Ni sahihi CCM kumtumia Mwanasheria Mkuu kwa mambo ya chama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sahihi CCM kumtumia Mwanasheria Mkuu kwa mambo ya chama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Apr 13, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  kwenye RaiaMWEMA la leo, kuna habari yenye kichwa "Rostam, Lowassa wakatwa miguu". Kwenye habari , inaeleza kwamba Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema aliharakisha kuanguka kwa watuhumiwa wa ufisadi. Mwanasheria Mkuu aliitwa kwenye kikao cha chama kuja kufafanua mambo kadhaa kama mchakato wa Katiba mpya. Werema alianza kwa kusema yeye si mwana CCM. Maana yake alikua pale kwa wadhifa wake kama Mwanasheria Mkuu. Je hii ni sahihi? Chama chengine kama Chadema, TLP etc kikimhitaji kwenye vikao vya chama kutoa maelezo ataenda?
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nchi hii ina vioja vingi sana, na werema naye wala hajui sheria kabisa! si ingetosha tu kama angesema yuko pale kama rafiki yake JK? nafikiri ingesound fair kidogo.

  inaonekana ili kujivua magamba ilibidi kuongezea magamba mengine juu kwa juu
   
 3. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  nimekua nikiongea na rafiki zangu wengi tulosoma nao wao wako chini yake wanasema hajui sheria vizuri cjui ujaji huo aliupataje
   
 4. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii nchi na marukfuku kuwa mtumishi wa umma then ukawa mfuasi au mwanachama wa chama fulani, ila sheria isiyo andikwa popote ila inadhihirika kwa vitendo vyake iko hivi - ili uwe mtumishi wa umma na upate nyadhifa za juu lazima uwe kada wa CCM na hata wakati promotion wanaangalia CV yako katika chama au mchango wako ni upi na ikidhibitika we ni mfuasi wa upinzani basi kazi huna, kama werema angeitwa na chadema asingezidi miezi mitatu kazini

  Kwani CCM si wana wanasheria wao kama Masumbuko Lamwai, Benno Malisa na wengine wengi au hizo nyadhifa ni vivuli tu?
   
 5. K

  KWELIMT Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wana JF mnashangaa nini? aliyemteua ndo m/kiti wa kile kikao,akimhitaji ili atoe maelezo na ushauri wa masuala ya kisheria atakataaje?.Sasa ndo maana inapendeza sana waziri wa mambo ya sheria awe weledi ktk eneo analooongoza ili kuepuka mkanganyiko huu.Na co AG tu nakumbuka kuna kipindi aliitwa Gavana wa BOT kwenye vikao vya ccm kueleza hali ya uchumi!

  KATIBA MPYA NDO MWAROBAINI TUKATOE MAONI CHANYA
  ish...............ish..........................mmh..................woooo.....................oooh......
  :confused3:
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tatizo watu wengi tumepewa madaraka lakini hatujui ni kivipi tunatakiwa kuyatumia madaraka hayo. Katiba iko wazi kuwa:

  59. Mwanasheria Mkuu wa Serikali


  (3) Mwanasheria Mkuu atakuwa ndiye mshauri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na, kwa ajili hiyo, atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria zitakazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais kuzitekeleza, na pia kutekeleza kazi au shughuli nyinginezo zilizokabidhiwa kwake na Katiba hii au na sheria yoyote.

  Kama alienda yalikuwa makosa makubwa sana kwani hiyo kazi haiko kwenye Katiba wala sheria
   
 7. B

  Bobby JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  FFT nashukuru umeleta hii issue hapa. Binafsi nadhani sio sahihi na ni makosa makubwa lakini kwakuwa ni Tanzania hamna noma tutaenda hivyo hivyo tumezoea.

  Nimeona pia in one of the blogs asubuhi picha kadhaa za vikao vya ccm Dodoma. Hizo pictures zote zimepigwa na Fred Maro ambaye ni mpiga picha wa rais wa JMT si mwenyekiti wa ccm. Bahati mbaya sana rais kwa sasa ndiye mwenyekiti wa ccm. You may think kwamba I'm going too far lakini it feels bad kwa mimi ambaye sina hata kadi ya chama chochote kodi yangu kutumika directly kwenye mambo ya ccm. CCM wanashindwa nini kuwa na mpiga picha wao akapiga picha za mwenyekiti wao? Sihitaji uthibitisho wa kutoka kwa yeyote kwani I'm sure Fred alikwenda Dodoma kwa pesa ya ikulu wakati safari nzima ilikuwa kwa ajili ya ccm. ccm mnaboa sana jifunzeni kuwa na uungwana japo kidogo.
   
 8. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba yetu mgogoro kwa vile haionyeshi wapi JK anakuwa mwenyekiti na ccm na pahala gani anakuwa rais, hivyo hata mpambe wake ndani ya vikao vya ccm anakuwapo. Hii yote ni mwendelezo wa matumizi ya mapesa ya mlipa kodi kwa shughuli za ccm. Watz tunaliwa na ccm!
   
 9. d

  dotto JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Watabalali!!ngoja tumuone!!
   
 10. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kwenye blue.Je kama Rais kikwete alimuagiza kufanya hivyo?.
   
 11. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  ndio kosa lenyewe hilo! Kikwete hakuenda Dodoma kwenye kikao kama Rais wa JMT alienda kama Mwenyekiti wa CCM Taifa. Wapi kwenye katiba ya JMT Rais anapewa mamlaka ya kuvunja sekretariat na kamati kuu ya CCM? Hii ni kwasababu alienda kama Mwenyekiti , na sio Rais wa JMT. Kutumia "resources" za IKULU ni KOSA!
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Katiba yetu haina mgogoro wowote watu ni overzelous tu, wanapenda kuwa jirani na mfalme masaa yote hamna kingine
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kwenye hiyo sentesi ya bluu kuna neno "au". Hilo neno halikuwekwa kimakosa limewekwa makusudi kunekuwa na tofauti kubwa kama sentensi hiyo hiyo ingekuwa na neno " na " au kungekuwa na neo " na". Kwa hali hiyo neno hilo au kabla ya maneno ya bluu ni kazi mbadala ya "na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria zitakazopelekwa kwake"

  Alichofanya huyu bwana haiangukii chini ya sentensi inayotangulia au mbadala wake uliouweka kwenye bluu.

  Hakutakiwa kabisa kwenda kwenye kikao hicho kwa nafasi yake kama Hon. AG
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  AG alikwenda kwenye kikao kile kutoa darasa kwa wajumbe wa CC ya NEC ya CCM juu ule muswada tete wa mchakato wa kuunda tume itakayoratibu maoni ya uundwaji wa KATIBA mpya. Akachangia na mengine mazuri tu kulingana na RaiaMwema ya leo. Sidhani kama akiitwa kwenda CUF, CHADEMA kwa nia njema kama ile atakataa.
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,345
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Wanaongea kirahisi lakini hawawezi kutenda............hii ndiyo ccm ile aliyoitabili kabla ya kifo chake baba wa taifa hayati mwalimu julius kambarage nyerere (jk halisi) ambaye hakutaka kupewa phd za aibu
   
Loading...