Ni safari gani "very risky" umewahi fanya kwa ajili ya mpenzi wako na bado ikaishia na machozi?

musicarlito

Senior Member
Dec 29, 2020
176
289
Wasalaam

Nilikuwa na manzi wangu nikiishi Ubungo Riverside by then, yeye akiishi Mbezi Kimara. Alikuja kunivuruga na chanzo kikiwa ni issue za kutoaminiana, aliniomba msamaha lakini nilikuwa nimeamua kumuacha na niliapa kutorudiana naye.

Baada ya mitihani alirudi kwao Arusha, masikini kumbe sikuwa na uhakika wa uamuzi niliofanya, bado nilikuwa nampenda. Nilijaribu kumuomba msamaha kwenye simu turudiane aligoma, baadae alinionea huruma na kunambia kama kweli nampenda niende Arusha tukayajenge.

Kwa mara ya kwanza nilipanda basi kuelekea Arusha, nikampa taarifa mwenyeji wangu alanambia nisijali ananisubiri, tulipofika Moshi nilimtaarifu akanipa pole akanambia niwe na amani.

Tunakaribia stendi nikampigia akanambia niwe mvilivu atachelewa kidogo...tulifika saa 2 usiku...nilipiga simu mara nyingi haikupokelewa, baadae simu ilikuwa haipatikani kabisa.

Sikuwa na jinsi zaidi ya kupanda basi jingine asubuhi kugeuka Dar, nikiwa njiani tumeiacha Moshi ikaaingia text yake ananiomba samahani anauliza bado niko stendi?

"Mellisa nimeshakusamehe ila sintokuja kusahau"

Safari gani huji kuisahau?
 
Kwenye graduu ya kidato cha 6 nilipanda basi paka Songea.

After there nilimpa simu na laptop ya kufanyia application za chuo na ile pesa ya kulipia TCU nilimpa alipopata chuo akaniacha. The same year nilimnyima mdogo wangu vyote hivyo nilimwambia apambane na hali yake.

Ney popote ulipo bado sijaisahau toshiba yangu.

Karma is....
Ujana uko na ujinga mwingi
 
aseee pole mkúu
 
Usijali boss papuchi imefanya vijana wengi tuwe wajinga
 
Mwaka 2013 nilisafiri kutoka Morogoro nilipokuwa naishi kwenda Tanga Majani mapana kumfata dame wangu mmoja hivi! nilikuwa sijawahi kufika Tanga! Nilifika saa 10 jioni saa moja demu akaja baada ya stori kidogo tu akanambia anaenda home kuweka mambo sawa ili arudi kulala pale gest nilipofikia! baadae simu haikupatikana mpaka kesho naamua kurudi moro! Daah! Frola stasahau kudadeki...
 
Kwenye graduu ya kidato cha 6 nilipanda basi paka Songea.

After there nilimpa simu na laptop ya kufanyia application za chuo na ile pesa ya kulipia TCU nilimpa alipopata chuo akaniacha. The same year nilimnyima mdogo wangu vyote hivyo nilimwambia apambane na hali yake.

Ney popote ulipo bado sijaisahau toshiba yangu.

Karma is....
Ujana uko na ujinga mwingi

Wana Jf bhnaa
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom