiyo naomba msingi wake kwa kuzingatia sheria za utumishi wa umma.
Naomba kuwasilisha kwa wajuzi wanisaidie
 
Haruhusiwi. Akitaka siasa anaachana na utumishi wa umma kinyume cha hapo sheria ya utumishi wa umma inambana.
 
Sasa ni vyema mngeweka na hivyo vifungu vya sheria vinavyoeleza huwo Uhuru wa watumishi wa umma kujumuika na vyama vya siasa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom