Ni sababu zipi zinazopelekea chuo cha teknolojia zanzibar kuweka ada ndogo kwa kozi za ufundi?

Poluyakhtov

JF-Expert Member
May 9, 2017
356
297
Habari za muda wanajukwaa!

Bila kupoteza muda,nimepitia Guidebook ya NACTE kwa upande wa kozi za Engineering na kukuta vigezo na maelezo juu ya ada za kozi tofauti tofauti.

Nimeangalia KARUME INSTITUTE OF SCIENCE AND TECHNOLOGY, ada zake kwa kozi za Engineering ngazi ya Basic Technician,Technician na Ordinary Diploma ni Tsh.529,000 kwa mwaka.

Wakati huo huo Kozi hizo hizo

ARUSHA TECHNICAL COLLEGE zinatolewa kwa ada isiyopungua Tsh.850,000.

Pia kwa upande wa DAR ES SALAAM INSTITUTE OF TECHNOLOGY ada yake haipungui Tsh.1,010,400.

Kigezo gani kinasababisha utofauti wa ada kwa vyuo hivyo?

Nawasilisha.
 
Maamuzi tu ya uongozi wa chuo na sehemu kilipo hicho chuo, yawezekana wanafanya hivyo kwa lengo la kupromote poeple waweze kuvutiwa na mafunzo hayo... ukiangalia Zanzibar ina watu wachache
 
Education quality may play part. Types of lecturers, facilitators, teaching/ learning environments etc.
Mtazamo tu
 
KIST apo ata mimi napashanga sana DIT 850K, ATC 850K, MUST 850K excluding Accommodation and meal and Direct cost Hio ni Tuition fees tu
 
KIST apo ata mimi napashanga sana DIT 850K, ATC 850K, MUST 850K excluding Accommodation and meal and Direct cost Hio ni Tuition fees tu
Mkuu ada DIT ni 1 Million,sijajua kama wamejumuisha na mambo mengine,hao KIST huenda wamefikiria hali halisi ya kiuchumi kwa Watanzania.
 
Zanzibar hawana tamaa mkuu...hapa KWETU KUNA CHUO CHA UBAHARIA(DMI)AISEE wamepandisha SHORT COURSE gharama kwa 40%'' course ya 350000 Mwaka jana... Mwaka huu imekuwa 500000.. Nashindwa kuwaelewa hawa jamaa... yaani wamepandisha course zote kwa ujumla....
 
nimejaribu kufuatilia lakini taarifa nyingi za vyuo vya Tz ikiwemo KIST ni ngumu kuzipata,ingekuwa vema unijulishe matatizo yake mkuu.

Mkuu kama unataka kusoma Engineering, chuo kizuri ni UDSM, maana kinajitosheleza kila kitu, kuanzia Lecturers na facilities zote muhimu. Vyuo vingine huwa na matatizo ya lecturers kiasi kwamba courses huwa zinaendeshwa kwa style ya extreme (Yaani kozi ya semester inaendeshwa kwa wiki mbili kwa kutumia part time kutoka UDSM). Nina uzoefu wa haya mambo, maana nimesoma UDOM na UDSM.
 
Na vipi DIT au ATC?
 
kuna s' bu za msingi zaiDi ila Policy ya chuo Husika, Urahisi uliopo ktk utoaji wa taaluma Husika na namna Chuo kinavyojienDesha..
Pengine S/kali imetia mkono wake zaiDi
 
Back
Top Bottom