Ni sahihi kampeni za Uchaguzi kuanza wakati Mgombea mmojawapo amewekewa Pingamizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sahihi kampeni za Uchaguzi kuanza wakati Mgombea mmojawapo amewekewa Pingamizi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Mar 15, 2012.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sielewi tuna sheria gani na kanunu za Uchaguzi. Mfano katika Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika April Mosi katika Jimbo la Arumeru Mashariki, mmoja wa Wagombea amewekewa pingamizi na mgombea mwenzake lakini cha kushangaza wote wemezindua kampeni huku shauri likiwa bado halijatoka.

  Kuna haja ya kuangalia upya hii sheria ya uchaguzi maana ikitokea hivi sasa Mgombea aliyewekewa pingamizi shauri lakamwondoa kwenye kinyang'anyiro itakuwa limemuingiza hasara kubwa yeye binafsi kama mgombea na chama chake ambacho kimeshazindua kampeni na kinaendelea na kampeni.
   
 2. n

  nrashu Senior Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumbiri, Pia mimi sikuelewa sababu ya kampeni kuendelea huku kukiwa na Pingamizi. Ila ndugu yangu nimefahamishwa kuwa uamuzi unajulikana ila lazima uelewe maana ya chama tawala kwenye nchi kama hii.
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Sasa ulitaka waahirishe uchaguzi kwa sababu ya mtu mmoja?? Kama mgombea atapigwa chini hiyo ndiyo hasara yao kwani walitakiwa kulijua hili kabla. Haiwezekani upinzani wakajua kuwa SIOI hana sifa za kugombea kama raia halafu yeye mwenyewe na CCM hawakulijua hilo. Kwa taarifa za mwanzo, swala la uraia wa SIOI lilizungumziwa CCM ila CCM kwa kibri chao wakaamua kumpitisha. Sasa ngoja tuone hizo evidence nyingine ambazo SIOI hakuwaonyesha CCM zitakapotoka na pamoja na maamuzi ya NEC!!
   
 4. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...mkuu kumbuka ya kuwa mwenyekiti wa chamama "CCM" ndo amemteua mwinyekiti wa tume ya uchaguzi,hapa ni sawa na kesi ya Tumbiri hakimu ni Ngedele...
   
 5. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Double standards!!..
   
 6. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ingekuwa ni mgombea wa Chadema amewekewa pingamizi sheria ingetafutwa mpaka mvunguni. ila madam ni mgombea wa Chama Cha Maasi basi kampeni zitaendelea
   
 7. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ila wafanye kama walivyomfanyia shitambala na chadema mwaka 2008 kule mbeya,hatutaki ubabaishaji
   
 8. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Jamani mbona tunatoa hukumu kabla ya kesi yenyewe, CDM wanadai Sioi sio Mtanzania, bado ni Madai tu, hayajathibitishwa hivyo bado anasifa mpaka itakapoamuliwa vinginevyo.
   
 9. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu siyo kwamba Mimi nataka waahirishe uchaguzi. La hasha! Lakini kimantiki kampeni zilipaswa kuanzwa wagombea wote wakiwa safi (Siyo huyu ana pingamizi, yule hana). Chukulia mfano hii ishu ingemkuta Nassari. Mi hoja yangu hapa ni kwamba Tume ya Uchaguzi iwe inatangaza tarehe ya kuanza kampeni baada ya kutoa shauri ya mapingamizi!
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa hatuzungumzii ishu ya Sioi na Nassari. Ndiyo maana hata ukiangalia thread husika sikutaja chama wala mgombea. Lengo likiwa ni kuiondoa thread katika mazingira ya kiitikadi. Ishu hapa ni kwamba kwa nini Sheria ya Uchaguzi na kanuni zake zinaruhusu kampeni kuanza wakati kuna pingamizi kwa mgombea mmojawapo?
   
Loading...