Ni sahihi kabisa siasa kuwepo kwenye vyuo vikuu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sahihi kabisa siasa kuwepo kwenye vyuo vikuu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, May 18, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wapo watu wanaotaka kutuaminisha kabisa kwamba migomo kwenye vyuo vikuu inasababishwa na siasa. Wamejaribu kupotosha kabisa maana halisi ya siasa ili kuonyesha udhaifu wa kiutendaji katika baadhi ya vyuo vikuu nchini, wizara na bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Hakuna mtu duniani 100% anaweza kikimbia siasa, siasa ni sawa na maji lazima utayanywa.

  Wanachoshindwa kutambua kuridhia kwenye nafsi zao kwamba siasa ni elimu, maarifa na ujuzi ambao hutoa msimamo na msingi wa jamii, kila jamii huwajibika kufuata misingi iliyowekwa katika maisha ya kila siku. Taasisi za elimu ya juu zilipaswa ndio ziwe tanuri la kuibua fikra mbadala kuelekea kwenye mafanikio ya kijamii na kiuchumi.

  Pamoja na kwamba siasa haijatambulika rasmi vyuo vikuu, ukweli tunaposwa kutambua kwamba siasa zipo sehemu yoyote ile. Mara nyingi ninashangaa mtu anayesema mimi sitaki mambo ya siasa wakati tunapanga na tunaishi na siasa. Natambua matendo ya ubabaishaji ya viongozi wetu ndio yanafanya kuibuka kwa fikra hizi lakini hatuwezi kujiridhisha na madhaifu ya kiutawala bila kutumia fikra zetu kutafakari mustakabali wa taifa letu kuanzia kwenye taasisi za elimu ya juu, na hatimaye kuleta mapambazuko ya kifikra ndani ya taifa letu.

  Ni sahihi kabisa mijadala ya kisiasa kuhusu kuwepo kwenye vyuo vikuu.

  Nawakilisha.

   
Loading...