Ni sahihi baba mwenye umri miaka 65 kuzaa ?

ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,275
5,961
Naomba ushauri. Baba yangu ana umri wa miaka 65 ametuzaa watoto 12. mtoto wa mwisho ana miaka 27. Lakini Baba ameamua kuzaa na binti (sio mama yetu au mama zetu) mwenye miaka 28. Jamani huyo mtoto atalelewa na nani wakati baba anatutegemea sisi wanae kwa matumizi.
Mzee akifariki leo je katika orodha ya warithi wa mali za mzee na huyo mwana ataorodheshwa. (SIO KAMA nINA MIND MALI ZA MZEE) Kila mmoja wa wanawe anajitegemea. Je mtoto huyo kama ataandikishwa kama mrithi mbona hajachangia chochote. au ndio zitamsaidia ili naye aewze kusoma? naomba msaada wenu wa ndugu.
 
mnampa hela nyingi ya matumizi mzee wenu mpaka anapata za kuhonga?(ndo maana amezaa huko)

ila swala la kuchangia mali za mzee sikuungi mkono huo ni uchoyo.

Kwa umri wa mzee wako mjiandae kumlea mdogo wenu huo utakua mzigo wenu
 
Kuzaa hakuna mipaka ila ni utashi wa wahusika. Sijui Baba yako ni mwumini wa dini gani? Lakini kwa vile Mahakama ya Kadhi haijaanza na umeamua kumchuria Baba yako ukiamini atatangulia kufa kabla yako, angalia haya. Sheria za mirathi za nchi hazimtambui mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Kama yupo aliyezaliwa nje ya ndoa basi mzazi (Baba) anatakiwa amgawie urithi mtoto husika wakati wa uhai wake. Vyovyote itakavyokuwa jiandaeni kulea wadogo zenu. La mwisho unaweza kumpeleka hospitali Baba yako akaondolewa uwezo wa kutia mimba akabakiziwa ya starehe tu.
 
Inaelekea huyo baba yako ni wembe kweli. Nadhani mama yenu/zenu hawamtoshelezi, hivyo usimlaumu
 
eti mtoto amechangia nini, kwani wewe umechangia nini?mtoto ni mtto tu
 
na huyo binti wa miaka 28,hana haki ya kupata mtoto?????

mbona unafikiria upande mmoja tu?
 
Hivi mwanaume huwa anazaa?
Naomba mwongozo kwa hili wadau..
 
Nilifikiri utahofia kua mtoto hatakua healthy... Kumbe mambo ya Mirathi... I am dissapointed.... SORRY.
 
dah! mie nadhani kama ni baba yangu kafanya hivyo, nitasema na step mom. frankly, 'mama kwa heshima na taadhima,do u have plan b na huyu mtoto/watoto? coz dont count on me!'anatafuta eda huyo bibie, transgenerational ni mbaya sana! kwanza baba yenu yuko kwenye high risk ya kupata magonjwa ya zinaa!alishindwa kupata mzee mwenzie.
 
Nilifikiri utahofia kua mtoto hatakua healthy... Kumbe mambo ya Mirathi... I am dissapointed.... SORRY.

Nani alikwambia mwanaume akiwa na umri mkubwa ndio huzalisha watoto wenye afya hafifu? Inategemea na life style ya mtu na afya yake; kuna watu wana miaka 65 lakini afya yao bomba na wanapiga muziki bila ya kutumia Viagra!!
 
Kuzaa hakuna mipaka ila ni utashi wa wahusika. Sijui Baba yako ni mwumini wa dini gani? Lakini kwa vile Mahakama ya Kadhi haijaanza na umeamua kumchuria Baba yako ukiamini atatangulia kufa kabla yako, angalia haya. Sheria za mirathi za nchi hazimtambui mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Kama yupo aliyezaliwa nje ya ndoa basi mzazi (Baba) anatakiwa amgawie urithi mtoto husika wakati wa uhai wake. Vyovyote itakavyokuwa jiandaeni kulea wadogo zenu. La mwisho unaweza kumpeleka hospitali Baba yako akaondolewa uwezo wa kutia mimba akabakiziwa ya starehe tu.
Sio kwamba namchuria baba hapana. Ukiondoa mipango ya mwenyezi Mungu Binadamu tunaamini kuwa aliyetangulia kuzaliwa atangulie mbele ya haki pia. Refer: LIFE EXPECTANCY OF HUMAN BEING. Ndio maana vijana wakitangulia kufa kabla ya wazazi, wazazi hujisikia vibaya atakayewazika nani kama nguvu kazi itatangulia.
 
Nani alikwambia mwanaume akiwa na umri mkubwa ndio huzalisha watoto wenye afya hafifu? Inategemea na life style ya mtu na afya yake; kuna watu wana miaka 65 lakini afya yao bomba na wanapiga muziki bila ya kutumia Viagra!!
kama ulinielewa vizuri mtoto wa mwisho kwetu ana miaka 27 na wote tunajitegemea na wazazi wetu wanatutegemea sisi( MATUNZO). Mirathi ni by the way kwa maana ya mila za kiafrika. Naomba ushauri wa kisheria tu. Huyo mtoto ni wa baba na mkewe na kila mzazi anao wajibu wa kutunza watoto wake.
 
na huyo binti wa miaka 28,hana haki ya kupata mtoto?????

mbona unafikiria upande mmoja tu?
HAHOFII KUACHWA MJANE AKINGALI BINTI? AU NDO MAPENZI HAYANA UMRI WALA KABILA? Pia kumbuka kijana wa mwisho kwetu ana karibu umri sawa na huyo mama yetu(MKE MDOGO WA MZEE) miaka 27 against 28.
 
labda alimpata bahati mbaya,mumkalishe kitako asizae tena na akizaa ajue atalea mwenyewe na sio kuwabebesha nyie mizigo.......kuhusu mirathi yeye ana haki kama mlivyo nyie hajapenda kuletwa duniani ila baba yako na ujinga wake ndio amemleta
 
inawezekana sio mdogo wenu pia,hivi vibinti vya mjini vijanja sana kny kubambikia mimba especially kama wakiona sehemu kuna masalahi,mirathi mshirikisheni huyo mtoto/mdogo wenu kwa sababu hana hatia ila huyo mama yake/huyo msichana hakikisheni hapati hata senti...hakuwepo wakati baba yenu na mama zenu wanachuma hizo mali period.
 
Back
Top Bottom